Asalaam Aleiykum,
Sasa nini ufanye Kiumbe wewe, Kumbuka Mwanaadamu una vitendea Kazi vitu viwili, Kimoja katika hivyo hakiguswi na chochote, hakuna jambo lolote linaloweza kufikia kitu hicho ambacho ndio hiyo Taa ya Fahamu(Pure Soul). Kama Mwanaadamu utakua unakitumia kifaa hiki au nikipe heshima kwa sababu ni kitu kitakatifu(Roho)kwa uerevu, basi daima utakua umo furahani, kwanini nikasema umo kwa sababu (Roho)(Nature)yake ni Furaha(Nisiseme hivi Mkasema kasema anaijua roho kitu hicho hakijulikani), lakini hasara yetu Wanaadamu Tunaishi au kutawaliwa na hicho chengine chenye kutupeleka kwenye kiza, kipi hicho?.
Akili(Hii ni sehemu ya Nafsi) ni nyenzo ambayo tunatakiwa kuitumia kwa uangalifu kwani ni (Very Powerful weapon)silaha kubwa sana, ukimilikiwa na Akili Binaadamu umekwisha, huna (Control) ya maisha yako kabisa.
Kwa sababu Akili inafanya kazi yake ya kukusanya, kupokea na kutupa kwenye hicho chumba, chumba hiki kiite (Memory or Subconscious)na kwa kuwa lolote lile lilopita kwenye taa yako ya Fahamu kumbuka liko humo chumbani umeliweka na wala halitoki, Sasa nini kinatokezea kuna baadhi ya nyakati Taa inawaka na kumurika yale mambo yaliyomo kwenye chumba iwe chuki, hasada, uzinifu, wizi, na ukimurika tu likija juu lazima ulitende kwa sababu hujalitupa ila umeliweka akiba, kwa hiyo tahadhari sana unapokwenda kwenye chumba chako, utakua unatenda mambo bila ya kukusudia, sasa kwa kuwa mambo yana kukera ndio unaamua kuzima Taa, na huku watu wanatumia ule msemo kajitoa fahamu.
Quraan imekuhurumia imesema unaleta nyudhuru yaani unazima Taa, ndio ikaendelea kukumbusha kuwa Mwanaadamu ni Mwenye kuiona Nafsi yake, ikimaanisha unao uwezo wa kuishinda Akili, tumepewa maarifa ya kukishinda kifaa hiki, kwanza kwa kujulishwa wewe na hicho kifaa ni tafauti, ndio maana ukaambiwa wewe unakiona kitu hicho, na una uwezo wa kukitumia usiache kikakutumia.
Sasa nini tumepewa ili ufike au urudi kwenye Taa yako ya fahamu, itabidi tuchukue mbinu hii ya Quraan ili tupate mafanikio ya kuitawala hii Akili badala ya Akili kututawala sisi, Napenda ufahamu ukitawaliwa na akili unakuwa mteja(addicted)na ukiitawala Akili unakua Mcha Mungu, hiyo ndio tafauti yake.Ndio maana tunajikuta huyu mteja wa mazungumzo, yule mteja wa wanawake, huyu mteja wa mali, mwengine yeye hafurahi mpaka agombane, mwengine mteja wa kuumwa tu haipiti siku bila ya kujipa maradhi, wengine wao wagonjwa wa (facebook)hiyo ndio Akili ilivyo ikikosa Balance, wengine wanataka wale tu akiona chakula hajiwezi, kuna maradhi ya kusema uongo, balaa zimetushukia wanaadamu na hatujui tufanye nini.
Sasa namalizia kwa kutoa dawa ifanye dawa hii na maajabu yake yatakua kama alivosema Nabii Yussuf a.s.. Ufanye nini?.
kitu kimoja anza zoezi hili la kuitizama Nafsi yako kwa kila ufanyacho, tabia zetu wanaadamu tunatizama yanotokea nje ya Nafsi zetu, sasa fanya kinyume chake tazama yanotokea ndani ya nafsi yako, utaanza kuona miujiza kidogo kidogo inatokezea, ukikitizama chakula wakati unakula basi hutokula mpaka tumbo livimbe utafikia pahala nafsi itakwambia nishatosheka, ukiitizima akili yako utaona Traffic ya mambo yanavopita, wewe tizama usjiunge na Traffic, Mwanamke au Mwanamme anapita wewe itizame akili yako na (Action)zake, kidogo kidogo utaona uteja unaanza kupungua, ukimaliza kutizama kwa njia hiyo sasa ukikaa kitandani umefunga macho tizama takataka za chumbani, anza kusafisha mavumbi, kidogo kidogo utaona unaanza kupunguza mambo yaliyomo kwenye chumba chako cha mawazo, kumbuka mambo yote yameingia kwa njia ya kutizama, na tumia njia hiyo ya kutizama ili uyatoe yote yalojaa kwenye Nafsi yako, mpaka ndoto za kipumbavu zinatoweka, taratibu utaona mwanga wa Taa yako ya Fahamu unaanza kuchomoza, na siku ambayo Taa itamurika chumba kizima siku hiyo ndio siku ya Rehma, ambapo akili inakukabidhi utawala wako unakua wewe ndio Mfalme wa nafsi yako, utakua kama mfano wa Nabii Yusuf a.s Mwanamke anakuja unakimbilia mlangoni na kanzu yako inachanwa kwa nyuma. ukifikia daraja hiyo elewa na Mollah wako anakusamehe madhanbi yako na hapo unaanza kuufahamu Ulimwengu huu vyengine kabisa, Akili ikaapo pembeni kila kitu unakiona kwa kutumia Nuru yako ya Fahamu, kama ulivokua utotoni ulipokua unaanza kupata Fahamu, kila kitu Miujiza, iwashe tena Taa hiyo na yote yalopita yatakua (History).
Kumbuka kutizama, kwanini nikasema kutizama na sio kuona, kwa sababu kutizama uko mbali na kuona uko karibu, na ukiwa karibu lazima ujiunge, "Waswahili wanasema utamu wa ngoma kucheza ukizunguka raha zimezidi" kwa hiyo na wewe usicheze utakuja kuzunguka, na ukizunguka hutoki kwenye duara, itakua unakera unafanya unatubu, unafanya tena unatubu, haina faida yoyote unateseka mpaka unaondoka kwenye Ulimwengu huu, utakuja kufufuliwa uteswe tena, hakuna atopata tabu isipokua wewe, unapewa njia itumie ili upate faida ya kurehemewa na Mollah wako. Hicho chumba nilichokitaja ni hiyo (Mind) ambayo uloijenga ukawa unaingia na kutoka, siku (Mind) itakaposita utabakiwa na (Brain) na Taa yako, hapo tena utakua Muhsin, Mja Mwema, kumbuka Mambo mema yanayafuta mabaya na huko ndio kusamehewa.
No comments:
Post a Comment