Asalaam Aleiykum
Unasoma aya hizi jitahidi usipite kama (Kasuku)utakua hupati maana, au utakua unapata tafsiri zako za kichwani halafu unajijibu (Imefanana) isikilize aya inasemaje, zama uitizame inakwambia nini?subiri ikufungulie miujiza yake. Kama ipi?
Quraan (Fajir 27)"يَـٰٓأَيَّتُہَا ٱلنَّفۡسُ ٱلۡمُطۡمَٮِٕنَّةُ "
"Ewe Nafsi" Kwanini ikatajwa nafsi na sio Mwanaadamu, Kwanini isisemwe ewe Kiumbe, Unajua maana yake?. Ni kwa sababu ya kukuonesha ishara ya kitu fulani muhimu, kukufahamisha kuwa kuna siku utavuliwa hilo guo ulilovaa(Body)Mwili, kwamba kuna siku utarejea kama (As Pure Being), Wacha kudanganyika na Ndevu, Nywele, uso mzuri, mara umetia (Make-up)vyote hivyo sio wewe, wewe nani?.
Wewe ndio hiyo Nafsi inayoitwa hapo juu au kwa jina jengine (Roho), Katika huo Mwili wewe unaishi kama unavoishi kwenye nyumba yako lakini bado hujijui.
Naam sasa kwanini ukaitwa Mwenye matumaini?, Neno hili asili yake limezaliwa katika mzizi wa neno (Tumaanin)likimaanisha utulivu, Nini utulivu? Utulivu ni (Peace)Amani, Na hiyo Amani ina njia mbili kupatikana kwake, ya kwanza inakua umeridhia hali yoyote ulo nayo, Na ya pili ni ile hali ya kupigana vita au kushindwa na kitu au jambo hapo tena ukawa huna hila au wala njia ila ku(Surrender).
Nini (Surrender)? Kiarabu (surrender) ndio hiyo (Islam). Kwa hiyo hapo unaitwa "ewe Nafsi ulo (Surrender) ukawa Muislam wa kweli, baada ya kugundua au kufahamu yakua mbio zako zote za Nje(Duniani)hazina faida na wewe, Wizi, Uzinifu, Choyo,Tamaa,Hasada,Hamaki,Chuki,Uongo,Ugonvi,Jeuri,Fitina,Uadui, ukaona vyote hivyo sasa havina faida na wewe, na umekua ukivifata Nje(Duniani)kwenye Umri wako wote na havijakupa ila madhara na mashaka matupu.
Vipi Mambo ya kidunia yana mashaka, hapa itabidi nikupe mifano ili upate kunifahamu kwa uzuri. kila kitu katika Ulimwengu huu kiko (Pairs) na mwenzake, Kama (Chungu mwenzie Tamu)Raha mwenzie Maumivu, kucheka Mwenzie kulia, sasa ukiangalia kwa undani utajua hakuna hata siku moja ukapata chungu ikawa chungu pekee, lazima kuna wakati utaonja tamu, hiyo ndio hukumu ya Ulimwengu huu vitu viko(Pair's). Sasa utakapogundua hayana faida kila siku mara chungu mara tamu unateseka tu, ukilielewa hilo hapo wewe ndio unakua tayari ushajiandaa kuanza (Jihad ya Nafsi).
Utajiuliza nini Jihad Nafsi?Mimi ntakujibu au Utajibiwa na quraan kama utaifahamu, Jihad ya Nafsi maana yake bakia ndani(Akhera)usende Nje (Duniani).
Niliposema mimi ntakujibu kwa sababu mimi rahisi kunifahamu, tunaongea lugha moja, Lakini Quraan ni maneno mazito "Siku zote inakwambia hichi haramu na hichi halali, unaacha vya halali na unafanya vya haramu", jee hapo unaifahamu. Sasa vipi ubaki Ndani? na Kwa nini ndani nikaita Akhera.
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment