Asalaam Aleiykum
Sasa swali la kujiuliza au kutafakari ni hili iwapo pamesemwa "Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu" nini habari yetu sisi kuhusu haya maisha yote tunayoishi katika "Ulimwengu huu", ukenda (Deep)Ndani kabisa utagundua kule Kuumbwa kwenyewe kwetu sisi kumetokana na Mapenzi ya Mollah wetu, kwani hujasoma aya iliyomo kwenye sura ya (Insaan aya 1)
هَلۡ أَتَىٰ عَلَى ٱلۡإِنسَـٰنِ حِينٌ۬ مِّنَ ٱلدَّهۡرِ لَمۡ يَكُن شَيۡـًٔ۬ا مَّذۡكُورًا
Hakika ulimpitia Mwanaadamu wakati mrefu katika dahari, hakuwa katika kitu kinachotajwa.
Hali kama hiyo wewe inakuhusu, Jikumbushe pale wazee wako wawili walipofanya maridhiano ya kufunga ndoa Mapenzi yakawateremkia na kukutana katika godoro la mapenzi, nini kilitokezea, kilotokezea hapo ni hiyo (Rehma)ambayo ni wewe, na ndio hiyo(Product of Love).
إِنَّا خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَـٰنَ مِن نُّطۡفَةٍ أَمۡشَاجٍ۬ نَّبۡتَلِيهِ فَجَعَلۡنَـٰهُ سَمِيعَۢا بَصِيرًا
"Kwa Hakika tumemuumba Mwanaadamu (Mtu)kutokana na mbegu ya Uhai iliyochanganyika,(Ya Mwanaume na Mwanamke)Na Tukamfanya Mwenye kusikia na kuona."
Kwa hiyo Wewe ni matunda ya mapenzi, ndio maana wakati mwengine unajihisi mapenzi na wakati mwengine umejaa chuki, (You are Both)Kama utatafakari utaziona hali zote hizo mbili zikikutokezea, yaani una urithi wa jinsia zote mbili, unageuka wakati(mara mama yako, mara baba yako)Jiangalie.
Nini cha kuangalia zaidi kitachokupa Afya na Furaha ni ile hali ya kukumbuka kuwa wewe ni (Full of Love) hiyo ndio (Nature)yako, ukiona mambo ya chuki, ufisadi unakuzungukia toka haraka sana katika hali hiyo, na hiyo ndio itakua dawa yako.
Kwani wewe hukumbuki Umelelewa kwa mapenzi, umeshawahi kujiuliza chanzo cha mapenzi hayo kimetokea wapi?. Majibu yapo kwenye sura ya (Taha aya ya 39)"وَأَلۡقَيۡتُ عَلَيۡكَ مَحَبَّةً۬ مِّنِّى وَلِتُصۡنَعَ عَلَىٰ عَيۡنِىٓ "Na nimekutilia Mapenzi yanaotokana kwangu, na ili ulelewe machoni mwangu, (Maneno hayo anaambiwa Nabii Musa a.s lakini kila mmoja wetu alopita kwenye Ulimwengu huu yanamgusa." Na hivi ndio kila mmoja wetu anavolelewa kwa mapenzi makubwa, Analelewa mtu kwa bawa la huruma, wazazi hawalali usiku kucha, ukiumwa wanahangaika ili wakupe dawa upone, ikisha ukitimia umri wa kuweza kutembea na kujitegemea Mwenyewe hapo wanakuacha kwenye uangalizi wa miujiza utokao kwa Mollah wako.
إِن كُلُّ نَفۡسٍ۬ لَّمَّا عَلَيۡہَا حَافِظٌ۬
"Hakuna Nafsi yoyote ila inayo mchungaji juu yake".
Ulipofika Umri wa kuachiwa huru unapata ulinzi mwengine wa yule aliyeumba mapenzi na kukuletea mchungaji(Malaika)unaambiwa kwa njia usizofahamu hapa usende, kule usipite, gari hii usipande, unanusuriwa na kila mabaya na mabalaa pasi na wewe kuyajua, yote hayo yanafanyika ndani ya kivuli cha mapenzi, "ewe binaadamu upendwe vipi ujijue unapendwa".
Mwanzo Mapenzi Mwisho Mapenzi.
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment