Asalaam Aleiykum
Kila jambo katika Ulimwengu huu lina mwenza au (Pair)yake(Mfano)Usiku na Mchana, Mwanamke na Mwanamme, Ardhi na Mbingu, Baridi na Joto, Uhai na Mauti, na mengi mengineyo ya kila aina katika Ulimwengu huu, Inatajwa habari hii katika Quraan sura ya (adh-Dhaariyat aya ya 49)وَمِن ڪُلِّ شَىۡءٍ خَلَقۡنَا زَوۡجَيۡنِ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ
"Na katika kila kitu tumeumba Dume na jike ili mpate kufahamu
. Leo Hapa Nakuchukua katika Ulimwengu wa Ndani na Mwenzie Nje, Nisije kusema Ndani na nje ukaanza kukimbilia kwenye Nyumba, leo sio kusudio lake hapa, Nilokusudia kukufahamisha hapa ni ile Ndani ya Maumbile yako ambayo unayo ishi.
Katika Ufalme wako wa Fahamu (Conscious) Una athari mbili ambazo unazozitumia za ima kwenda nje au kubakia ndani, (Mfano)Katika matendo ya kubakia ndani unaweza kuficha siri katika kifua chako, unaweza kufuga chuki, unaweza kuzuia hamaki, unaweza kuota ndoto usimwambie mtu, kuna mambo chungu nzima unaweza kuweka katika kifua chako ikawa mtu yoyote hajui isipokuwa wewe na Mollah wako ndio wenye kujua nini umekificha katika kifua chako, huko ndio ndani nnapo kusudia katika darsa hii ya leo, huko ndiko kwenye mahusiano na (Akhera) Na kule nje unako kwenda kutembea ni huku kwenye makelele, kwenye karata, kwenye kushea (Joke) kwenye Mazungumzo, kwenye magonvi, kwenye maasi, kwenye husda choyo na chuki, kwenye fujo zote za maisha na harakati za (Dunia) huko ndio nje ambako pia ntafahamisha madhara yake.
Kama kawaida yangu ntaichukua aya 4 zilizomo mwisho wa kwenye Sura ya (Fajir) ili itupeleke katika safari hii ya ndani na nje, Hapa itabidi mnisamehe nianze safari hii kutokea ndani kwenda nje ili tupate faida zote mbili.
Kwanini nikaanza Ndani kwa sababu hiyo ndio (Nature)yako, huko ndiko unakotokea, nje unakua umepotea.
Basi kabla ya kuzichukua aya hizo za mwisho za sura ya (Fajir)wacha nikuonjeshe aya ili ikubebe katika safari hii ya ndani akhera na nje duniani ili upate kufahamu vizuri.
Quraan aya ya 20(Ash-Shura)
مَن كَانَ يُرِيدُ حَرۡثَ ٱلۡأَخِرَةِ نَزِدۡ لَهُ ۥ فِى حَرۡثِهِۦۖ وَمَن كَانَ يُرِيدُ حَرۡثَ ٱلدُّنۡيَا نُؤۡتِهِۦ مِنۡہَا وَمَا لَهُ ۥ فِى ٱلۡأَخِرَةِ مِن نَّصِيبٍ
"Mwenye kutaka Jaza(Malipo)ya Akhera tutamzidishia katika jaza yake hiyo, Na anayetaka jaza ya dunia tutampa, Lakini Akhera hatakuwa na sehemu yoyote ile ya kheri".
Natoa msisitizo amkeni usiku msali na ikisha msome Quraan, au nyakati za alfajiri ili upate ushuhuda au ufunuo wa maneno haya mazito yaloteremka katika dini hii ya Uislam.
Aya imeanza Mwenye kutaka jaza, mimi nikasema neno(Malipo)kwa ukweli sio malipo umefanya nini hata ulipwe, lakini ili unifahamu ndio nikasema neno (malipo)lakini aya imesema Jaza, na Jaza ikatiwa neno tutamzidishia, ina maana unayo tayari, ila ukitaka jaza ya hiyo Akhera utazidishiwa, kivipi? na vipi utataka? Jaza ya kutokea upande wa pili wewe unayo, kama afya njema, furaha, unalala na kuamka, umepewa mke au umepewa mume, ndio aya ikasema tutamzidishia, kuzidishiwa hapa ni kule kupewa kwako katika hayo maeneo mawili ya (Akhera na Duniani) na kutaka kwako ni huko kufanya (Taqwa)ndio aya ikasema tutamzidishia(Ndani kiko na nje unaongezewa).
Na huyo Mwenye kutaka vya Dunia pia na yeye tutampa, hapo aya imebadilika, mwanzo utazidishiwa, sasa imekuja na neno tutampa, kupewa maana yake huna, unapewa, kupewa ni kwa muda, mara unanyanganywa, mara kinamalizika, mara ulikua tajiri na sasa umekua masikini, huko ndiko kupewa, halafu ukaambiwa ukipewa ujue Akhera utakua huna kitu, kwa sababu kupewa ni kwenye Dunia(Temporary), na dunia ni yenye kukusahaulisha na kila kitu chenye mahusiano na Akhera. Ndani Akhera nje Duniani.
Endelea Part 2
No comments:
Post a Comment