Thursday, November 3, 2016

TAA YA FAHAMU PART 2

Asalaam Aleiykum

Akili ina mwenendo wa njia mbili, Njia ya kwanza kutupa kila kitu kwenye chumba chake, halafu inazima Taa, inajifanya haitazami tena, haina haja ya kuwasha Taa tena na kusafisha chumba, na njia ya Pili ambayo ya kusafisha hicho chumba au kuwasha Taa ukaona vitu vilivyomo huitumii kabisa, kumbuka kila kiingiacho chumbani kinahitaji kutolewa, na huwezi kuvitoa vitu hivyo mpaka uwashe Taa hii ya fahamu, Nikimaanisha jambo lolote linaloingia kwenye akili pia linashuka kwenye moyo, Sasa maradhi yote na matatizo yote yanakukuta sababu ndani ya chumba chako kuna takataka nyingi, vumbi limejaa, umebeba mizigo ambayo huna haja nayo katika safari yako.
Kwa hiyo unatakiwa ufanye jitihada kutupa yaliyomo ndani ili uishi kwenye Ulimwengu huu kwa Furaha, na kutokana na sababu hiyo ndio sasa nakutaka uwashe hiyo Taa ya fahamu ili upate kutoka kwenye kiza. Kumbuka Nabii Yusuf a.s anasema Nafsi ina amrisha maovu na kuna njia moja tu ya kuweza kuishinda nafsi ambayo yeye aliitumia na sasa ushafika wakati na wewe uitumie.
Aliendelea na kusema isipokua upate Rehma ya Mwenye enzi Mungu, vipi unaipata Rehma hiyo, kawaida yako wewe unafanya kazi ndani ya Rehma, maisha yako yote ni Rehma, na hakuna Rehma kubwa kama hii ya kuona. Sasa nini kinatokezea?kila jambo linatokezea unapeleka kwenye nafsi yako, Senema unaangalia wanawake au wanaume vimo humo, unafanya wizi na ufisadi, unasema uongo, unashuhudia maasi na kila machafu hayo yote kumbuka yanapita na kuingia kwenye chumba chako, ikisha unakwenda kulala wewe chumba kimejaa mambo, unazima taa huna wasiwasi, ukiamka unaanza tena na tena, sasa hata siku moja hujasafisha ndani ya chumba, unakata kucha, unapaka (Poda)unakoga unatia uturi, Nyumba nje Mashaallah inasafishwa kikweli, lakini nini habari ya ndani?, Nani basi wa kukusafishia isipokua Mwenyewe, na Chumbani kiza utasafisha vipi si lazima uwashe Taa.
Kumbuka yote uloyaona na kusikia yamo ndani na kusafisha kwenyewe lazima iwe (Reverse)kinyume chake. kumbuka Taa ikizimika Uharibifu wote ndio unatokea, kwa sababu umo gizani unajikwaa kwenye Furniture, unajikwaa kwenye kila Dhanmbi, unatibu watu wengine kumbe wewe Mwenyewe Mgonjwa, Watu wanakushangaa jamani huyu si Sheikh mbona anafanya mambo haya, kumbe hawajui wewe na wao nyote Taa zimezimwa.
Nabii Yusuf a.s aliposema sijitakasi Nafsi yangu alikua anajua hawezi kujichukulia dhamana na Nafsi pekee, nafsi ina vituko, imo kwenye kuamrisha ufisadi na maovu kutokana inaishi kwenye giza.
Sasa ufanye nini unatakiwa utoke gizani uelekee kwenye Nuru.
Endelea part 3

No comments:

Post a Comment