Sunday, October 2, 2016

MWANZO MAPENZI MWISHO MAPENZI PART 1

Asalaam Aleiykum

Siku zote inasomwa aya hii inosema:
وَإِذَا قُرِئَ ٱلۡقُرۡءَانُ فَٱسۡتَمِعُواْ لَهُ ۥ وَأَنصِتُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ
Na isomwapo Quraan isikilizeni, Nyamazeni ili mpate kurehemewa.
Watu wengi wamepata tafsiri tafauti na kusudio ya aya hii, wengine wanadhani kurehemewa hapo ni kupewa mali, au kupewa utajiri, na hili limetokana na Akili zetu kuzihusisha sana na mambo ya kipato, au biashara, ukifanya hivi utalipwa vile, Mwanaadamu unakua hupo kabisa unaambiwa kitu chengine unafahamu kitu chengine, Unaambiwa lete (Kawa)unaleta kahawa, huko kabisa mawazo yapo kwengine, ndio maana mkaambiwa itakaposomwa isikilizeni, halafu nyamazeni, kwanini yakasemwa maneno hayo kwa sababu kusikiliza ni jambo jengine na kunyamaza pia ni jambo jengine, lazima uyaunganishe mawili haya ndio unaipata hiyo Rehma, unaipata hiyo Fahamu, lakini kama hujayaunganisha mawili haya matokeo ndio yanakua hayo ya (Kawa na Kahawa).
maana ya kusikiliza ni tendo ambalo huna (Miliki nalo)unasikia kila jambo, lakini maana ya kunyamaza ni kuwa unakua (empty) katika (Mind)yako, kimya unasikiliza kitu hususia, na hapo kitu chenyewe ni hayo maneno ya ndani ya Quraan, na Rehma yenyewe ni hiyo fahamu, lakini wale wenye kusikiliza bila ya kufahamu inakua Rehma haifiki, unaishia kupenda sauti, unaishia kupenda anavosoma, hasara ilioje kuikosa Rehma ya kitabu cha Mwenye enzi Mungu. Bwana Mtume s.a.w anaambiwa nini?(Muzzamil aya ya 5)"إِنَّا سَنُلۡقِى عَلَيۡكَ قَوۡلاً۬ ثَقِيلاً ".
"Hakika sisi tutakuteremshia kauli nzito".
Sasa maneno yashateremka unaambiwa tulia uyasikilize ili urehemewe, kurehemewa kwenyewe kukoje, kuko hivi, katika kupewa Sheria na Muongozo, kupewa Dawa ndani ya maneno hayo, kujazwa Imani katika nyoyo yako, na mengi yalojificha makubwa makubwa ambayo huyajui, na ndio ukaambiwa tulia ufunguliwe mambo, poa upewe maana, wacha kelele upewe code za mambo zimo ndani ya Quraan, lakini wapi, nani anaye sikiliza, wangapi wenye kuipata maana ya ndani ya Kitabu hichi, hutowakuta ila wachache sana.
Sasa vipi utajua kuwa Rehma imekuteremkia?Pale itakaposomwa aya ima iwe kwenye Sala au venginevyo, Na wewe ukawa nje unasikiza ndani umetulia hakuna hadith za ajabu zinaingia mawazoni, hakuna biashara unafanya kwenye Akili, ndio pale itakaposomwa aya mfano wa hii sura ya (Rumi aya ya 21)
وَمِنۡ ءَايَـٰتِهِۦۤ أَنۡ خَلَقَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَٲجً۬ا لِّتَسۡكُنُوٓاْ إِلَيۡهَا وَجَعَلَ بَيۡنَڪُم مَّوَدَّةً۬ وَرَحۡمَةً‌ۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ 
"Na Katika Ishara zake(Za kuonesha Mapenzi yake juu yenu)ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mupate utulivu kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu, Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofikiri".
Mwanzo Mapenzi Mwisho Mapenzi.
endelea part 2


