Friday, December 2, 2016

MIUJIZA NJE YA AKILI PART 2

Asalaam Aleiykum

Naam, Mtoto yumo kwenye  hiyo (Hekima)(Wisdom)Lakini hajijui ndio maana hata Kwenye Quraan lilipotajwa jambo la (Hekima) Luqman alimuanza nani? isome Quraan uone vipi inakua kupoteza saa, vipi unajua tafauti ya saa na (Hekima). Anasemaje Mollah wako? Luqman aya ya 12 mpaka 13 na kuendelea. Zama kwenye maneno hayo ujue hekima inatokea wapi.

 وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا لُقۡمَـٰنَ ٱلۡحِكۡمَةَ أَنِ ٱشۡكُرۡ لِلَّهِ‌ۚ وَمَن يَشۡڪُرۡ فَإِنَّمَا يَشۡكُرُ لِنَفۡسِهِۦ‌ۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِىٌّ حَمِيدٌ۬
Kwa yakini tulimpa Luqman Hekima(Wisdom), Tukamwambia Mshukuru Mwenye Enzi Mungu, Na atakaeshukuru kwa yakini anashukuru kwa ajili ya Nafsi yake, Na atakae kufuru Mwenye enzi Mungu(Amejitosheleza)Mkwasi asifiwaye, (Si Mwenye kuhitaji shukurani zenu)
Nini (Wisdom)au Hekima? Ni hali au uwezo wa kumiliki Nafsi yako nje ya Akili, au kwa lugha nyengine ni mkusanyiko wa ufahamu mambo yalopita na yajayo ukawa unaishi nayo sasa hivi, hiyo ndio tafsiri ya Rahisi ya hilo jambo la (hekima)lakini hata halijafikia ukaribu wake na kusudio ya hiyo hali ya kuwa na (Hekima).
Anasemaje Luqman? Tulimpa Luqman Hekima, tukamwambia Mshukuru Mollah wako, kwanini ashukuru, kwa sababu kitu hicho ni kitu (Adhimu)ni (State of Knowing),Hiyo ndio Hekima, Binaadamu ukijijua basi unashukuru kwa kupewa neema na rehma hiyo, Mnyama ana lala na wewe unalala, halafu nyote mnaamka, lakini kuna mmoja anajijua kaamka, na huyo ni wewe, Shukuru kwa Neema hiyo ya kuumbwa Mwanaadamu na ukapewa cheo cha kujijua, Shukuru kwa Nafsi yako uko mzima, unavuta pumzi bila ya taabu, unatembea na kurudi bila ya shida, unapata riziki yako kama ilivopangwa, shukuru kwa ajili ya Nafsi yako, na kama hutaki hilo au kumshukuru Mollah wako, Yeye hana (haja na shukuruni yako),  endelea kumkanusha, kumpinga na kumuasi na yeye atakunyima miujiza hii nje ya Akili.
Naam sasa toka kwenye saa uingie kwenye miujiza wa (Hekima) za (Luqman), Hekima inakuja kwa njia ya kusubiri, katika Ulimwengu wa sasa Binaadamu kasoma sana, lakini kwa kufanya hivyo kapoteza (Hekima), kwa sababu ya haraka za maisha, ndio maana (Luqman)akaona aanze kwa Kumtahadharisha Mwanawe, kwa sababu (Asiye funzwa na mamae hufunzwa na Ulimwengu).

وَإِذۡ قَالَ لُقۡمَـٰنُ لِٱبۡنِهِۦ وَهُوَ يَعِظُهُ ۥ يَـٰبُنَىَّ لَا تُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ‌ۖ إِنَّ ٱلشِّرۡكَ لَظُلۡمٌ عَظِيمٌ۬ 
Na(Wakumbushe)Luqman alipomwambia Mwanawe na hali yakuwa anampa nasiha, Ewe Mwanangu usimshirikishe Mwenye Enzi Mungu, Maana kushirikisha ndiyo dhulma kubwa.
Hapo kuna tafauti kubwa baina ya Baba na mtoto, tafauti yenyewe mwenye hekima hawezi kukupa hekima yake, ila ikitoka kwake inakua nasiha. Nasiha ni tahadhari na hapa kuna maneno makubwa inatupasa kuyazingatia. Kasema Luqman usimshirikishe Mwenye enzi Mungu hakika shirki ni dhulma kubwa.
Katika kuifahamu au kujificha katika aya hii watu wengi wakadhani Shirki ni ile ya kuabudu kitu chengine pekee cha asiekuwa Mwenye enzi Mungu, lakini mengine yote hayapo kwenye Shirki, leo hii nakwambieni ukiapa kwa jina la Mwenye enzi Mungu kiapo cha uongo hiyo ni dhulma na umemshirikisha Mwenye enzi Mungu na ni dhulma kubwa,(Umelitumia jina lake kwenye Uharamia wako).
Ukimuomba asiyekua Yeye basi umemshirikisha, ukimtegemea asiyekua yeye basi umemshirikisha, ukitoa ushahidi wa uongo basi umemshirikisha,Ukenda kwa mganga kuroga umemshirikisha Mollah wako,  Kwanini ikawa hivyo? Kwa sababu wewe unazo sifa zake mbili muhimu za (kuona na kusikia)Kheri hii alokupa ndio unaifanya nyenzo ya kuibia au kupata kisicho haki yako, Na hiyo ni dhulma kubwa kabisa. Ndio maana kwenye aya ya 15 Mwenye enzi Mungu wasia wake kwa wanaadamu akasema,Na kuanza na wazazi wako,  iwapo wazazi wako wakikulazimisha kunishirikisha mimi basi usiwatii (Abadan).
Endelea Part 3

No comments:

Post a Comment