Friday, March 3, 2017

KIDOLE KINAONESHA MBINGUNI PART 1

Asalaam Aleiykum

Katika Ulimwengu huu kuna vitu Binaadamu lazima uvijue kabla ya Mauti yako, Na kama hufanyi jitihada za kuvijua basi utaondoka kwenye Ulimwengu huu kama ulivokuja, itakua kama alivokufa kuku na wewe hakuna tafauti. Kwanini nikasema hivyo kwa sababu Mwenye enzi Mungu katupa sisi Fahamu za kujijua(Awareness)au Tuite kwa Lugha unayofahamu wewe (Roho), Kwanini nikasema kwa lugha, kwa sababu hujui bado nini hiyo (Roho)Japokua unayo Mwenyewe, Unajua kwa kutumia lugha lakini sio kitendo cha kufahamu.
Sasa nakuchukua kidogo kidogo katika darsa zangu asaa unaweza kuacha kushangaa (Ferry au Forodhani) Na ukaelekeza Mshangao wako kwenye Mbingu, Tembea na mimi kwenye Bustani hii ya kujua mambo ya Sayansi mbili ile ya ndani na nje katika Ulimwengu huu. Mwenye enzi Mungu katutaka sana katika kitabu chake kwa kutuonesha Tufikiri, Tutafakari, tutumie Nyenzo ya Akili ili apate kutufungulia mambo. Na ukiwa na Sayansi hii ya ndani basi mambo mengi unayajua (In-Advance)Kuna vitu vimeumbwa kama Usingizi, Njaa, Uzima, Kuamka, Usiku, Pumzi na mengi katika Ulimwengu huu ya sayansi ya ndani lakini hakuna hata mmoja mwenye kutaka kuingia katika darsa hizo na kujua vipi nalala au vipi naamka, vipi njaa inakuja wakati gani, vipi navuta pumzi, kwani ukiweza kuvijua vitu hivyo ndipo utaweza kujijua kama wewe ni Roho, lakini najua woga uko pale utakapo kutana na ukweli wa Mauti, utakapojua siku zako zimekaribia, ndio maana wengi tunajificha kwenye muziki, tunajificha kwenye mipira, siasa, ulevi, yote hayo ni mambo ya kujishaulisha hii sayansi ya ndani, basi ikiwa hiyo hatuiwezi, kwanini hatuongezi nguvu za Imani kwa kuijua sayansi ya Nje japokua tumefanyiwa na wenzetu ili tupate kuamini.
Miaka Elfu moja na Mia Nne Mwenye enzi Mungu alitutumia kitabu kupitia kwa Mtume wake s.a.w, ndani ya kitabu hicho alisema maneno haya yaliyomo kwenye aya ya 12 sura ya (Talaq).
ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَ سَبۡعَ سَمَـٰوَٲتٍ۬ وَمِنَ ٱلۡأَرۡضِ مِثۡلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ ٱلۡأَمۡرُ بَيۡنَہُنَّ لِتَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىۡءٍ۬ قَدِيرٌ۬ وَأَنَّ ٱللَّهَ قَدۡ أَحَاطَ بِكُلِّ شَىۡءٍ عِلۡمَۢا (١٢
Mwenye Enzi Mungu Ni Yule ambaye ameziumba Mbingu saba, Na Ardhi kuwa mfano wa hizo, Amri (zake) zinashuka baina yao, ili mjue kwamba Mwenye enzi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu, Na kwamba Mwenye enzi Mungu amekizunguka kila kitu kwa Elimu(Ujuzi)wake.
Katika aya hiyo hapo kuna neno itabidi ulizamie kusudio lake kwa ajili ya kuendelea uzuri na darsa yetu hii, tupia macho sentensi moja pekee isemayo,(Ili Mjue kwamba Mwenye enzi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu)kulikua na watu wanakitilia shaka kitabu cha Quraan na kukifananisha na (Bible)pale ilipotolewa makosa na (Galileo)aliposema Dunia sio (Centre of Everthings)haiko kati dunia, ila dunia inalizunguka jua, Walikuja juu viongozi baada ya kuona maneno hayo yamekwenda kinyume na kitabu, Wakamwambia abadilishe kauli yake.Kwa miaka mingi watu wakawa wanatafuta kuikosoa Quraan na hayo maneno yaliyomo kwenye hiyo aya ya kusema kuna Ardhi saba. Alosema maneno haya alikua Mwana sayansi wa (Inner science)akiishi Jangwani katika Bara la Arab, hakua na vifaa vyovyote vya kuchungulia huko Mbinguni, hivi majuzi Wanasayansi wa (Outer science) wamekuja na ugunduzi wao na kusema kweli tumeziona Ardhi saba zenye kufatana kwa Tabaka kama zilivo tajwa kwenye Quraan, Yafatilie maelezo hayo ya ugunduzi huo kupitia (NASA) na tafuta uvumbuzi huo wa hivi karibuni wa ardhi saba unaoitwa (Trappist-1planet discovery). tunapewa habari hizi ili kuzidisha Imani zetu, ili kupewa uthibitsho wa haki kuwa yupo Muumbaji, tumeoneshwa mfano wa Ardhi saba na bado hatujui ziko hizo tu au ziko zengine ambazo zimetapakaa kwenye Ulimwengu huu. Sasa Kwanini zikatajwa?.
Endelea part 2 










No comments:

Post a Comment