Sunday, April 2, 2017

USINGIZI WA ROHO PART 3

Asalaam Aleiykum
Naam sasa turudi nyuma tujue nini kinacho kufanya uendelee kulala wakati ushaamka, na hilo ndio lenye kuchangia matatizo yako yote, ukiweza kulijua hilo na kulimiliki basi utakua Mwenye kufuzu. Sasa Wacha nikurudishe mwanzo pale unapoamka, kitu cha mwanzo kabisa kinatokea wakati ule ni kwanza unakua hujijui, baada ya (seconds)kadhaa unapata fahamu ya kujijua(Jitizame wewe kila ukiamka utaijua siri hii)hapo ndipo inapatikana (Separation)angalia kwa makini, kuwa mtulivu utaiona hali hiyo ambayo mimi naita(Presence)Hali ya uwepo, ni (Gap)ambayo bado huja(Connect)na(Mind)Yako.
Na kama utakua Mtu Mwenye Utulivu wa (Mind)basi unaweza kuona kumbe mimi na (Body)yangu ni vitu viwili tafauti, Na huo ni Muujiza mkubwa, siku utakayoona Mwili wako na wewe upo pembeni unautizama ndio siku utakayo badilika (Forever), wala usishtuke bado hujafa, hiyo ni (Gap)inapatikana kwa (seconds)chache lakini hasara yako huzioni kwa sababu unaruka na kujiunga na Akili moja kwa moja, Na Mollah ameitaja Akili kwa kusema katika sura ya (Qalam aya ya mwanzo)"نٓ‌ۚ وَٱلۡقَلَمِ وَمَا يَسۡطُرُونَ"
"Nuun"(Naapa kwa )Kalamu na yale waandikayo (Kwa kalamu hizo).
Kalamu yenyewe ndio hiyo Akili yako, sasa hebu ichunguze kalamu yako inaandika nini kwa siku, hiyo (Bio computer) yako inakusanya mambo mangapi kwa siku, kumbuka wewe umo ndani unaletewa taarifa huku umelala, (Mind)au Akili yako ndio yenye kufanya kazi, sasa kila ukiamka unavuta (Mafile)ya jana unaendelea nayo, huku ukitaarisha (Mafile)ya kesho, na hivi ndivo unavoendelea kuuchapa usingizi, (leo Mimi nipo najaribu kushare na wewe ujuzi huu)ili upate kuamka kiroho, huna haja ya kuiachia Akili ikufanyie kazi zote, Pata (direct communication ), ndio maana sasa hivi Sala zako, unakwenda hupo kabisa, unasali sikatai lakini inayokuongoza katika hiyo Sala ni akili, Roho imelala, ndio utajikuta mpaka unatukana ndani ya sala, unafonya, unauza na kununua humo humo kwenye Sala, umefunga sala umesimama unaonesha kidole cha shahada, bado hujijui kama umelala?, Jitizame wewe hata ukila mawazo yako kwengine hata raha ya chakula huoni, uko na mke au mume mekaa pamoja lakini wapi huyu yuko mpirani yule yuko kwenye taarab, halafu unageuka hanipendi, (inasikitisha sana ninapoona wana ndoa wanateseka kwa jambo la kipuuzi)Wengine wamo mpaka Misikitini, Wengine Maimamu lakini bado wamelala, wanadanganya wenzao, viburi vimewashika wanajiona wao ndio wenye kufanya mema, basi hebu amka uchungulie buku lako japo kidogo uone kama kweli unakwenda Peponi?.
Sasa nini kinatokea?, pale unapoamka(Awaken)kila siku unapewa nafasi hii ya kuamka lakini huitaki, wewe unafanya nini? jiangalie pale mwanzo usingizi unapokwisha, baada ya kuhudhuria muujiza uliopo hapo, wewe unarejea tena kulala, unajaribu kufunga macho, unageuka huku na kule, hiyo yote ni ile mbinu ya kujiunga tena na akili na kuendelea na mambo uloyaacha jana. Na Akili ikiona Mzee Kumbe Mvivu,(Watchman)hatizami nyumba yake, Hapo ndipo mfanyakazi anakamata madaraka, anachukua dhamana zote, na huyo mfanyakazi ndio hiyo Akili au (Mind)ambayo inakusanya yote mabaya na mazuri, lakini tabia ya mfanyakazi huyu haipendi mazuri, kwa sababu mazuri yote yanamilikiwa na (Roho), ndio maana utaona mambo mema rahisi kusahauliwa, na yale maovu yanakumbukwa kila mara kwa sababu ya hiyo Akili.
