Asalaam Aleiykum
Siku zote inasomwa aya hii inosema:
وَإِذَا قُرِئَ ٱلۡقُرۡءَانُ فَٱسۡتَمِعُواْ لَهُ ۥ وَأَنصِتُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ
Na isomwapo Quraan isikilizeni, Nyamazeni ili mpate kurehemewa.
Watu wengi wamepata tafsiri tafauti na kusudio ya aya hii, wengine wanadhani kurehemewa hapo ni kupewa mali, au kupewa utajiri, na hili limetokana na Akili zetu kuzihusisha sana na mambo ya kipato, au biashara, ukifanya hivi utalipwa vile, Mwanaadamu unakua hupo kabisa unaambiwa kitu chengine unafahamu kitu chengine, Unaambiwa lete (Kawa)unaleta kahawa, huko kabisa mawazo yapo kwengine, ndio maana mkaambiwa itakaposomwa isikilizeni, halafu nyamazeni, kwanini yakasemwa maneno hayo kwa sababu kusikiliza ni jambo jengine na kunyamaza pia ni jambo jengine, lazima uyaunganishe mawili haya ndio unaipata hiyo Rehma, unaipata hiyo Fahamu, lakini kama hujayaunganisha mawili haya matokeo ndio yanakua hayo ya (Kawa na Kahawa).
maana ya kusikiliza ni tendo ambalo huna (Miliki nalo)unasikia kila jambo, lakini maana ya kunyamaza ni kuwa unakua (empty) katika (Mind)yako, kimya unasikiliza kitu hususia, na hapo kitu chenyewe ni hayo maneno ya ndani ya Quraan, na Rehma yenyewe ni hiyo fahamu, lakini wale wenye kusikiliza bila ya kufahamu inakua Rehma haifiki, unaishia kupenda sauti, unaishia kupenda anavosoma, hasara ilioje kuikosa Rehma ya kitabu cha Mwenye enzi Mungu. Bwana Mtume s.a.w anaambiwa nini?(Muzzamil aya ya 5)"إِنَّا سَنُلۡقِى عَلَيۡكَ قَوۡلاً۬ ثَقِيلاً ".
"Hakika sisi tutakuteremshia kauli nzito".
Sasa maneno yashateremka unaambiwa tulia uyasikilize ili urehemewe, kurehemewa kwenyewe kukoje, kuko hivi, katika kupewa Sheria na Muongozo, kupewa Dawa ndani ya maneno hayo, kujazwa Imani katika nyoyo yako, na mengi yalojificha makubwa makubwa ambayo huyajui, na ndio ukaambiwa tulia ufunguliwe mambo, poa upewe maana, wacha kelele upewe code za mambo zimo ndani ya Quraan, lakini wapi, nani anaye sikiliza, wangapi wenye kuipata maana ya ndani ya Kitabu hichi, hutowakuta ila wachache sana.
Sasa vipi utajua kuwa Rehma imekuteremkia?Pale itakaposomwa aya ima iwe kwenye Sala au venginevyo, Na wewe ukawa nje unasikiza ndani umetulia hakuna hadith za ajabu zinaingia mawazoni, hakuna biashara unafanya kwenye Akili, ndio pale itakaposomwa aya mfano wa hii sura ya (Rumi aya ya 21)
وَمِنۡ ءَايَـٰتِهِۦۤ أَنۡ خَلَقَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَٲجً۬ا لِّتَسۡكُنُوٓاْ إِلَيۡهَا وَجَعَلَ بَيۡنَڪُم مَّوَدَّةً۬ وَرَحۡمَةًۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ
"Na Katika Ishara zake(Za kuonesha Mapenzi yake juu yenu)ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mupate utulivu kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu, Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofikiri".
Mwanzo Mapenzi Mwisho Mapenzi.
endelea part 2
Shukran
ReplyDelete