Sunday, April 17, 2016

ZAWADI KUTOKA MAKKA PART 2

Asalaam Aleiykum

Huyo alikua ni Mtume s.a.w akipelekwa Mbinguni kuoneshwa Miujiza ya huko, Sasa na wewe umepata bahati ya kwenda kwenye Mji Mtakatifu, Masjid Haram ya Makka, umejaaliwa kwenda kwenye Nyumba anayoabudiwa Mwenye Enzi Mungu, Nyumba ilotajwa kwenye Quraan (Al-Imran aya ya 96)
"إِنَّ أَوَّلَ بَيۡتٍ۬ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِى بِبَكَّةَ مُبَارَكً۬ا وَهُدً۬ى لِّلۡعَـٰلَمِينَ "
Kwa yakini Nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya Ibada) ni ile iliyoko Makka, yenye Baraka na uwongozi kwa ajili ya Walimwengu wote.
Katika Nyumba hii lazima ziko alama hizo za Baraka na uongozi lakini hasara yetu wengi wetu hatuzioni, Waweza kwenda ukaanza kushangaa  na (Al-kaaba) au ukawa unahijji kwenye Jumba la saa, au kutwa unaishia Madukani kufanya (Shopping), au kwa siku hizi inakua umevaa vazi la kuhijji lakini hupo kabisa kwenye hijja au umra wewe umo kwenye kuchat au (Facebook).
Sasa ikiwa kwenye Sala ya Ijumaa Waumin wanakumbushwa "Enyi Mloamini Kukiadhiniwa kwa ajili ya sala ya ijumaa nendeni upesi kumtaja Mwenye enzi Mungu na acheni biashara". Nini habari yako wewe mpita njia tu hapo Makka, mgeni wa Mwenye Enzi Mungu katika Msikiti Mtukufu wa Makka umeshughulika na kuchat na kufanya (Shopping).
Ewe Ndugu yangu unapotia Nia ya kufanya Ibada hii ya Hajj au Umra jifunge upate faida hizi ntazokusimulia ili upate hizo Baraka na Muongozo. Pata kwa ukamilifu Kufanya Ibada zako katika Misikiti hii miwili ya Makka na Madina ukiwa huna shaka ya kufanikiwa.
Kwanza kabisa Ibada hii kabla ya kuianza unatakiwa ujisafishe(tohara)Kwanini ujisafishe?
Quraan sura ya Hajj aya ya 29

ثُمَّ لۡيَقۡضُواْ تَفَثَهُمۡ وَلۡيُوفُواْ نُذُورَهُمۡ وَلۡيَطَّوَّفُواْ بِٱلۡبَيۡتِ ٱلۡعَتِيقِ
"Kisha Wajisafishe taka zao, Na watimize nadhiri zao, na Waizunguke Nyumba ya kale(Al-Kaaba).
Kwa hiyo sasa unajitia Tohara ya Nje ni kule kukoga na Tohara ya Ndani ni kutaka au (Kuomba)Maghfira kwa Wingi. Kuanza kwa nia yako ni kule kujifunga kwa kumtaja Mollah wako na kumkumbuka yeye pekee katika Ibada hii Maalum, Jambo la Pili unatakiwa Ku (Surrender)Unavuliwa Nguo zote na kubakishwa na vipande viwili vya kitambaa cheupe(Ihram) hii kuoneshwa wewe ni (Nothing)ni (Symbolic)sawa sawa na wengine wote, au kujionesha kwa Mollah wako mimi mbele yako sina cheo chochote, kwako sina Mamlaka, niko hapa naitikia ule Mwito wako wa kuidhuru Nyumba yako Tukufu. Na hiyo ndio Nafsi inayotakiwa ya yule alokwenda kudhuru Miji hii ya Makka na Madina, kama inavotaja aya ya (32)
ذَٲلِكَ وَمَن يُعَظِّمۡ شَعَـٰٓٮِٕرَ ٱللَّهِ فَإِنَّهَا مِن تَقۡوَى ٱلۡقُلُوبِ
Namna hivi anaziheshimu Alama za (Dini ya)Mwenye Enzi Mungu , Basi hilo ni jambo katika Utawa (Ucha Mungu) wa Nyoyo.
Shukran zote Mollah wangu unastahiki wewe kwa kunipa Imani na Afya ya Mimi kuja kuabudu kwenye Ardhi hii, Neema zote hizi na Ufalme wa haya yote ni wako wewe Mollah wangu, Na wala huna Mshirika.
Endelea part 3

No comments:

Post a Comment