Asalaam Aleiykum
Pata fursa nzuri ya kuijua Milango hii minne ya Dhanmbi inayotutesa sisi Walimwengu mpaka tukawa tunaishi bila ya Raha, tunaishi na Maradhi ya Dhanmbi, tunaishi kinyume na sheria za Ulimwengu huu, na sababu kubwa ni kupita kwetu kwenye Milango hii na kuingia kwenye hicho chumba chenye kuishi Dhanmbi.
Vipi tunaingia katika chumba hicho ndio chanzo cha darsa ya leo, Na dhumuni kubwa ni kukufanya usiwe unatumia milango hii kuingia kwenye hicho chumba.Labda tukikuonesha Alama na kukwambia (No Entry)pengine Mja unaweza kuepuka mateso na maangamizi yaletwayo na Dhanmbi.
Dhanmbi ilikujaje?, Ilikuja ili kutizamwa Mwanaadamu utamtii Mollah wako pale utakapo kula tunda la kujua, ndio maana kabla ya kula tunda hili unakua huna dhanmbi, na muda mchache baada ya kula unapata bahati ya kusamehewa, lakini matatizo yanakuja ukenda kuchuma tena au kuendelea kuishi kwenye bustani hii ya Dhanmbi.
Nini Dhanmbi?
Ili usije ukajichanganya kwenye ufafanuzi wacha nikupe tafsiri ya neno dhanmbi, Dhanmbi ni makatazo yote yaendayo kinyume na sheria za Mwenye enzi Mungu, Hapa nimetaja makatazo ili usibabaishwe na tafsiri ya neno Maamrisho, (Maamrisho na Makatazo)ni maneno mawili tafauti.
Naam hiyo ndio Dhanmbi, Sasa vipi unaingia?. ili kujua vipi unaingia itabidi kama ilivyo kawaida yetu tuombe muongozo au tusome aya ndani ya (Quraan) ili itujulishe kitu kilichomo ndani ya Bahari hii ya (Milango Minne ya Dhanmbi), na utakapo pata fahamu za kuelewa sababu zake hapo tena utachukua hatua za kujiepusha au kutumia milango hii ya dhanmbi.
Napenda kukumbusha tena jumba hili japokuwa lina milango minne lakini lina vyumba vingi, kuna vyumba vya Haram ambavyo ndio (Dhanmbi) na kadhalika kuna vyumba vya Halali ambavyo ni (Thawabu) na vyenginevyo. Hapa leo tunashughulika na vyumba hivi vya (Dhanmbi) na aya ya ukumbusho inasemaje kuhusiana na kadhia hii ya Milango.(An-Nisaa-17)
إِنَّمَا ٱلتَّوۡبَةُ عَلَى ٱللَّهِ لِلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَـٰلَةٍ۬ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ۬ فَأُوْلَـٰٓٮِٕكَ يَتُوبُ ٱللَّهُ عَلَيۡہِمۡۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَڪِيمً۬ا
"Toba Inayopokelewa na Mwenye Enzi Mungu ni ya Wale wanaofanya uovu(Dhanmbi)kwa Ujinga, ikisha wakatubia kwa upesi, hao ndio Mwenye Enzi Mungu huipokea Toba yao, Na Mwenye Enzi Mungu ni Mjuzi na Mwenye Hekima".
Kitu cha mwanzo kabisa napenda nikujulishe kuwa daima (Ujinga unambatana na Werevu) aya inayofatia ya (18)ikaendelea na kusema.
وَلَيۡسَتِ ٱلتَّوۡبَةُ لِلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ حَتَّىٰٓ إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ ٱلۡمَوۡتُ قَالَ إِنِّى تُبۡتُ ٱلۡـَٔـٰنَ وَلَا ٱلَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمۡ ڪُفَّارٌۚ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ أَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمً۬ا
"Hawana Toba wale ambao hufanya maovu mpaka mauti yamemhudhuria mmoja wao, Akasema, Hakika mimi sasa natubu, Na (Hawana Toba)wale ambao wanakufa katika hali ukafiri, hao tumewaandalia adhabu iumizayo."
Sasa nini kinatokezea kutokana na meneno yaliyomo kwenye aya mbili hizi, ili kupata faida zake endelea part 2
No comments:
Post a Comment