Asalaam Aleiykum
Mie mpenzi sana wa Lugha ya Kiswahili, Lugha ambayo imekusanya maneno kutoka lugha nyingi tafauti na kujiunda lugha moja ya Kiswahili, ndani yake kimo Kihindi, Kiengereza,Kireno,Kiarabu,Kiafrica na lugha nyengine kadhaa, Ndani ya Lugha hii kuna misemo mingi ilo jaa hekima, Mie leo nimechagua msemo ulokua unapendwa na wazee usemao,"Asofunzwa na Mamae hufunzwa na Ulimwengu".
Hapa yametumika maneno yenye thamani kubwa, Maneno ambayo yanaishinda almasi, ukiyazingatia maneno haya utagundua hayajatokea kwenye Akili, Wapi yametokea? hilo ndio dhumuni ya darsa yetu leo.
Nina Tabia niendapo likizo Nyumbani Africa hupendelea kujumuika na vijana kwenye vikao vya kahawa, siku moja wakati tumekaa alipita kijana mmoja maskin anacheka na kuzungumza peke yake, Vijana nilokaa nao wakanambia yakua kijana Mwenzao kapoteza saa, Mimi nikawajibu basi tumsaidie kutafuta, wale walokuwepo pale walicheka sana, Mimi nilifahamu yule kijana ni mgonjwa wa Akili, wao wakanifahamu mimi ni mjinga wa Lugha, na sifahamu chochote, lakini ndani ya Nafsi yangu nilikua nawaangalia jee wale waliopo pale wamefunzwa na Ulimwengu, nikagundua wamesema maneno makubwa lakini hawajui maana yake, kama vile kusema Kiarabu ukawa hujui tafsiri yake.
Sasa mimi leo Nakuchukua katika Safari hii ya "Miujiza Nje ya Akili" ili upate kufahamu kwa uzuri inakuaje ukipoteza saa. nje ya Akili inakuje,Watoto wa Nabii Adam a.s Habil na Kabil Mmoja wao alipomuua mwenzie akabakia kakamata saa hajui afanyeje, Ulimwengu ulimfunza vipi?
فَبَعَثَ ٱللَّهُ غُرَابً۬ا يَبۡحَثُ فِى ٱلۡأَرۡضِ لِيُرِيَهُ ۥ كَيۡفَ يُوَٲرِى سَوۡءَةَ أَخِيهِۚ قَالَ يَـٰوَيۡلَتَىٰٓ أَعَجَزۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِثۡلَ هَـٰذَا ٱلۡغُرَابِ فَأُوَٲرِىَ سَوۡءَةَ أَخِىۖ فَأَصۡبَحَ مِنَ ٱلنَّـٰدِمِينَ (٣١)
Hapo Mwenye enzi Mungu akamleta kunguru anayefukua katika Ardhi ili amuonyeshe jinsi ya kuificha maiti ya ndugu yake, (Akasema yule Ndugu aliyeua) ole wangu nimeshindwa kuwa sawa na kunguru huyu na kuficha maiti ya ndugu yangu, basi akawa miongoni mwa wenye kujuta.
Kwanini akajuta?, kwa sababu Kunguru kaja na hekima, yeye akasoma kupitia kwa Kunguru, Basi kujuta kwake ni kule kumdhulumu ndugu yake na kushindwa kuuhifadhi Mwili wa ndugu yake.
Nimekupa aya hii moja ili iwe muongozo wa darsa yetu, yule ndugu aliyeua ilipomponyoka saa alishuhudia kitendo cha mshangao, Kutokana na amri ya Mwenye enzi Mungu kaletwa kunguru kwa njia ya Hekima ili amuoneshe vipi kuustiri maiti ya ndugu yake. Asofunzwa na Mamae hufunzwa na Ulimwengu.
Saa ilokusudiwa hapo ni hiyo Akili(Mind), Napenda uelewe mambo yote yanotokea katika Akili yanahitaji muda, ndio hiyo saa au ita (Time) ukijumlisha ndio unapata siku, pahala, jana na kesho, hiyo ndio (Time) au (Memory) ukiyapoteza au ukitoka katika (system) hiyo ndio huko kupoteza saa.
