Asalaam Aleiykum,
Kuna Msemo wa "Kiswahili Mzuri sana"unasema hivi"(Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga) Hiyo ni kweli kabisa, hali kama hiyo Mwanaadamu unayo lakini bado hujaifanyia kazi, pengine dunia imekushughulisha, basi kutokana na makumbusho haya labda waweza kuanza kutafakari na kujiwezesha kuwacha kuishi kizani,utaanza kuishi kwa njia ya kutumia Taa ulonayo,Usikubali tena Umeme wa Nje Uzimwe na wa ndani kwenye Nafsi yako Uzimike.
Nini Taa?. Mpaka leo hakuna aliyeweza kutwambia au kuchambua , au kujua nini Taa, Si Wanasayansi wa Dunia wala wa Dini walofanikiwa kujua nini Taa, Wanasayansi wao wamechambua na kufikia kuieleza utendaji wake wa kazi, wakasema hakuna kitu kiendacho kwa kasi kama Taa(speed of light) na hivi karibuni wamegundua kuwa kila kitu mwishoe kinabadilika na kuwa hiyo Taa(Light), Lakini wakiulizwa Taa yenyewe ni kitu gani hawawezi kulijibu swali hilo.
Na Wanasayansi wa Kidini au niwaite(Wanazuoni)wao wamegundua kuwa kila ukenda ndani au kuzidisha Ibada unakutana na hii Taa(Light), Lakini pia hawajui nini uwezo wa hiyo Taa ya ndani, nini kazi yake?, ila wanaamini hii Taa ina uwezo wa kukuongoza kutoka kwenye giza kwenda kwenye Nuru, ziko dalili zinaonesha iwapo utapunguza Ibada au kutenda Dhanmbi inakua inapungua nuru ya taa hiyo.
Tukizungumza Taa inabidi tuieleze Taa ya aina gani, kwa sababu Taa ziko za aina nyingi japokua asili yake ni moja. Mfano Taa hii ya Jua ambayo ndani yake zinapatikana faida nyingi tu si za kuondosha usiku pekee mpaka (Vitamin D)imo kwenye Taa hiyo. Kwa hiyo taa ni nyingi na zina kazi tafauti, leo sisi tutaizungumzia Taa ya ndani, taa ya Nafsi yako, kabla ya kwenda mbali wacha tuutizame mfano mdogo ili utupe muelekeo wa Darsa yetu, na hapa tutaichukua Taa yetu ya kawaida(Umeme), Na wakati mzuri ni ule ambao Taa zimezimwa, Kiza kimetawala chumbani, nini kinatokezea?.
Inapokua kiza maana yake huoni kitu, lakini mara inapoletwa au kuwashwa Taa unaviona vitu vyote viliopo katika chumba hicho, na hivyo pia ndivyo Taa ya Fahamu inavofanya kazi yake, mfano ni uleule hakuna tafauti.
Sasa kwa Mwanaadamu Taa hii ina kazi mbili ama kazi ya kwanza nini kukutoa kwenye Ujinga na kukupeleka kwenye werevu au ita (Elimu)na kazi ya pili ni kukuonesha chumba chako cha Nafsi na Takataka, mavumbi, fanicha na vyote vilojificha kwenye Nafsi yako. Ndio maana tutatumia aya moja kutufahamisha kuwapo kwa Taa hii, na vipi "Ukweli Ukidhihiri uongo hujitenga", vipi inakua wakati ukiigundua taa hii, faida gani unaipata katika kuitumia Taa hii.
Sura ya Kiyama aya ya (14-15)
بَلِ ٱلۡإِنسَـٰنُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ بَصِيرَةٌ۬
Bali Mwanaadamu ni Shahidi(Mwenye kuona)Nafsi yake.
وَلَوۡ أَلۡقَىٰ مَعَاذِيرَهُ
Ingawa anatoa Nyudhuru zake.
Naam ilipotajwa kuona au kuishuhudia Nafsi yako hapo inatakiwa ujiulize nini kimekusudiwa, Lazima ujiulize nini nafsi na nani Mwenye kuiona, na utafute maana halisi yakutambua kumbe kama najiona ina maana mimi ni tafauti na nafsi. Basi ikiwa tafauti kwanini naleta Nyudhuru, ukiweza kugundua mawili hayo hapo hapo utaelewa kumbe hii nyudhuru ndiko huko kuzima hiyo Taa.
Mwanaadamu unajiona matendo yako yote, na kuona huku ndio huo Muujiza, kwa sababu macho yanoona wewe una uwezo wa kuyaona, sasa hicho kinachoona nini?, kifanyie kazi upate kukijua, kama nilivosema wewe na Nafsi ni vitu viwili tafauti, ila unazidiwa na nafsi, Nafsi inakutawala nakuchukua madaraka yako, inatakiwa ufanye kazi kubwa sana kuishinda Nafsi, ndio Nabii Yusuf akathibitisha kwenye quraan sura ya Yussuf aya 53.
وَمَآ أُبَرِّئُ نَفۡسِىٓۚ إِنَّ ٱلنَّفۡسَ لَأَمَّارَةُۢ بِٱلسُّوٓءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّىٓۚ إِنَّ رَبِّى غَفُورٌ۬ رَّحِيمٌ۬
Nami sijitakasi nafsi yangu , kwa hakika (Kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu, isipokua ile ambayo Mollah wangu ameirehemu, Hakika Mollah wangu ni Mwingi wa Kusamehe na Mwingi wa Kurehemu.
Naam hiyo ndio Akili ina Mwenendo upi?
Endelea Part 2
No comments:
Post a Comment