Sunday, April 17, 2016

ZAWADI KUTOKA MAKKA PART 3

Asalaam Aleiykum

Nakukumbusha wakati unaingia Mji wa Makka kuna mambo yanakutokezea, kwanini sijasema yanatokea?, kwa sababu wewe bado huna (uwezo wa kuyaona)bado huwezi kuwaona majini nao Wakitufu, ndio maana nikasema au kukwambia ujitizame mwenyewe kwenye nafsi yako nini kina kutokezea.
Yasikilize mambo yanotokea, kama wewe ni (Nagative Energy) ambayo ni (Receptive)yenye kupokea, yenye desturi ya (surrender)basi moja kwa moja ukiiona (Al-Kaaba)utajiona unatokwa na machozi, au hali yako unabadilika pengine khofu inakujaa, usiogope kuna kitu kinatokezea, na hali kama hii inawapata hususan Wanawake wanayo Baraka hii ya (Nagative Energy of surrender-)Wanawake wao (Receptive) ndio maana wao rahisi kulia, kwa kuwa pahala kama hapa (Something of beyond happening)kuna kitu kinatokezea, basi ikikukuta hali kama hiyo usiogope jitupe kwa Mollah wako angua kilio cha kweli kweli kuomba kwa Mollah wako tumia wakati huo adhimu usije ukaukosa pengine hutolia tena mpaka unaondoka Mji Mtukufu.
Wala usione haya ukajizuia kugaragara kwa maombi ukawa unaona haya, mbona zamani ulikua ukicheza (dance) chacha, pachanga,(disco)huoni haya, leo uko kwenye nyumba ya Mwenye Enzi Mungu ndio unaona haya. utakapoona unajizuia basi jijue bado huja(Surrender).
Na Kwa wale wenye (Positive Energy of Giver)inachukua muda lakini mabadiliko (Transformation)yanatokea, Na kama umekwenda kwenye Mji huu ikawa hujapata mabadiliko yoyote basi Nakuusia Nenda tena, wewe bado hujenda, utakua umekwenda lakini utakua sawa sawa na wale (Maqureish) waliopo pale, wako chini ya (Al-Kaaba)lakini wameshughulika na biashara(Khamsa Riyal na Punch Riyal) Maskini hawana njia ya kujua kwenye nyoyo zao thamani ya pahala hapo.
Tumo tukiendelea kufungua zawadi yetu kutoka Makka na sasa tunakutana na swali hili la Mshangao, Mbona Makka kuko (active)mbona kumoto, watu wake wakali, wamechangamka, pirika pirika zimezidi?, Watu wote wameshughulika pana nini pahala hapa?.
Nisikilize kwa Makini jawabu yake ili kama na wewe utakwenda au kuna Mtu anakwenda umueleweshe mambo yalioko huko, kwanini ikawapo hali kama hiyo, Inapaswa ikumbuke pahala popote anapoteua Mfalme wa Mbingu na Ardhi basi sehemu hiyo inakua Takatifu, na eneo hilo lazima liwe liko katika jinsia ya (fire) au Moto, kuna mkusanyiko wa Majini na Malaika hapo. Ndio Maana utaona katika Safari ya Miraji Sydna Jibril a.s alimwambia Bwana Mtume s.a.w kuna sehemu mimi sifiki, nenda peke yako, (Lazima ipatikane Transformation fulani)Na hapo Makka kuna hilo Jiwe la (Hajral-Aswad)Ndani ya (Al-Kaaba), jiwe lilotokea Mbinguni ambalo hutokezea miujiza, ita utakavyo (Power, Energy)  lakini elewa hapo kuna kitu chenye kuwafanya wengine warukwe na akili, wengine wasihisi chochote, wengine hata wasione hiyo Kaaba, wengine wapate uongofu na  kama ilivompata Nabii Musa a.s, angalia nini kilimtokezea yule Msemezwa na Mollah wake.