Na huko kupoteza saa kupo kwa aina mbili, aina ya kwanza ni ile ya kupoteza Fahamu, ugonjwa wa Akili, (Drugs) N.k, Na aina ya Pili ndio hio Miujiza una (Function)au unaingia kwenye (Eternity)au (Wisdom). (Mfano) ukilala unapoteza saa hujijui, lakini wakati wa kufa unapoteza saa unajijua.
Endelea part 2 uingie kwenye Ulimwengu wa Hekima.
endelea part 2
Friday, December 2, 2016
MIUJIZA NJE YA AKILI PART 2
Asalaam Aleiykum
Naam, Mtoto yumo kwenye hiyo (Hekima)(Wisdom)Lakini hajijui ndio maana hata Kwenye Quraan lilipotajwa jambo la (Hekima) Luqman alimuanza nani? isome Quraan uone vipi inakua kupoteza saa, vipi unajua tafauti ya saa na (Hekima). Anasemaje Mollah wako? Luqman aya ya 12 mpaka 13 na kuendelea. Zama kwenye maneno hayo ujue hekima inatokea wapi.
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا لُقۡمَـٰنَ ٱلۡحِكۡمَةَ أَنِ ٱشۡكُرۡ لِلَّهِۚ وَمَن يَشۡڪُرۡ فَإِنَّمَا يَشۡكُرُ لِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِىٌّ حَمِيدٌ۬
Kwa yakini tulimpa Luqman Hekima(Wisdom), Tukamwambia Mshukuru Mwenye Enzi Mungu, Na atakaeshukuru kwa yakini anashukuru kwa ajili ya Nafsi yake, Na atakae kufuru Mwenye enzi Mungu(Amejitosheleza)Mkwasi asifiwaye, (Si Mwenye kuhitaji shukurani zenu)
Nini (Wisdom)au Hekima? Ni hali au uwezo wa kumiliki Nafsi yako nje ya Akili, au kwa lugha nyengine ni mkusanyiko wa ufahamu mambo yalopita na yajayo ukawa unaishi nayo sasa hivi, hiyo ndio tafsiri ya Rahisi ya hilo jambo la (hekima)lakini hata halijafikia ukaribu wake na kusudio ya hiyo hali ya kuwa na (Hekima).
Anasemaje Luqman? Tulimpa Luqman Hekima, tukamwambia Mshukuru Mollah wako, kwanini ashukuru, kwa sababu kitu hicho ni kitu (Adhimu)ni (State of Knowing),Hiyo ndio Hekima, Binaadamu ukijijua basi unashukuru kwa kupewa neema na rehma hiyo, Mnyama ana lala na wewe unalala, halafu nyote mnaamka, lakini kuna mmoja anajijua kaamka, na huyo ni wewe, Shukuru kwa Neema hiyo ya kuumbwa Mwanaadamu na ukapewa cheo cha kujijua, Shukuru kwa Nafsi yako uko mzima, unavuta pumzi bila ya taabu, unatembea na kurudi bila ya shida, unapata riziki yako kama ilivopangwa, shukuru kwa ajili ya Nafsi yako, na kama hutaki hilo au kumshukuru Mollah wako, Yeye hana (haja na shukuruni yako), endelea kumkanusha, kumpinga na kumuasi na yeye atakunyima miujiza hii nje ya Akili.
Naam sasa toka kwenye saa uingie kwenye miujiza wa (Hekima) za (Luqman), Hekima inakuja kwa njia ya kusubiri, katika Ulimwengu wa sasa Binaadamu kasoma sana, lakini kwa kufanya hivyo kapoteza (Hekima), kwa sababu ya haraka za maisha, ndio maana (Luqman)akaona aanze kwa Kumtahadharisha Mwanawe, kwa sababu (Asiye funzwa na mamae hufunzwa na Ulimwengu).
وَإِذۡ قَالَ لُقۡمَـٰنُ لِٱبۡنِهِۦ وَهُوَ يَعِظُهُ ۥ يَـٰبُنَىَّ لَا تُشۡرِكۡ بِٱللَّهِۖ إِنَّ ٱلشِّرۡكَ لَظُلۡمٌ عَظِيمٌ۬
Na(Wakumbushe)Luqman alipomwambia Mwanawe na hali yakuwa anampa nasiha, Ewe Mwanangu usimshirikishe Mwenye Enzi Mungu, Maana kushirikisha ndiyo dhulma kubwa.
