Asalaam Aleiykum
Katika Ulimwengu huu kuna vitu Binaadamu lazima uvijue kabla ya Mauti yako, Na kama hufanyi jitihada za kuvijua basi utaondoka kwenye Ulimwengu huu kama ulivokuja, itakua kama alivokufa kuku na wewe hakuna tafauti. Kwanini nikasema hivyo kwa sababu Mwenye enzi Mungu katupa sisi Fahamu za kujijua(Awareness)au Tuite kwa Lugha unayofahamu wewe (Roho), Kwanini nikasema kwa lugha, kwa sababu hujui bado nini hiyo (Roho)Japokua unayo Mwenyewe, Unajua kwa kutumia lugha lakini sio kitendo cha kufahamu.
Sasa nakuchukua kidogo kidogo katika darsa zangu asaa unaweza kuacha kushangaa (Ferry au Forodhani) Na ukaelekeza Mshangao wako kwenye Mbingu, Tembea na mimi kwenye Bustani hii ya kujua mambo ya Sayansi mbili ile ya ndani na nje katika Ulimwengu huu. Mwenye enzi Mungu katutaka sana katika kitabu chake kwa kutuonesha Tufikiri, Tutafakari, tutumie Nyenzo ya Akili ili apate kutufungulia mambo. Na ukiwa na Sayansi hii ya ndani basi mambo mengi unayajua (In-Advance)Kuna vitu vimeumbwa kama Usingizi, Njaa, Uzima, Kuamka, Usiku, Pumzi na mengi katika Ulimwengu huu ya sayansi ya ndani lakini hakuna hata mmoja mwenye kutaka kuingia katika darsa hizo na kujua vipi nalala au vipi naamka, vipi njaa inakuja wakati gani, vipi navuta pumzi, kwani ukiweza kuvijua vitu hivyo ndipo utaweza kujijua kama wewe ni Roho, lakini najua woga uko pale utakapo kutana na ukweli wa Mauti, utakapojua siku zako zimekaribia, ndio maana wengi tunajificha kwenye muziki, tunajificha kwenye mipira, siasa, ulevi, yote hayo ni mambo ya kujishaulisha hii sayansi ya ndani, basi ikiwa hiyo hatuiwezi, kwanini hatuongezi nguvu za Imani kwa kuijua sayansi ya Nje japokua tumefanyiwa na wenzetu ili tupate kuamini.
Miaka Elfu moja na Mia Nne Mwenye enzi Mungu alitutumia kitabu kupitia kwa Mtume wake s.a.w, ndani ya kitabu hicho alisema maneno haya yaliyomo kwenye aya ya 12 sura ya (Talaq).
ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَ سَبۡعَ سَمَـٰوَٲتٍ۬ وَمِنَ ٱلۡأَرۡضِ مِثۡلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ ٱلۡأَمۡرُ بَيۡنَہُنَّ لِتَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىۡءٍ۬ قَدِيرٌ۬ وَأَنَّ ٱللَّهَ قَدۡ أَحَاطَ بِكُلِّ شَىۡءٍ عِلۡمَۢا (١٢
Mwenye Enzi Mungu Ni Yule ambaye ameziumba Mbingu saba, Na Ardhi kuwa mfano wa hizo, Amri (zake) zinashuka baina yao, ili mjue kwamba Mwenye enzi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu, Na kwamba Mwenye enzi Mungu amekizunguka kila kitu kwa Elimu(Ujuzi)wake.
