Friday, December 2, 2016

MIUJIZA NJE YA AKILI PART 3

Asalaam Aleiykum

Tuko katika kutizama (Hekima) za Luqman, Na kwenye aya ya 18 anasema:
وَلَا تُصَعِّرۡ خَدَّكَ لِلنَّاسِ وَلَا تَمۡشِ فِى ٱلۡأَرۡضِ مَرَحًا‌ۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخۡتَالٍ۬ فَخُورٍ۬
Wala usiwatizame (Watu kwa Jeuri)kwa upande mmoja wa uso(Dharau)wala usende katika nchi kwa maringo, Hakika Mwenye enzi Mungu Hampendi kila ajivunae, ajifahirishaye.
Ukiingia au kupewa Hekima unajua Mwenye Enzi Hapendi wala kuchukia kwa sababu Yeye hana mfano wa Binaadamu, lakini kwa ajili ya kuwasiliana na wewe ndio yakatumika maneno hayo, Lakini ndani ya maneno ya Luqman kwenye hekima yake anajua kuwa Wanaadamu wana (Energy)maalum inayotoka katika Roho zao, kutokana na nguvu za (Energy)hiyo Mwenye enzi Mungu anakuondoshea kinga yake kwa yale unayowafanyia wenzio, na maringo yako, ndio mara unaanguka kimaisha au kupata maradhi.
Nimemtumia Luqman kuonesha ukipewa Hekima unakua mtu wa aina gani. Mama akishirikiana na Ulimwengu anakulea taratibu, kama vile Mti unavokua, mboga zinavyochipua, matunda yanavo wiva, Ulimwengu hautaki haraka unakwenda na sheria ilivopangwa.
Sasa ukija na Ujana wako umebeba saa, unaishi ndani ya saa yako, ndio utajiona uko mbioni unahangaika na maisha, Ama Mtu mzima yeye ana (Option)kwa sababu kashapewa nasiha, Akitaka na kuridhiwa na Mollah wake ana uwezo wa kuingia kwenye Hekima, Na kama hakutaka basi atabakia na saa lake mpaka kufa kwake.
Sasa ukiingia au kupewa Hekima Miujiza gani inatokezea?.
Kwa Mara ya Mwanzo unapata utulivu wa Akili, unakua hupangi au kuamua mambo kwa kutumia Akili, huoni au kuangalia kwa kutumia Akili, Kwa Mara ya Mwanzo unapata mambo kwa uhakika, hapo tena unajijua rasmi kama utakufa, ukioneshwa rangi ya kijani unaiyona kwa uhalisia wake, hukioni chama au bendera unaona (Pure)green na kazi zake, Kwa mara ya mwanzo unapata kuwasiliana na Roho yako, Na Maswali na majibu yanatoka kwenye hiyo (Source), Hukurupuki na kujibu maswali ovyo ovyo kama ufanyavo hivi sasa, Naam hiyo ndio Hekima, na hayo kwako ndio yatakua miujiza ya kuipoteza hiyo saa ulonayo hivi sasa.
Sasa Pazia linaondoshwa ukiwa hai baina ya Akili na Roho yako, hiyo ndio Hekima. Madhanmbi unayaona kwenye asili yake na madhara yake, sasa hivi unajua dhanmbi lakini hujui dhara yake, omba au ingia kwenye Hekima uone dhara yake. Ingia kwenye Muujiza huu wa Hekima upate kuona mambo kwenye original yake, Hekima ni haki yako fanya jitihada upoteze saa ili uipate hekima, najua unashituka kuipoteza saa yako, lakini kumbuka saa umeinunua kutoka kwa wazee wako, walimu wako, marafiki zako, lakini Hekima ni (Original)yako, kumbuka ulivokua mtoto ukawa unashangaa hichi nini na kile nini, rejea tena kule kwa mara ya pili ukashuhudie Miujiza, kaipate (Truth), Ndio Maana Mwenye enzi mungu akasema sura ya (Baqarah aya ya 269)
يُؤۡتِى ٱلۡحِڪۡمَةَ مَن يَشَآءُ‌ۚ وَمَن يُؤۡتَ ٱلۡحِڪۡمَةَ فَقَدۡ أُوتِىَ خَيۡرً۬ا ڪَثِيرً۬ا‌ۗ وَمَا يَذَّڪَّرُ إِلَّآ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَـٰبِ
Mwenye enzi Mungu humpa hekima amtakaye, Na aliyepewa Hekima bila shaka amepewa kheri nyingi, Na hawakumbuki ila wenye Akili.
Kwa hiyo ni vizuri kuwa na hiyo saa ambayo itakufanya uikumbuke hiyo Hekima, na Akili imewekwa ni kama sehemu ya kuchupia uende kwenye hiyo Hekima, Muujiza uko hapo katika kukumbuka ukachupa.
Wacha niendelee kufafanua ili ufahamu vizuri, Elimu ni Mafunzo ya Nafsi, Sheikh kakwambia hivi, Mwalimu kakwambia vile, watu wanasema haya, na wewe unajua hili, ni mambo katika Ulimwengu huu yaloletwa na hiyo saa, Lakini hekima ni Mafundisho ya Kiroho ambayo yanatoka kwa Mwenyewe subhanna, kama vile ukitia mbegu kwenye Ardhi unatokeza kuwa Mti, Kwa hiyo Elimu ni jambo litokealo nje, Na hekima ni jambo unalolipata kutokea ndani, kumbuka la kwanza kutokea kwenye Akili na la pili ni lile litokalo kwenye Roho.
Unaweza Ukapewa Kitabu, umesoma na (PHD)lakini ukawa hukupewa Hekima, unakua na hasara kubwa, kile cha muhimu huna, umebakia na saa lako, ndio maana ukipewa Hekima unaambiwa Ushukuru kama alivo (Shukuru)Luqman.
Sasa Muujiza nje ya Akili ni upi, Ni ule uwezo wa kuishi katika (State)au hali Mbili, Ya kwanza ni ile ya Mnyama, unalala, unakula, Na ya pili ni ile ya Ubinaadamu ya kuelewa (There is something beyond)Unakumbuka na kusahau, unapita katika hali hizi mara umeponyoka umetenda dhanmbi, halafu unakumbuka unarudi tena na kutubu, ukiwa katika hali hiyo ya kukumbuka huo ndio muujiza wenyewe na ukipewa ukawa unakumbuka daima huo ndio ucha Mungu, na kuishi katika kukumbuka ndio huko kuipoteza saa, sababu saa inabadilika lakini kukumbuka kuko vile vile, Ukiingia kwenye sala, ukitoka wewe uko vile vile mpaka ukilala unajijua wewe nani, Na ukiamka unajijua wewe nani hubadiliki, kumbuka saa yako inabadilika lakini hekima yako iko vile vile. Ishi kwenye hekima upate Miujiza yake na hutotaka kutoka tena kwa Uwezo wa Mollah wako.

No comments:

Post a Comment