Friday, December 2, 2016

MIUJIZA NJE YA AKILI PART 1

Asalaam Aleiykum

Mie mpenzi sana wa Lugha ya Kiswahili, Lugha ambayo imekusanya maneno kutoka lugha  nyingi tafauti na kujiunda lugha moja ya Kiswahili, ndani yake kimo Kihindi, Kiengereza,Kireno,Kiarabu,Kiafrica na lugha nyengine kadhaa, Ndani ya Lugha hii kuna misemo mingi ilo jaa hekima, Mie leo nimechagua msemo ulokua unapendwa na wazee usemao,"Asofunzwa na Mamae hufunzwa na Ulimwengu".
Hapa yametumika maneno yenye thamani kubwa, Maneno ambayo yanaishinda almasi, ukiyazingatia maneno haya utagundua hayajatokea kwenye Akili, Wapi yametokea? hilo ndio dhumuni ya darsa yetu leo.
Nina Tabia niendapo likizo Nyumbani Africa hupendelea kujumuika na vijana kwenye vikao vya kahawa, siku moja wakati tumekaa alipita kijana mmoja maskin anacheka na kuzungumza peke yake, Vijana nilokaa nao wakanambia yakua kijana Mwenzao kapoteza saa, Mimi nikawajibu basi tumsaidie kutafuta, wale walokuwepo pale walicheka sana, Mimi nilifahamu yule kijana ni mgonjwa wa Akili, wao wakanifahamu mimi ni mjinga wa Lugha, na sifahamu chochote, lakini ndani ya Nafsi yangu nilikua nawaangalia jee wale waliopo pale wamefunzwa na Ulimwengu, nikagundua wamesema maneno makubwa lakini hawajui maana yake, kama vile kusema Kiarabu ukawa hujui tafsiri yake.
Sasa mimi leo Nakuchukua katika Safari hii ya "Miujiza Nje ya Akili" ili upate kufahamu kwa uzuri inakuaje ukipoteza saa. nje ya Akili inakuje,Watoto wa Nabii Adam a.s  Habil na Kabil Mmoja wao alipomuua mwenzie akabakia kakamata saa hajui afanyeje, Ulimwengu ulimfunza vipi?

فَبَعَثَ ٱللَّهُ غُرَابً۬ا يَبۡحَثُ فِى ٱلۡأَرۡضِ لِيُرِيَهُ ۥ كَيۡفَ يُوَٲرِى سَوۡءَةَ أَخِيهِ‌ۚ قَالَ يَـٰوَيۡلَتَىٰٓ أَعَجَزۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِثۡلَ هَـٰذَا ٱلۡغُرَابِ فَأُوَٲرِىَ سَوۡءَةَ أَخِى‌ۖ فَأَصۡبَحَ مِنَ ٱلنَّـٰدِمِينَ (٣١)
Hapo Mwenye enzi Mungu akamleta kunguru anayefukua katika Ardhi ili amuonyeshe jinsi ya kuificha maiti ya ndugu yake, (Akasema yule Ndugu aliyeua) ole wangu nimeshindwa kuwa sawa na kunguru huyu na kuficha maiti ya ndugu yangu, basi akawa miongoni mwa wenye kujuta.
Kwanini akajuta?, kwa sababu Kunguru kaja na hekima, yeye akasoma kupitia kwa Kunguru, Basi kujuta kwake ni kule kumdhulumu ndugu yake na kushindwa kuuhifadhi Mwili wa ndugu yake.
Nimekupa aya hii moja ili iwe muongozo wa darsa yetu, yule ndugu aliyeua ilipomponyoka saa alishuhudia kitendo cha mshangao, Kutokana na amri ya Mwenye enzi Mungu kaletwa kunguru kwa njia ya Hekima ili amuoneshe vipi kuustiri maiti ya ndugu yake. Asofunzwa na Mamae hufunzwa na Ulimwengu.
Saa ilokusudiwa hapo ni hiyo Akili(Mind), Napenda uelewe mambo yote yanotokea katika Akili yanahitaji muda, ndio hiyo saa au ita (Time) ukijumlisha ndio unapata siku, pahala, jana na kesho, hiyo ndio (Time) au (Memory) ukiyapoteza au ukitoka katika (system) hiyo ndio huko kupoteza saa.
Na huko kupoteza saa kupo kwa aina mbili, aina ya kwanza ni ile ya kupoteza Fahamu, ugonjwa wa Akili, (Drugs) N.k, Na aina ya Pili ndio hio Miujiza una (Function)au unaingia kwenye (Eternity)au (Wisdom). (Mfano) ukilala unapoteza saa hujijui,  lakini wakati wa kufa unapoteza saa unajijua.
Endelea part 2 uingie kwenye Ulimwengu wa Hekima.
endelea part 2

No comments:

Post a Comment