Asalaam Aleiykum
Nina Desturi ya kumuuliza kila anorejea kutoka (Makka)swali hili, Jee kuna kitu gani kimetokezea kwako wewe ukiwapo huko Makka?. Swali hili nawauliza watu wengi, Masheikh na Maimamu na wengineo wenye kufanya ziara hii ya (Baitul Haram), basi huwa sipati jawabu ila mshangao, wengine wanatetemeka mashavu hawajui wanijibu nini au nimekusudia nini.
Kusudio langu ndio hii zawadi ambayo leo nataka kukupa zawadi hii ya Makka, ili kama umebahatika kwenda, uende ukapate faida za Hajj na Umra kwa ukamilifu. Kuna baadhi ya watu Wanamaradhi ya kuona vyeti, wanapopata bahati ya kusoma maandiko yangu wananiuliza "Cheti" au "Certificate"wajue nimesoma chuo gani, Mpaka naandika hivi, au nakuhadithia mambo ulokua huyajui bado unasisitiza nikupe cheti ndio uridhike, Ukiona unauliza maswali ya nimesoma wapi, basi jielewe bado umo kwenye Jela ya chuo chako au madhehebu yako, au umefungika na Maalim wako au Sheikh wako kwa hiyo unataka na mimi nizungumze au kuongea sawa sawa na Mulla wako.
Toka nje uwe huru, njoo nje kuna maajabu, pata fikra mpya , usikae kuuliza vitambulisho havina faida yoyote na wewe, Wewe soma Mwenyewe hiyo ndio elimu nzuri, nani alokufundisha kusema? Nani kakufundisha kuhema, nani kakufundisha kuona na kusikia, nani kakufundisha kutembea? hizo elimu umezipata na mpaka leo hujamuuliza alokufundisha shahada yake, sio kumuuliza, kumjua humjui. Umeshikilia Mtu lazima akuoneshe cheti, au aje na elimu yake akutie kichwani mwako na wewe ndio uwe umesoma, hiyo ni sawa sawa na kukopia.
Sasa pata zawadi kama hizi zenye kukutoa kwenye kiza na kukupeleka kwenye Nuru, Na huko ndiko niliko soma mimi. Naam katika darsa hii ya Zawadi kutoka Makka Ntakuchukua taratibu ili upate kunifahamu, nakutaka ufungue zawadi hii kwa utulivu uone nini nimekuletea kutoka Makka, Napenda uelewe haya ni mazungumzo baina yangu na wale walio safarini na mimi katika darsa zangu, ni mazungumzo ya Kiroho kwa wale wenye hamu ya kujua maajabu ya Mollah wetu na Alama zake,Ni mazungumzo baina ya viumbe viwili vilojitolea kuujua ukweli kwa njia ya kusema na kusikiliza, kwa njia ya mawasiliano ya kimoyo kwa wale wenye kutumia Akili kwa ajili ya kutafakari.
Ama kwa wale wenye kupanda ndege wakajiendea tu, watabaki kuona Jumba la saa, watahadithia habari za watu na wengine watafika huko na kuendelea kuchat na masimu yao.
Sasa tuanze safari yetu kuelekea Mji Mtukufu wa (Makka)Nitazitia aya za (Quraan) ili upate kufahamu kusudio la maelezo yangu, wala aya hizo hazina mahusiano ya kufungamana na darsa hii, bali ni kukupa wewe msomaji muelekeo au (Dira) Ramani ili unifate kwenye safari hii kwa umakini mkubwa na unielewe kwa ukamilifu.
Aya yenyewe inasemaje? Quraan Israil aya ya mwanzo (1)
سُبۡحَـٰنَ ٱلَّذِىٓ أَسۡرَىٰ بِعَبۡدِهِۦ لَيۡلاً۬ مِّنَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ إِلَى ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡأَقۡصَا ٱلَّذِى بَـٰرَكۡنَا حَوۡلَهُ ۥ لِنُرِيَهُ ۥ مِنۡ ءَايَـٰتِنَآۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ
"Utukufu ni wake Yule ambaye alimpeleka Mja wake usiku kutoka Msikiti Mtukufu (Wa Makka) mpaka msikiti wa Mbali (Wa Baitul Muqaddas)ambao tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake(Tulimpeleka hivyo) ili tumuoneshe baadhi ya alama zetu, Hakika yeye (Mwenye Enzi Mungu) ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona".
Jambo la Mwanzo nikukumbushe huwezi kwenda pahala ila atake Mwenye Enzi Mungu, unaweza kulazimisha ukataka kwenda na kuachiwa uende lakini madhara ya safari hiyo ni makubwa kuliko faida zake, Sasa hapo aya inasema kachukuliwa Mtume s.a.w Kutoka Msikiti Mtukufu(Masjid Haram) mpaka Masjid (Baitul Muqqadas) ili tumuoneshe "Alama zetu" kwa Kupelekwa Mbinguni, pia ikatajwa Kubarikiwa kwa vilivyomo pembezoni mwake. Maneno ukiyasoma kwa makini ni mazito na yanataka uchambuzi wa ndani.
Endelea part 2
No comments:
Post a Comment