Katika aya hiyo hapo kuna neno itabidi ulizamie kusudio lake kwa ajili ya kuendelea uzuri na darsa yetu hii, tupia macho sentensi moja pekee isemayo,(Ili Mjue kwamba Mwenye enzi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu)kulikua na watu wanakitilia shaka kitabu cha Quraan na kukifananisha na (Bible)pale ilipotolewa makosa na (Galileo)aliposema Dunia sio (Centre of Everthings)haiko kati dunia, ila dunia inalizunguka jua, Walikuja juu viongozi baada ya kuona maneno hayo yamekwenda kinyume na kitabu, Wakamwambia abadilishe kauli yake.Kwa miaka mingi watu wakawa wanatafuta kuikosoa Quraan na hayo maneno yaliyomo kwenye hiyo aya ya kusema kuna Ardhi saba. Alosema maneno haya alikua Mwana sayansi wa (Inner science)akiishi Jangwani katika Bara la Arab, hakua na vifaa vyovyote vya kuchungulia huko Mbinguni, hivi majuzi Wanasayansi wa (Outer science) wamekuja na ugunduzi wao na kusema kweli tumeziona Ardhi saba zenye kufatana kwa Tabaka kama zilivo tajwa kwenye Quraan, Yafatilie maelezo hayo ya ugunduzi huo kupitia (NASA) na tafuta uvumbuzi huo wa hivi karibuni wa ardhi saba unaoitwa (Trappist-1planet discovery). tunapewa habari hizi ili kuzidisha Imani zetu, ili kupewa uthibitsho wa haki kuwa yupo Muumbaji, tumeoneshwa mfano wa Ardhi saba na bado hatujui ziko hizo tu au ziko zengine ambazo zimetapakaa kwenye Ulimwengu huu. Sasa Kwanini zikatajwa?.
Endelea part 2
Asalaam Aleiykum
Zimetajwa ili upate uhakika sio wa kusoma bali wakujua, Kwa sababu kidole hakisomeshi, kidole kinaonesha, Sasa kidole hichi kwanza kimekuonesha hiyo aya kabla ya ugunduzi, na hivi sasa kinakutaka utizame Mbinguni, ukibakia unashangaa kwenye kidole utakua huoni kitu Mbinguni, Sasa umepewa uhakika wa jambo hilo na vizuri zaidi hizo Ardhi haziko mbali ni kama miaka 40(40 light years away)kwa hesabu ya sayansi ni karibu sana.
Unatakiwa sasa ujiulize swali, Ikiwa nimeambiwa Ardhi saba na Mbingu Saba ziko kwa Mfano huo huo, ina maana pia uwezekano wa zenyewe kuonekana pia uko karibu?, Tatizo sio kuonekana, tatizo ni kuzijua nini khassa hizo Mbingu, Mpaka hii leo hatujui, au imefichwa katika elimu zetu kutambua nini Mbingu. tumetajiwa kwenye sura ya (Mulk aya ya tatu)kuwa Zimeumbwa Mbingu kwa Tabaka, na aya ya (tano)ikasema "Tukaipamba hii Mbingu ya Karibu kwa Mataa", lakini tukionacho sisi ni hiyo Taa na wala sio Mbingu, Furaha kubwa kuwa Wanasayansi wadunia wanaendelea na Ugunduzi wao na hapana shaka watapata jawabu la swali hilo kwa Uweza wa Mollah hivi karibuni.
Aya ya hapo juu inataja kwa kusema Mwenye enzi Mungu kakizunguka kila kitu kwa (Kukijua), Na kwanini isiwe hivyo wakati yeye ndie aliyeviumba, kila kitu katika Ulimwengu huu kina elimu yake, kina (Intelligence) yake, Utizame Mwili wako(Body) unavofanya kazi zake bila ya kuingiliwa na wewe, kumbuka wewe ni tafauti na huo Mwili wako, wewe umebebwa tu na huo Mwili, tizama unavosaga chakula, tizama unavosikia, tizama unavoona na mambo mengine ya ndani, ulikaa ukazingatia hayo, basi na hali kama hiyo kidole kinakuonesha tena aya ya 18 sura ya (Hajj)ili upate kuyajua mambo.
أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يَسۡجُدُ لَهُ ۥ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَمَن فِى ٱلۡأَرۡضِ وَٱلشَّمۡسُ وَٱلۡقَمَرُ وَٱلنُّجُومُ وَٱلۡجِبَالُ وَٱلشَّجَرُ وَٱلدَّوَآبُّ وَڪَثِيرٌ۬ مِّنَ ٱلنَّاسِۖ
Jee huoni ya kwamba Mwenye enzi Mungu kinamsujudia kila kilichomo Mbinguni na kilichomo Ardhini na Jua na Mwezi na Nyota na Milima na Miti na Wanyama na wengi miongoni mwa Watu?(Mpaka Mwisho wa aya inavoendelea).