MWANZO MAPENZI MWISHO MAPENZI PATR 2

Asalaam Aleiykum

Sasa swali la kujiuliza au kutafakari ni hili iwapo pamesemwa "Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu" nini habari yetu sisi kuhusu haya maisha yote tunayoishi katika "Ulimwengu huu", ukenda (Deep)Ndani kabisa utagundua kule Kuumbwa kwenyewe kwetu sisi kumetokana na Mapenzi ya Mollah wetu, kwani hujasoma aya iliyomo kwenye sura ya (Insaan aya 1)
هَلۡ أَتَىٰ عَلَى ٱلۡإِنسَـٰنِ حِينٌ۬ مِّنَ ٱلدَّهۡرِ لَمۡ يَكُن شَيۡـًٔ۬ا مَّذۡكُورًا 
Hakika ulimpitia Mwanaadamu wakati mrefu katika dahari, hakuwa katika kitu kinachotajwa.
Hali kama hiyo wewe inakuhusu, Jikumbushe pale wazee wako wawili walipofanya maridhiano ya kufunga ndoa Mapenzi yakawateremkia na kukutana katika godoro la mapenzi, nini kilitokezea, kilotokezea hapo ni hiyo (Rehma)ambayo ni wewe, na ndio hiyo(Product of Love).
إِنَّا خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَـٰنَ مِن نُّطۡفَةٍ أَمۡشَاجٍ۬ نَّبۡتَلِيهِ فَجَعَلۡنَـٰهُ سَمِيعَۢا بَصِيرًا 
"Kwa Hakika tumemuumba Mwanaadamu (Mtu)kutokana na mbegu ya Uhai iliyochanganyika,(Ya Mwanaume na Mwanamke)Na Tukamfanya Mwenye kusikia na kuona."
Kwa hiyo Wewe ni matunda ya mapenzi, ndio maana wakati mwengine unajihisi mapenzi na wakati mwengine umejaa chuki, (You are Both)Kama utatafakari utaziona hali zote hizo mbili zikikutokezea, yaani una urithi wa jinsia zote mbili, unageuka wakati(mara mama yako, mara baba yako)Jiangalie.
Nini cha kuangalia zaidi kitachokupa Afya na Furaha ni ile hali ya kukumbuka kuwa wewe ni (Full of Love) hiyo ndio (Nature)yako, ukiona mambo ya chuki, ufisadi unakuzungukia toka haraka sana katika hali hiyo, na hiyo ndio itakua dawa yako.
Kwani wewe hukumbuki Umelelewa kwa mapenzi, umeshawahi kujiuliza chanzo cha mapenzi hayo kimetokea wapi?. Majibu yapo kwenye sura ya (Taha aya ya 39)"وَأَلۡقَيۡتُ عَلَيۡكَ مَحَبَّةً۬ مِّنِّى وَلِتُصۡنَعَ عَلَىٰ عَيۡنِىٓ "Na nimekutilia Mapenzi yanaotokana kwangu, na ili ulelewe machoni mwangu, (Maneno hayo anaambiwa Nabii Musa a.s lakini kila mmoja wetu alopita kwenye Ulimwengu huu yanamgusa." Na hivi ndio kila mmoja wetu anavolelewa kwa mapenzi makubwa, Analelewa mtu kwa bawa la huruma, wazazi hawalali usiku kucha, ukiumwa wanahangaika ili wakupe dawa upone, ikisha ukitimia umri wa kuweza kutembea na kujitegemea Mwenyewe hapo wanakuacha kwenye uangalizi wa miujiza utokao kwa Mollah wako.
إِن كُلُّ نَفۡسٍ۬ لَّمَّا عَلَيۡہَا حَافِظٌ۬ 
"Hakuna Nafsi yoyote ila inayo mchungaji juu yake".
Ulipofika Umri wa kuachiwa huru unapata ulinzi mwengine wa yule aliyeumba mapenzi na kukuletea mchungaji(Malaika)unaambiwa kwa njia usizofahamu hapa usende, kule usipite, gari hii usipande, unanusuriwa na kila mabaya na mabalaa pasi na wewe kuyajua, yote hayo yanafanyika ndani ya kivuli cha mapenzi, "ewe binaadamu upendwe vipi ujijue unapendwa".
Mwanzo Mapenzi Mwisho Mapenzi.
Endelea part 3