Sura ya Taha aya ya 10.
إِذۡ رَءَا نَارً۬ا فَقَالَ لِأَهۡلِهِ ٱمۡكُثُوٓاْ إِنِّىٓ ءَانَسۡتُ نَارً۬ا لَّعَلِّىٓ ءَاتِيكُم مِّنۡہَا بِقَبَسٍ أَوۡ أَجِدُ عَلَى ٱلنَّارِ هُدً۬ى
Alipouona Moto, akawaambia watu wake (Alokua nao) Ngojeni, hakika nimeona moto, huenda nikakuleteeni kijinga katika huo(Moto)au Nitapata muongozaji katika moto huo.
Nabii Musa a.s kasema maneno mawili inatubidi tuyazingatie sana, la kwanza kasema huenda nikakuleteeni kijinga(ambacho hakina maana)au nitapata muongazaji. Sehemu yoyote Takatifu ukenda kumbuka utarudi na mambo mawili huenda ukarudi na (Kijinga)maneno mengi, habari chungu nzima, au utarudi umebadilika umepata uongofu kwa hiyo Tahadhari.
Ukirudi na habari ndio itakua Al-kaaba iko hivi, Jabal Nur liko vile, lakini ukirudi na Muongozo huna hadith, unakaa kimya, ukifunga macho ufunuo unakujia, vikija vishawashi unakua mwepesi wa kuviepuka, huku unasikia watu wanasema, karudi Makka siku hizi hachezi tena Ngoma, na hivi na vile.
Basi alipofika Nabii Musa a.s alijaa khofu alikuta Moto unawaka lakini hauunguzi chochote, akaambiwa vua viatu sasa uko kwenye Jangwa Takatifu la (Tuwa) na kilicho endelea hapo ni (History of ten commandments). Na hali kama hiyo inakutokea wewe ukifika katika Sehemu Takatifu, lakini pengine ukhisi kwa mizigo ya Dhanmbi ulobeba, au moyo una kutu bado hujajisafisha.
Nabii Musa a.s kuanzia hapo akapata (Transformation)akapewa (Wahyi)awapelekee mayahudi, Mayahudi wakanyanyuliwa kuanzia hapo kwa darja, Na kutokea hapo kwenye Mlima wa sinai na Makka sio masafa marefu,  Mtume Mohammad s.a.w akapewa Utume kwenye hilo Jabal Nur, akateremshiwa Quraan napo si mbali na hiyo Baitul Haram(Al-Kaaba)Na Maqureish nao wakanyanyuliwa na hizo Baraka zilzopo pembezoni(Mafuta Nk).
Ama kuhusu Madina hapo kuna (Receptive Energy), hapo ndipo alipozikwa yule ambaye ndani ya mifupa yake imepita hii Quraan, yule ambaye alipelekwa Mbinguni kwenye usiku Mmoja kuoneshwa miujiza ya huko, yule ambaye aliyeiona (Lailatul Qadir)akapata (Enlightement) baada ya Miaka 1400 (Energy)yake imebakia au Wasila unofanya Mji huo kuwa wa (Peace)kuwa wa (Surrender)Na kwa ajili hiyo kila anokwenda kwenye mji huo anapata kuhisi tafauti hiyo. Na kama hamjui siri iliyopo kwenye Mji huo wa Madina hebu waulizeni (Wa-Hindu)mbona nyote mkifa mnachomwa moto isipokua akifa (Sheikh)wenu hamchomi moto kwanini? jawabu lake linaweza kukusaidia kupata kujua hali ya utulivu unayokutana nayo Madina. Hapo ndipo alipolala yule aloaminiwa na Billion ya watu ulimwenguni kote, yule Mwenye kutajwa kila siku mara tisa. leo umehudhuria katika Mji alozikwa lazima upate (Experience) ya (Energy) inoendelea kumiminika kwenye Mji huo wa Madina, basi ukifika kakae Msikitini kwake upate shufaa, upate Faraja na Umasalimie Mtume wako bila ya woga.




No comments:

Post a Comment