Hapo juu limetajwa neno"Huoni"haikusemwa"Hutizami"kutizama ni jambo la mbali lakini kuona ni jambo la karibu, unatakiwa uwe Mwana sayansi wa (Inner)ndani ili uweze kuona, ikiwa (Body) yako ina(Elimu)ya kutosheleza ya kujiendesha basi kutokana na aya hiyo kidole kinaonesha tena uwepo wa (Conscious Level of Mind)tabaka ya ufahamu kwa ajili ya vitu hivyo, Na lazima ufahamu huo upo katika (Level)saba. Ndio Maana utaona vinyama vinajenga na kunyonyesha, vinazungumza, Miti inazungumza, Mawe pia yana fahamu, Milima inazungumza, jua pia lina fahamu zake, Mwezi nao una mambo yake una (Control) bahari mpaka hedhi za wanawake, lakini yote hayo mnatakiwa mkae na mtafute elimu hizi za ndani ili mpate kuyajua, isiwe unaambiwa Milima na jua na mwezi vinamsujudia Mollah wao, ukawa unashangaa, unastaajabu kwa sababu huyajui mambo, ukikuta wenye elimu zao wanazungumza na Mti utaona huyooo sasa hivi ataanza kupiga kelele, Ulimwengu huu kila jambo limezungukwa na elimu ya Mwenye Enzi Mungu, Na upeo wa Mwenye enzi Mungu ni Mkubwa wala hauna mpaka.
Na haya yote yamefanywa ili Wewe upate kumjua Mollah wako, usije kuleta ubishi pale unaposomewa aya ya Mwenye enzi Mungu inayosema :يَوۡمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ ٱمۡتَلَأۡتِ وَتَقُولُ هَلۡ مِن مَّزِيدٍ۬(Qaf aya ya 30)
Siku tutakapoiambia Jahannam Jee, Umejaa Nayo Itasema Je kuna zaidi?. Mpaka Moto nao Umeumbwa na unafahamu na unajua ukuadhibu vipi, ndio maana ukajibu iko zaidi.
Kidole kinaendelea Kuonesha Mbinguni basi na wewe endelea kutizama.sehemu ya 3
Asalaam Aleiykum
Wale wenye kuhudhuria Umauti wa mtu wanajua au wanofanya kazi (Hospital)Wanajua Mtu akiwa anakufa Macho yanabiruka na kutizama Mbinguni au ita Juu, Kidole kinatwambia nini kuhusu swali hili,( Quraan aya ya 22 sura ya Adh-Dhaariyat)
وَفِى ٱلسَّمَآءِ رِزۡقُكُمۡ وَمَا تُوعَدُونَ
"Na Katika Mbingu ziko Riziki zenu na Mliyoahidiwa".
Kuanzia leo Ukitizama Mbinguni ujue kule ndio inakopangwa Riziki yako upate ngapi, uwe na nini? na kiasi gani, kule Mbinguni ndiko tunanyanyua Mikono yetu kuonesha uwazi wa viganja vyetu kwa kuomba tukitaraji kupewa na Mollah wetu, Huko Mbinguni ndiko tunakotoa sauti zetu zisikike ili tupate kujibiwa dua zetu(Vipi leo mnatwambia tunyamaze kimya)huko huko Mbinguni ndiko siku ya kufa kwako unapelekwa na Malaika kama (Destination)ya mapumziko katika Makaazi yaitwayo(Barzaak).
Kwa hiyo ukiwa unatizama Mbinguni napenda uelewe yale Mloahidiwa mabaya ya (Moto)Na Mazuri ya (Pepo)yote yako huko, kwa hiyo kaa ukijua Safari unayo ya Kwenda Mbinguni, nasisitiza usije kuangalia Kidole, kwani kidole kinabaki hapa hapa ila tizama kinaonesha wapi. Kaa tayari kusikia Miujiza zaidi itokayo huko, Pata faida usikize kisa cha Miraji ili upate uyakinifu wa hayo yaloonekana huko Mbinguni ambayo na wewe hakuna shaka utakwenda kuyaona.