Hapo kuna tafauti kubwa baina ya Baba na mtoto, tafauti yenyewe mwenye hekima hawezi kukupa hekima yake, ila ikitoka kwake inakua nasiha. Nasiha ni tahadhari na hapa kuna maneno makubwa inatupasa kuyazingatia. Kasema Luqman usimshirikishe Mwenye enzi Mungu hakika shirki ni dhulma kubwa.
Katika kuifahamu au kujificha katika aya hii watu wengi wakadhani Shirki ni ile ya kuabudu kitu chengine pekee cha asiekuwa Mwenye enzi Mungu, lakini mengine yote hayapo kwenye Shirki, leo hii nakwambieni ukiapa kwa jina la Mwenye enzi Mungu kiapo cha uongo hiyo ni dhulma na umemshirikisha Mwenye enzi Mungu na ni dhulma kubwa,(Umelitumia jina lake kwenye Uharamia wako).
Ukimuomba asiyekua Yeye basi umemshirikisha, ukimtegemea asiyekua yeye basi umemshirikisha, ukitoa ushahidi wa uongo basi umemshirikisha,Ukenda kwa mganga kuroga umemshirikisha Mollah wako, Kwanini ikawa hivyo? Kwa sababu wewe unazo sifa zake mbili muhimu za (kuona na kusikia)Kheri hii alokupa ndio unaifanya nyenzo ya kuibia au kupata kisicho haki yako, Na hiyo ni dhulma kubwa kabisa. Ndio maana kwenye aya ya 15 Mwenye enzi Mungu wasia wake kwa wanaadamu akasema,Na kuanza na wazazi wako, iwapo wazazi wako wakikulazimisha kunishirikisha mimi basi usiwatii (Abadan).
Endelea Part 3

MIUJIZA NJE YA AKILI PART 3
Asalaam Aleiykum
Tuko katika kutizama (Hekima) za Luqman, Na kwenye aya ya 18 anasema:
وَلَا تُصَعِّرۡ خَدَّكَ لِلنَّاسِ وَلَا تَمۡشِ فِى ٱلۡأَرۡضِ مَرَحًاۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخۡتَالٍ۬ فَخُورٍ۬
Wala usiwatizame (Watu kwa Jeuri)kwa upande mmoja wa uso(Dharau)wala usende katika nchi kwa maringo, Hakika Mwenye enzi Mungu Hampendi kila ajivunae, ajifahirishaye.
Ukiingia au kupewa Hekima unajua Mwenye Enzi Hapendi wala kuchukia kwa sababu Yeye hana mfano wa Binaadamu, lakini kwa ajili ya kuwasiliana na wewe ndio yakatumika maneno hayo, Lakini ndani ya maneno ya Luqman kwenye hekima yake anajua kuwa Wanaadamu wana (Energy)maalum inayotoka katika Roho zao, kutokana na nguvu za (Energy)hiyo Mwenye enzi Mungu anakuondoshea kinga yake kwa yale unayowafanyia wenzio, na maringo yako, ndio mara unaanguka kimaisha au kupata maradhi.
Nimemtumia Luqman kuonesha ukipewa Hekima unakua mtu wa aina gani. Mama akishirikiana na Ulimwengu anakulea taratibu, kama vile Mti unavokua, mboga zinavyochipua, matunda yanavo wiva, Ulimwengu hautaki haraka unakwenda na sheria ilivopangwa.
Sasa ukija na Ujana wako umebeba saa, unaishi ndani ya saa yako, ndio utajiona uko mbioni unahangaika na maisha, Ama Mtu mzima yeye ana (Option)kwa sababu kashapewa nasiha, Akitaka na kuridhiwa na Mollah wake ana uwezo wa kuingia kwenye Hekima, Na kama hakutaka basi atabakia na saa lake mpaka kufa kwake.
Sasa ukiingia au kupewa Hekima Miujiza gani inatokezea?.
Kwa Mara ya Mwanzo unapata utulivu wa Akili, unakua hupangi au kuamua mambo kwa kutumia Akili, huoni au kuangalia kwa kutumia Akili, Kwa Mara ya Mwanzo unapata mambo kwa uhakika, hapo tena unajijua rasmi kama utakufa, ukioneshwa rangi ya kijani unaiyona kwa uhalisia wake, hukioni chama au bendera unaona (Pure)green na kazi zake, Kwa mara ya mwanzo unapata kuwasiliana na Roho yako, Na Maswali na majibu yanatoka kwenye hiyo (Source), Hukurupuki na kujibu maswali ovyo ovyo kama ufanyavo hivi sasa, Naam hiyo ndio Hekima, na hayo kwako ndio yatakua miujiza ya kuipoteza hiyo saa ulonayo hivi sasa.