MWANZO MAPENZI MWISHO MAPENZI PART 3

Asalaam Aleiykum

Unapofikia kubaleghe au ujanani sio kuwa mapenzi hayo yanasita bali yanaendelea japokua unapita katika dhoruba za uharibifu wa maasi, unafanya ya kufanya bado mapenzi yanaendelea kumiminika kutoka kwa  wazazi wako na kwa Mollah wako.
 Ukiumwa Mollah wako anakuponesha, Anakupa riziki na mengineyo, huku wazee nao wanataabika kwa mapenzi wakitaka ushike njia ilonyooka. Kwa mapenzi hayo ukapambiwa Ulimwengu huu kila jambo zuri, ukatiliwa furaha ambayo unaishi nayo, jiangalie wewe ukiwa mgonjwa unaweza kuwa na furaha, ndio maana ukaambiwa unapewa Uhuru wa kuchagua ama shukuru kwa mapenzi haya au kufuru.
Vipi kushukuru?, jee unamkumbuka aliyekupa na kukufanyia mapenzi haya, una (share)mapenzi haya na wenzio, kwa kile unachopewa unakitoa, unaonea huruma wenzio, ama ukenda kinyume na hayo ndio huko kukufuru. Na kukufuru ni hiyo njia ya mateso, njia ya chuki, kwa ajili ya mapenzi ya Mollah  wetu anatusubiria  na kutuacha tuishi katika enzi yake ya mapenzi, ama wale wenye (gratitude)waloridhika na mapenzi ya Mollah wao, wao hawana shaka, wameridhika kwa kuumbwa kwao na kila walichopewa, Na kila linalokuja wako tayari wakijua linafanyika kwa ajili ya mapenzi ya Mwenye enzi Mungu, hakika walokufuru ni wale wenye kuyakataa mapenzi haya, wale wasoridhika na (Qadara) ya Mollah wao.
Na kwanini hawaridhiki hali wanapewa kupumzika wakichoka(Usingizi), wakishapumzika wanaamshwa ili waendelee na harakati za maisha, wakishikwa na njaa wanapewa chakula na riziki zao nyengine, wakishikwa na Kiu wanapewa maji, wanapewa uwezo wa kuona na kusikia, wakiumwa Mollah wao anawaponesha, Na ukizidi kumuasi husema asaa hawa viumbe wangu huwenda pengine wakarudi, lau ingekua si mapenzi ya Mollah wetu basi tungeangamia. Chukua mfano unamuasi Mollah wako kwa kulewa, "Tena unaimba ningekua na Pajero ningelewa Tirarira"Unalewa tirarira"Unaendesha Pajero lako, unafika nyumbani kwako Mollah wako anakutoa kwenye Pajero kwa usalama bila hata kuchuna kioo, unakwenda kwenye kitanda unalala na kuamka salama, basi hujijui kiumbe wewe kwamba unaishi ndani ya (Being of Love)Mapenzi.Na kila ukipindukia ukawa huogopi, na umefika katika umuri wa Utu uzima bado upo kwenye vilabu vya pombe, hutoki kwenye vikao vya Taarab, unaendelea kufanya maasi, Mollah wako anakwita kwa njia ya mapenzi, vipi?
قُلۡ يَـٰعِبَادِىَ ٱلَّذِينَ أَسۡرَفُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ لَا تَقۡنَطُواْ مِن رَّحۡمَةِ ٱللَّهِ‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَغۡفِرُ ٱلذُّنُوبَ جَمِيعًا‌ۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ
"Sema "Enyi waja wangu Mlojidhulumu nafsi zenu msikate tamaa na Rehma ya Mwenye enzi Mungu, bila shaka Mwenye enzi Mungu husamehe dhanmbi zote, hakika yeye ni Mwingi wa kusamehe(Na)Mwingi wa kurehemu."
