Asalaam Aleiykum
Unapofikia kubaleghe au ujanani sio kuwa mapenzi hayo yanasita bali yanaendelea japokua unapita katika dhoruba za uharibifu wa maasi, unafanya ya kufanya bado mapenzi yanaendelea kumiminika kutoka kwa wazazi wako na kwa Mollah wako.
Ukiumwa Mollah wako anakuponesha, Anakupa riziki na mengineyo, huku wazee nao wanataabika kwa mapenzi wakitaka ushike njia ilonyooka. Kwa mapenzi hayo ukapambiwa Ulimwengu huu kila jambo zuri, ukatiliwa furaha ambayo unaishi nayo, jiangalie wewe ukiwa mgonjwa unaweza kuwa na furaha, ndio maana ukaambiwa unapewa Uhuru wa kuchagua ama shukuru kwa mapenzi haya au kufuru.
Vipi kushukuru?, jee unamkumbuka aliyekupa na kukufanyia mapenzi haya, una (share)mapenzi haya na wenzio, kwa kile unachopewa unakitoa, unaonea huruma wenzio, ama ukenda kinyume na hayo ndio huko kukufuru. Na kukufuru ni hiyo njia ya mateso, njia ya chuki, kwa ajili ya mapenzi ya Mollah wetu anatusubiria na kutuacha tuishi katika enzi yake ya mapenzi, ama wale wenye (gratitude)waloridhika na mapenzi ya Mollah wao, wao hawana shaka, wameridhika kwa kuumbwa kwao na kila walichopewa, Na kila linalokuja wako tayari wakijua linafanyika kwa ajili ya mapenzi ya Mwenye enzi Mungu, hakika walokufuru ni wale wenye kuyakataa mapenzi haya, wale wasoridhika na (Qadara) ya Mollah wao.
Na kwanini hawaridhiki hali wanapewa kupumzika wakichoka(Usingizi), wakishapumzika wanaamshwa ili waendelee na harakati za maisha, wakishikwa na njaa wanapewa chakula na riziki zao nyengine, wakishikwa na Kiu wanapewa maji, wanapewa uwezo wa kuona na kusikia, wakiumwa Mollah wao anawaponesha, Na ukizidi kumuasi husema asaa hawa viumbe wangu huwenda pengine wakarudi, lau ingekua si mapenzi ya Mollah wetu basi tungeangamia. Chukua mfano unamuasi Mollah wako kwa kulewa, "Tena unaimba ningekua na Pajero ningelewa Tirarira"Unalewa tirarira"Unaendesha Pajero lako, unafika nyumbani kwako Mollah wako anakutoa kwenye Pajero kwa usalama bila hata kuchuna kioo, unakwenda kwenye kitanda unalala na kuamka salama, basi hujijui kiumbe wewe kwamba unaishi ndani ya (Being of Love)Mapenzi.Na kila ukipindukia ukawa huogopi, na umefika katika umuri wa Utu uzima bado upo kwenye vilabu vya pombe, hutoki kwenye vikao vya Taarab, unaendelea kufanya maasi, Mollah wako anakwita kwa njia ya mapenzi, vipi?
قُلۡ يَـٰعِبَادِىَ ٱلَّذِينَ أَسۡرَفُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ لَا تَقۡنَطُواْ مِن رَّحۡمَةِ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَغۡفِرُ ٱلذُّنُوبَ جَمِيعًاۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ
"Sema "Enyi waja wangu Mlojidhulumu nafsi zenu msikate tamaa na Rehma ya Mwenye enzi Mungu, bila shaka Mwenye enzi Mungu husamehe dhanmbi zote, hakika yeye ni Mwingi wa kusamehe(Na)Mwingi wa kurehemu."
Kusamehe pekee mapenzi, kurehemewa ndio huo upole(Kindness)kunusuriwa na adhabu, mpaka Mwisho wa maisha yenu mapenzi yanakufateni, rehema zinakufateni, unachotakiwa ni kugeuka kidogo ukajiunga na hiyo (Gratitude)ili uwe katika walofuzu, jiunge na mapenzi ya Ulimwengu huu ili nawe uwe Mcha Mungu.
Sasa ikiwa hapo juu umeambiwa usikate tamaa hapa chini inafatia aya nyengine zilizomo kwenye sura ya (Fajr 27 mpaka 30)"Zina kuita kwa jina jengine, kule uliitwa (Abdi)hapa kwenye sura hii unaitwa Ewe Nafsi"uliyetua, Nafsi iliyotua ni ile yenye matumaini, Nafsi ambayo imekiri makosa yake na kukubali mazuri yake, ikarejea kwa Mollah wake hali ya kujua ima imefeli mitihani yake au imepasi, Na kwa ajili hiyo haina nafsi uwezo wa kufanya lolote ila kumuachia Mwenye enzi Mungu mwenye mapenzi ya kiumbe chake kumsamehe na kumuingiza na kumuweka na waja wema peponi.
Nini Matumaini?Matumaini ni (State of Gurantee)Ni hali ya kujiridhisha kisaikolijia, Kwa sababu hakuna Mwenye (Gurantee) isipokua kutoka kwa Mollah wako uliyopewa kwenye kitabu, na ukifikia mpaka kulijua hilo ina maana na wewe umo, unatakiwa katika safari hiyo, ambayo hakuna ajuae unakwenda wapi? nini kinatokea ukishafukiwa kwenye dongo, hesabu zako zimefichwa, pepo imefichwa, Moto umefichwa, Lakini kwa Mapenzi ya Mollah wetu matumaini kayaweka wazi, basi usikubali mtu yoyote ayachukue, sababu Mwenyewe alokuumba anakwambia rejea kipenzi changu, kwa sababu kutokana na mapenzi yangu wewe nimekuumba, kutokana na mapenzi yangu leo nakuchukua urejee nyumbani ulikotokea ndio maana umeitwa kwa jina la Nafsi, (sio Abdulla au jina jengine wewe Nafsi)leo rudi umeishi pengine kwa raha au dhiki, umeishi na maradhi au furaha basi rejea nyumbani uje kupumzika kama unavopumzika (Ukilala). Tena ondoa khofu ukiwa peke yako utakua (Boring)wewe unapenda (chit chat)kuzungumza basi ingia ukakutane na waja wema, hakuna mazungumzo ya kipuuzi tena huku ujako. Mwanzo Mapenzi mwisho Mapenzi, na kama utataka kinyume cha hayo Mapenzi ndio hiyo Dhiki tupu, mara wasiwasi, mara maradhi, mara hasira mara chuki, mara umehamaki, mara umenuna, Binaadamu jihadhari sana na kujitia maradhini, jitahidi kuyalea mapenzi na ndio hiyo (Taqwa).
Sasa utayajuaje hayo mapenzi? Mapenzi yenyewe ni haya maisha, Maisha ni zawadi kubwa Mwanaadamu alopewa na Mollah wake, ambayo unatakiwa uithamini. Jitahidi sana wakati unaishi kwenye Ulimwengu huu ishi na watu kwa mapenzi, ona raha kuwa umeamka mpaka unalala hujamkera Mollah wako, hujakera viumbe wenzako, hujaua hata kinyama, umeabudu kwa utulivu, ukiimaliza siku kwa njia hiyo jijue umo kwenye mapenzi, na hayo ndio matumaini ambayo yanakupa (gurantee)Bila ya khofu. Omba sana msamaha kwa ili uwe Mapenzini.
No comments:
Post a Comment