Sasa ufanye nini Mja wewe, kinatakiwa kitu kimoja uzijue mbinu za kumzuia mfanyakazi (Mind)isikutawale(stop the Mind then you are awake). na ukiamka ndio Uwalii, ukiamka  ndio ucha Mungu, na nikisema ukiamka usidhani ulilala (Roho)hailali kinacho lala ni kiwiliwili chako(Ndio maana kwenye baadhi ya dua unasema mimi nimedhulumu nafsi dhulma kubwa kabisa)basi ukishaamka hufanyi dhulma tena, tabia zako zitabadilika, sio kwa kulazimisha na kujifanya Mcha Mungu, laa unakua Mcha Mungu (automatic)sio Ucha Mungu wa (wazimu) bali wa haki na mapenzi kwa ajili ya Mollah wako, na hapo kila kitu kinafunguliwa kwako, Riziki zako zitakuja kwa njia isojulikana, Dua zako zitakubaliwa kwa njia ya Maajabu, Sala zako zitakua hazina khitilafu kabisa, Maisha yako yatageuka yatakua ya (Blissful)na kila ataesogea karibu na wewe atakua anapata mambo ya kiajabu, atasikia furaha, mara atacheka, mara atataka kulia hajui nini kimetokea, akiwa karibu na wewe anahisi mambo ya kiajabu yanatokea lakini hajui chanzo chake, na Ulimwengu huu utauona kwa njia nyengine kabisa, kuna mambo yaso mwisho yatafunguliwa kwako, kinachotakiwa (Just)Amka(Then Blessing)(Then Benediction)(Then You are Awaken the rest is History).lakini kumbuka kitu kimoja isimamishe hiyo kalamu kuandika usoyataka. Mie sio mtoa Mawaidha ila ntakukumbusha baadhi ya mambo unayoambiwa yakusaidie kusimamisha kalamu yako, kama dondosha macho yako usitizame vya haramu, funga masikio yako usisikilize haramu, kwa maana nyengi jilinde na mambo ya kipuuzi, kidogo kidogo utaanza kuisimamisha Akili kuandika usoyataka.Na Akili ikisimama (Roho)inaamka, huna haja mpaka upigiwe honi, au uamshwe usingizini, utakua huna haja ya kuambiwa Sala bora kuliko usingizi, utakua unajua Mwenyewe, na huko ndiko kuamka, sio mpaka akwambie mtu, nenda peponi kwa mguu wako mwenyewe.
Na wapi utaanzia mazoezi haya ya kuisimamimsha hiyo Akili, hakuna kwengine isipokua kulifunua guo la usiku, ukanyanyuka nyakati za usiku na kufanya Ibada, kwani wakati huo umetajwa ndani ya (Quraan Muzzamil aya ya 6)
"إِنَّ نَاشِئَةَ ٱلَّيۡلِ هِىَ أَشَدُّ وَطۡـًٔ۬ا وَأَقۡوَمُ قِيلاً "
Hakika kuamka usiku(na kufanya Ibada)kunawafikiana zaidi na moyo, Na maneno (Yake)yanatuwa zaidi.
Msiseme haya ni maneno yangu, aya inathibitisha hapo juu kuhusu kuisimamisha Akili, Angalia vizuri tafsiri ya aya, halafu utizame ukimya wa maneno unasemaje?. Kwanza kwanini uamke?, Kwa sababu unatakiwa ukalale mapema, ukisha kulala mapema hiyo kalamu yako (Akili)inachambua Ma(File)yako yote ya Mchana kutwa, Ikisha unapoamka Akili ina(Stop). Sasa jiulize kwa sababu gani Maneno yanatuwa zaidi, kwa sababu Akili ishaanza kupunguza kazi za uchambuzi, kwa hiyo maneno utakayo yasoma moja kwa moja yanateremka kwenye moyo, na hapo inakua kama ulojifundisha (Baskeli)husahau tena, Mawasiliano ni baina ya (Roho) ilo macho na Nafsi yenye kupokea, ukiigundua hali kama hiyo ukawa unaishi nayo Mchana kutwa, basi wewe utakua (Msalihina, Muttakina,Musabihinna,Mudhakirinna)kila kitu utakua wewe. Pata kuamka Uipate zawadi ya kudumu.

No comments:

Post a Comment