Kusamehe pekee mapenzi, kurehemewa ndio huo upole(Kindness)kunusuriwa na adhabu, mpaka Mwisho wa maisha yenu mapenzi yanakufateni, rehema zinakufateni, unachotakiwa ni kugeuka kidogo ukajiunga na hiyo (Gratitude)ili uwe katika walofuzu, jiunge na mapenzi ya Ulimwengu huu ili nawe uwe Mcha Mungu.
Sasa ikiwa hapo juu umeambiwa usikate tamaa hapa chini inafatia aya nyengine zilizomo kwenye sura ya (Fajr 27 mpaka 30)"Zina kuita kwa jina jengine, kule uliitwa (Abdi)hapa kwenye sura hii unaitwa Ewe Nafsi"uliyetua, Nafsi iliyotua ni ile yenye matumaini, Nafsi ambayo imekiri makosa yake na kukubali mazuri yake, ikarejea kwa Mollah wake hali ya kujua ima imefeli mitihani yake au imepasi, Na kwa ajili hiyo haina nafsi uwezo wa kufanya lolote ila kumuachia Mwenye enzi Mungu mwenye mapenzi ya kiumbe chake kumsamehe na kumuingiza na kumuweka na  waja wema peponi.
Nini Matumaini?Matumaini ni (State of Gurantee)Ni hali ya kujiridhisha kisaikolijia, Kwa sababu hakuna Mwenye (Gurantee) isipokua kutoka kwa Mollah wako uliyopewa kwenye kitabu, na ukifikia mpaka kulijua hilo ina maana na wewe umo, unatakiwa katika safari hiyo, ambayo hakuna ajuae unakwenda wapi? nini kinatokea ukishafukiwa kwenye dongo, hesabu zako zimefichwa, pepo imefichwa, Moto umefichwa, Lakini kwa Mapenzi ya Mollah wetu matumaini kayaweka wazi, basi usikubali mtu yoyote ayachukue, sababu Mwenyewe alokuumba anakwambia rejea kipenzi changu, kwa sababu kutokana na mapenzi yangu wewe nimekuumba, kutokana na mapenzi yangu leo nakuchukua urejee nyumbani ulikotokea ndio maana umeitwa kwa jina la Nafsi, (sio Abdulla au jina jengine wewe Nafsi)leo rudi umeishi pengine kwa raha au dhiki, umeishi na maradhi au furaha basi rejea nyumbani uje kupumzika kama unavopumzika (Ukilala). Tena ondoa khofu ukiwa peke yako utakua (Boring)wewe unapenda (chit chat)kuzungumza basi ingia ukakutane na waja wema, hakuna mazungumzo ya kipuuzi tena huku ujako. Mwanzo Mapenzi mwisho Mapenzi, na kama utataka kinyume cha hayo Mapenzi ndio hiyo Dhiki tupu, mara wasiwasi, mara maradhi, mara hasira mara chuki, mara umehamaki, mara umenuna, Binaadamu jihadhari sana na kujitia maradhini, jitahidi kuyalea mapenzi na ndio hiyo (Taqwa).
Sasa utayajuaje hayo mapenzi? Mapenzi yenyewe ni haya maisha, Maisha ni zawadi kubwa Mwanaadamu alopewa na Mollah wake, ambayo unatakiwa uithamini. Jitahidi sana wakati unaishi kwenye Ulimwengu huu ishi na watu kwa mapenzi, ona raha kuwa umeamka mpaka unalala hujamkera Mollah wako, hujakera viumbe wenzako, hujaua hata kinyama, umeabudu kwa utulivu, ukiimaliza siku kwa njia hiyo jijue umo kwenye mapenzi, na hayo ndio matumaini ambayo yanakupa (gurantee)Bila ya khofu. Omba sana msamaha kwa ili uwe Mapenzini.