Asalaam Aleiykum
Kitu cha mwanzo itabidi ukitafute nini kinacho kushawishi utoke Nje(Duniani) kinachokupa ushawishi huo hakuna chengine isipokua hiyo Akili yako(Mind)inakupa amri zote kwa njia ya (Memory)"Wewe Bwana unageuka Mtwana", Sasa vipi unakwenda Nje, Ni kwa ajili ya fikra zako, zimekutawala na mambo ya Nje, itizame (Mifano). Fulani atasemaje, Kajenga vipi mimi nishindwe, Mbona kahamaki, Kwanini anavaa vizuri mimi siwezi, Kuna siku ntawakomesha, Mbona kanicheka, Utajiri kapata wapi,nikimpata atanikoma, vipi nimuibie, kutwa nzima wewe ni Mwenye kuishi nje kwenye Madhanmbi, Ndio maana "Bwana Mtume s.a.w" Akaashiria kwenye kifua akihimiza watu warudi ndani kwenye (Taqwa).
Taqwa au Ucha Mungu uko Ndani, huko nje mnako kimbilia ni dhanmbi tupu. Kwa hiyo aya ya 28 inaendelea kwa kusema.
ٱرۡجِعِىٓ إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً۬ مَّرۡضِيَّةً۬
Rudi kwa Mollah wako hali yakua utaridhika na (Mollah)wako aridhike na wewe. Watu wengi wanadhani usubiri mpaka mauti yamehudhuria ndio urejee, marejeo yalokusudiwa hapa ni yale ya (Taqwa)Ucha Mungu.Urejee uwe unaishi ndani(Akhera)vipi utarejea huna taqwa, hujatenda mema, vipi wewe utarejea na mijidhanmbi yako, kinachotakiwa hapo urudi ungali uko hai, Na kurejea ukiwa hai ni huko kuishi ndani, vipi utarudi kwa Mollah wako?, Wanojua hawaulizi swali hili kwani wanajua hiyo Roho imetokana na yeye, kwa hiyo ukirudi ndani unakutana na Mambo ya Akhera, na huo ndio Ucha Mungu.
Unarejea Vipi? Pata habari hii ndio iwe ngao yako, iwe ndio sababu ya kubadilika kwako, wepi wanorejea kama huwajui wacha nikujulishe ni hawa hapa.ٱلَّذِينَ يَذۡكُرُونَ ٱللَّهَ قِيَـٰمً۬ا وَقُعُودً۬ا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمۡ وَيَتَفَڪَّرُونَ فِى خَلۡقِ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ رَبَّنَا مَا خَلَقۡتَ هَـٰذَا بَـٰطِلاً۬ سُبۡحَـٰنَكَ فَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ
"Ambao humkumbuka Mwenye enzi Mungu wakiwa wamesimama na wakikaa na wakilala, Na hufikiri umbo la Mbingu na Ardhi,(Wakasema)Mollah wetu hukuviumba hivi bure, Utukufu ni wako,Basi tuepushe na adhabu ya moto."
Hao ndio wenye kuishi ndani, Ukiishi ndani unakua huna mawazo mengine isipokua kumkumbuka Mollah na hiyo ndio (Taqwa) Na huko ndani ndio unaipata hiyo (Tafakuri)huko ndio utakapofunguliwa mambo ukaijua yakini kuwa kweli hakuumba vitu hivi bure, na huko ndani ndiko utakapogundua kweli Moto upo na utaomba uepushwe nao, inayotakiwa ni hiyo (Tafakuri) nini Tafakuri,ni hali ya kwenda (Beyond mind) unayoipata ukiishi ndani.
aya inasema "Rudi utaridhika"(Umeridhika)kuridhika kwenyewe ni huko kukaa ndani, ukawa hutaki mali, hutaki umaarufu, hutaki Uadui, hutaki Uongo, Hutaki wanawake au wanaume, hutaki siasa wala kumchukia mtu, hutaki mambo yote ya kipuuzi yaliyopo nje(Duniani).
Ukisharidhika ikawa umekubali hali ulo nayo, na ukawa kiukweli hutaki tena vilivyopo nje, Basi (automatic)unabakia ndani(Akhera), Na kubakia ndani hakuna chengine isipokua unakutana na Taqwa,(Kamailivotajwa katika hiyo aya hapojuu), Na kumbuka wewe ukiridhika kikweli basi haichukui muda hapo hapo Mollah wako na yeye anaridhika na wewe.
Unageuka kuwa mtu wa aina nyengine kabisa, Unapata mambo mengine kabisa sio ya Ulimwengu huu, kwa sababu ndani hakuna kawaida unayo ifahamu wewe ya tamu na chungu, Raha na maumivu, ndani unakwenda (Beyond)kukutana na kitu kiitwacho(Bliss)ndio mwanzo wa darsa aya ikasema"Unazidishiwa"kama utataka vya Akhera, hiyo (Bliss) siwezi kukuhadithia inabidi uende ndani Mwenyewe ukaonje, lakini shuruti lake kwanza lazima uridhike, ikisha ndio upewe zawadi hiyo ikaayo ndani.
Halafu tena aya ya 29 inaendelea kwa kusema.
فَٱدۡخُلِى فِى عِبَـٰدِى
Basi ingia katika waja wangu.
Hapo sasa kuna mabadiliko (Mwanzo ilikua Nafsi) na sasa unaitwa kwa jina la (Abdi)Mja, Sababu hiyo Roho ni yenye (Bliss) tupu ili ku(Enjoy)au ku (Experience)unahitaji(Body)"Kutokana na hiyo Ardhi nyinyi tumekuumbeni, tunakufisheni na kukufueni kwa mara nyengine tena"Kwa hiyo sasa unaitwa Mja ili uwe katika waja wake ambao hawakutajwa wepi, na sababu kubwa wako wa aina nyingi, inategemea na Ucha Mungu wako na daraja uliyonayo kwa Mollah wako, kuna Ibad Swalihunna, Muhsinuna,Muslihunna,Muttaqinna, na wengi wengineo, kwa hiyo sasa na wewe unaitwa ukiwa Ume(Surrender)na daraja yako utaijua ukiingia ima ndani au kama aya inavomalizia.
وَٱدۡخُلِى جَنَّتِى
Ingia Peponi
Kumbuka huko ndani ndio kwenye hiyo Pepo. Na kwanini urudi kwa sababu mwanzo ulikua huko peponi(Hukumbuki kisa cha Baba yetu Adam)mwanzo tulifukuzwa humo peponi na sasa unaambiwa umesamehewa na Mollah wako karidhika na wewe, kwa kuwa umetubu, umeacha uliyokua ukiyapenda kwa ajili yake, na wala hurejei tena. Basi ukiwa umelijua hilo nakutaka utambue mwanzo rejea ndani upate hiyo (Taqwa)ikisha utaupata huo mlango wa kuingia peponi, hiyo ndio maana ya Ndani(Akhera)Taqwa, na Nje(Duniani)Dhanmbi. Basi mpaka unasoma darsa hii najua bado uko nje, kwa hiyo una hiyari yako ima kuingia ndani au kubaki nje.
No comments:
Post a Comment