Asalaam Aleiykum
Zimetajwa ili upate uhakika sio wa kusoma bali wakujua, Kwa sababu kidole hakisomeshi, kidole kinaonesha, Sasa kidole hichi kwanza kimekuonesha hiyo aya kabla ya ugunduzi, na hivi sasa kinakutaka utizame Mbinguni, ukibakia unashangaa kwenye kidole utakua huoni kitu Mbinguni, Sasa umepewa uhakika wa jambo hilo na vizuri zaidi hizo Ardhi haziko mbali ni kama miaka 40(40 light years away)kwa hesabu ya sayansi ni karibu sana.
Unatakiwa sasa ujiulize swali, Ikiwa nimeambiwa Ardhi saba na Mbingu Saba ziko kwa Mfano huo huo, ina maana pia uwezekano wa zenyewe kuonekana pia uko karibu?, Tatizo sio kuonekana, tatizo ni kuzijua nini khassa hizo Mbingu, Mpaka hii leo hatujui, au imefichwa katika elimu zetu kutambua nini Mbingu. tumetajiwa kwenye sura ya (Mulk aya ya tatu)kuwa Zimeumbwa Mbingu kwa Tabaka, na aya ya (tano)ikasema "Tukaipamba hii Mbingu ya Karibu kwa Mataa", lakini tukionacho sisi ni hiyo Taa na wala sio Mbingu, Furaha kubwa kuwa Wanasayansi wadunia wanaendelea na Ugunduzi wao na hapana shaka watapata jawabu la swali hilo kwa Uweza wa Mollah hivi karibuni.
Aya ya hapo juu inataja kwa kusema Mwenye enzi Mungu kakizunguka kila kitu kwa (Kukijua), Na kwanini isiwe hivyo wakati yeye ndie aliyeviumba, kila kitu katika Ulimwengu huu kina elimu yake, kina (Intelligence) yake, Utizame Mwili wako(Body) unavofanya kazi zake bila ya kuingiliwa na wewe, kumbuka wewe ni tafauti na huo Mwili wako, wewe umebebwa tu na huo Mwili, tizama unavosaga chakula, tizama unavosikia, tizama unavoona na mambo mengine ya ndani, ulikaa ukazingatia hayo, basi na hali kama hiyo kidole kinakuonesha tena aya ya 18 sura ya (Hajj)ili upate kuyajua mambo.
أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يَسۡجُدُ لَهُ ۥ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَمَن فِى ٱلۡأَرۡضِ وَٱلشَّمۡسُ وَٱلۡقَمَرُ وَٱلنُّجُومُ وَٱلۡجِبَالُ وَٱلشَّجَرُ وَٱلدَّوَآبُّ وَڪَثِيرٌ۬ مِّنَ ٱلنَّاسِۖ
Jee huoni ya kwamba Mwenye enzi Mungu kinamsujudia kila kilichomo Mbinguni na kilichomo Ardhini na Jua na Mwezi na Nyota na Milima na Miti na Wanyama na wengi miongoni mwa Watu?(Mpaka Mwisho wa aya inavoendelea).
Hapo juu limetajwa neno"Huoni"haikusemwa"Hutizami"kutizama ni jambo la mbali lakini kuona ni jambo la karibu, unatakiwa uwe Mwana sayansi wa (Inner)ndani ili uweze kuona, ikiwa (Body) yako ina(Elimu)ya kutosheleza ya kujiendesha basi kutokana na aya hiyo kidole kinaonesha tena uwepo wa (Conscious Level of Mind)tabaka ya ufahamu kwa ajili ya vitu hivyo, Na lazima ufahamu huo upo katika (Level)saba. Ndio Maana utaona vinyama vinajenga na kunyonyesha, vinazungumza, Miti inazungumza, Mawe pia yana fahamu, Milima inazungumza, jua pia lina fahamu zake, Mwezi nao una mambo yake una (Control) bahari mpaka hedhi za wanawake, lakini yote hayo mnatakiwa mkae na mtafute elimu hizi za ndani ili mpate kuyajua, isiwe unaambiwa Milima na jua na mwezi vinamsujudia Mollah wao, ukawa unashangaa, unastaajabu kwa sababu huyajui mambo, ukikuta wenye elimu zao wanazungumza na Mti utaona huyooo sasa hivi ataanza kupiga kelele, Ulimwengu huu kila jambo limezungukwa na elimu ya Mwenye Enzi Mungu, Na upeo wa Mwenye enzi Mungu ni Mkubwa wala hauna mpaka.
Na haya yote yamefanywa ili Wewe upate kumjua Mollah wako, usije kuleta ubishi pale unaposomewa aya ya Mwenye enzi Mungu inayosema :يَوۡمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ ٱمۡتَلَأۡتِ وَتَقُولُ هَلۡ مِن مَّزِيدٍ۬(Qaf aya ya 30)
Siku tutakapoiambia Jahannam Jee, Umejaa Nayo Itasema Je kuna zaidi?. Mpaka Moto nao Umeumbwa na unafahamu na unajua ukuadhibu vipi, ndio maana ukajibu iko zaidi.
Kidole kinaendelea Kuonesha Mbinguni basi na wewe endelea kutizama.sehemu ya 3
No comments:
Post a Comment