Asalaam Aleiykum
Jambo la pili kutajwa kati aya hiyo ni Njaa, Kwanini ikatajwa njaa, kwa sababu baada ya hofu kinachofatia ni Njaa, tizama mahusiano haya mawili yalivyo, ukiwa na hofu wakati wote unakua unafikiri, na ukiwa na njaa hali ni hiyo hiyo vipi utapata chakula uhifadhi tumbo lako, unajua kama sikula nitakufa, Njaa pia inahusiana na Mauti, Kama hujala kwa miezi mitatu unakufa, (Body)haiwezi ku(survive) zaidi ya hapo.
Ndio maana Makureish wakaambiwa kwenye sura ya (Quraysh)"Wakaambiwa wanachukuliwa dhamana ya janga la njaa halitowafika, Na kuwa hapo pamejengwa Nyumba Tukufu basi pia imepatikana dhamana ya hofu haitowafika kwa kushambuliwa kivita na kupoteza maisha yao". Ndio maana na hata serekali zenu zina kitu kinaitwa (food security)wanapita watu kutizama hali ya ukame ikoje, mazao yamepungua, mvua za kutosha, akiba ya chakula ipo, kwa sababu njaa ikikithiri watu na Taifa zima liko hatarini, watu watashindwa kutekeleza wajibu wao.
Na ukiutizama huo Mwili unategemea chakula ili uweze kuendelea kuishi katika safari hii ya maisha.
Jambo la tatu kwenye Mtihani wa safari hii ya mwanaadamu ni kupungukiwa na mali, Mali ulochuma inaanza kupunguzwa kwa njia usizozifahamu, Ukiangalia utaona watu wengi walikua na mali lakini kidogo kidogo wanaanza kufilisika, sasa kwa yule Mwenye Akili anajua Mwenye enzi Mungu ndie aliyenipa na haina haja mimi kuteseka na kuanza kuitafuta kwa nguvu zangu, huu mtihani na mimi nauridhia.
Na jambo la Nne utalishangaa mali ikipungua na watu wanaanza kupungua, Marafiki wanakimbia, sasa huna kitu, wote walikusanyika sababu ya mali yako, wengine wanakufa, wengine wanatoweka, na wewe afya yako inaanza kupungua, kutokana na kuegemea kwako kwenye mihimili ya mali na watu huwezi kuchukua sasa unaanza kuumwa, afya yako inadhurika.
Na jambo la Tano, kama ulikua na mashamba vitu havioti kikawaida, Hapo tena ndio furaha inapungua, biashara hazendi, ulowakopa wanataka walipwe madeni yao, hapo ndipo kila kitu kinakuja juu mara (Blood Pressure)mara una (stress)mara Bul sukari(Diabetic), Nini sababu yake umeshikamana na mali, unaipenda pesa, unapenda mali huwezi kuzikosa, hapo tena na maradhi yanakupenda wewe yanaanza kukupa (sign)jirekebishe, mara (Minor stroke)mara hichi mara kile unapunguzwa kidogo kidogo kwanza Nje halafu kwenye Nafsi yako.
Unajikuta umebaki peke yako na hiyo ndio safari ya Maisha, hiyo ndio njia anayopita kila mmoja wetu kwenye Ulimwengu huu. Lakini kwa kuwa Mwenye enzi Mungu anawapenda Viumbe vyake kaamua kuwapa siri wakiweza kuisikiliza na kuijua maana yake basi watakua wamegundua kitu Adhimu sana, watakua wameikomboa nafsi yake kutoka kwenye mitihani hii ya safari ya maisha.
Kawaambia nini?, Kasema kwenye mwisho wa aya Wabashirie Wenye Kusubiri, Nini subira?. Subira (Sabr)ni katika majina ya Mwenye enzi Mungu, Nini kinapatikana kama utaingia katika Ufalme wa Subira, Ndani ya Subira hakuna siku wala saa, hakuna Mchana wala usiku wewe umo katika hali ya subira, ikiwa unaumwa unaweza kupona au usipone, inaweza ukapewa au usipewe, wewe upo katika hali ya ku(surrender)Ndani ya subira ndio unafunguliwa ukweli wa mambo, kama kweli umejifunga katika subira, huna shaka hata chembe, hutaki hirizi wala kafara, unaacha itokee kama ilivoandikwa, inakua umejikabidhi kwenye Ufalme ulokuumba, sasa huna madaraka yoyote, kama maradhi ndio yapo, kama shida ndio zipo, kama Mauti ndio yapo, na ndio haki ya Mwanaadamu, sasa wewe ushajijua huna la kufanya, Na umeamua kukaa kwenye shimo la (Abyss)ya subira unasubiri. Na ikiwa kweli ni Mwenye kusubiri basi ndani ya hiyo subira utafunguliwa kitu, kitu hicho ukikijua wakati uko hai inakua faraja, unajua kumbe huyu ndio mimi, Mimi ndio Roho, ndio nilokua nasikia hadith zake, ndio mimi nasubiri, kumbe mimi tafauti na hayo mambo yanaonikuta katika hii misiba mitano ya misukosuko.
Basi hapo ndio utaweza kutamka kwa Ukweli hayo maneno ya yaliyomo katika aya inayofatia ya (156) "Ambao uwapatapo Msiba husema""Hakika sisi ni wa Mwenye enzi mungu"Na kwake yeye tutarejea".
Ukiweza kutamka maneno hayo Kiroho, hapo utakua na Mamlaka ya kujiita "Walii" au jina lolote jengine, kwa sababu kuanzia hapo wewe ni kiumbe mwengine kabisa, hivi sasa unajijua wewe binaadamu unatamka maneno hayo kila siku, akifa mtu unasema lakini huyajui maana yake, Lakini ukishajijua Kwamba wewe ni Roho, basi kila msiba unao kufika katika dunia hii utalisema neno hilo lilokuwemo kwenye hiyo aya huku umehudhuria, akifa mtu utakua unajua khalifa karudi Nyumbani.
Na ukifikia hali hiyo ukajigundua kuwa wewe ni Roho basi Sala yako itakua ya aina nyengine, vitendo vyako vitabadilika, utakua mwenye (control) ya maisha yako mpaka kuondoka kwenye Ulimwengu huu, hapo tena utakua huna haja ya kupenda mali, kupenda majumba, kupenda mapesa, kupenda watoto, unakua huna haja hiyo, unakua ushajijua kumbe mimi hapa napita tu, kama nilivokuja sina kitu, kumbe duuh mpaka hili jina wamenipa nilipowasili hapa duniani, kuanzia leo sitaki tena Kumuasi Mollah wangu Mpenzi alonikirimu maisha haya ya Ulimwenguni, Na kuanzia sasa nitafanya kazi ya kuwaonea huruma wageni wenzangu, kuwafanyia mema walo karibu yangu, huku nikitaraji kurejea nyumbani wakati wowote alonipangia Mollah wangu.
Kila mmoja yupo Safarini tufanye hima ya kupunguza mizigo tulobeba ili safari ya maisha isizidi kuwa nzito.
Jifahamu wewe nani utapata raha ya maisha ya hapa duniani na huko nyumbani unakorejea.
No comments:
Post a Comment