Sasa Pazia linaondoshwa ukiwa hai baina ya Akili na Roho yako, hiyo ndio Hekima. Madhanmbi unayaona kwenye asili yake na madhara yake, sasa hivi unajua dhanmbi lakini hujui dhara yake, omba au ingia kwenye Hekima uone dhara yake. Ingia kwenye Muujiza huu wa Hekima upate kuona mambo kwenye original yake, Hekima ni haki yako fanya jitihada upoteze saa ili uipate hekima, najua unashituka kuipoteza saa yako, lakini kumbuka saa umeinunua kutoka kwa wazee wako, walimu wako, marafiki zako, lakini Hekima ni (Original)yako, kumbuka ulivokua mtoto ukawa unashangaa hichi nini na kile nini, rejea tena kule kwa mara ya pili ukashuhudie Miujiza, kaipate (Truth), Ndio Maana Mwenye enzi mungu akasema sura ya (Baqarah aya ya 269)
يُؤۡتِى ٱلۡحِڪۡمَةَ مَن يَشَآءُۚ وَمَن يُؤۡتَ ٱلۡحِڪۡمَةَ فَقَدۡ أُوتِىَ خَيۡرً۬ا ڪَثِيرً۬اۗ وَمَا يَذَّڪَّرُ إِلَّآ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَـٰبِ
Mwenye enzi Mungu humpa hekima amtakaye, Na aliyepewa Hekima bila shaka amepewa kheri nyingi, Na hawakumbuki ila wenye Akili.
Kwa hiyo ni vizuri kuwa na hiyo saa ambayo itakufanya uikumbuke hiyo Hekima, na Akili imewekwa ni kama sehemu ya kuchupia uende kwenye hiyo Hekima, Muujiza uko hapo katika kukumbuka ukachupa.
Wacha niendelee kufafanua ili ufahamu vizuri, Elimu ni Mafunzo ya Nafsi, Sheikh kakwambia hivi, Mwalimu kakwambia vile, watu wanasema haya, na wewe unajua hili, ni mambo katika Ulimwengu huu yaloletwa na hiyo saa, Lakini hekima ni Mafundisho ya Kiroho ambayo yanatoka kwa Mwenyewe subhanna, kama vile ukitia mbegu kwenye Ardhi unatokeza kuwa Mti, Kwa hiyo Elimu ni jambo litokealo nje, Na hekima ni jambo unalolipata kutokea ndani, kumbuka la kwanza kutokea kwenye Akili na la pili ni lile litokalo kwenye Roho.
Unaweza Ukapewa Kitabu, umesoma na (PHD)lakini ukawa hukupewa Hekima, unakua na hasara kubwa, kile cha muhimu huna, umebakia na saa lako, ndio maana ukipewa Hekima unaambiwa Ushukuru kama alivo (Shukuru)Luqman.
Sasa Muujiza nje ya Akili ni upi, Ni ule uwezo wa kuishi katika (State)au hali Mbili, Ya kwanza ni ile ya Mnyama, unalala, unakula, Na ya pili ni ile ya Ubinaadamu ya kuelewa (There is something beyond)Unakumbuka na kusahau, unapita katika hali hizi mara umeponyoka umetenda dhanmbi, halafu unakumbuka unarudi tena na kutubu, ukiwa katika hali hiyo ya kukumbuka huo ndio muujiza wenyewe na ukipewa ukawa unakumbuka daima huo ndio ucha Mungu, na kuishi katika kukumbuka ndio huko kuipoteza saa, sababu saa inabadilika lakini kukumbuka kuko vile vile, Ukiingia kwenye sala, ukitoka wewe uko vile vile mpaka ukilala unajijua wewe nani, Na ukiamka unajijua wewe nani hubadiliki, kumbuka saa yako inabadilika lakini hekima yako iko vile vile. Ishi kwenye hekima upate Miujiza yake na hutotaka kutoka tena kwa Uwezo wa Mollah wako.

Subscribe to:
Posts (Atom)