Sunday, April 2, 2017

USINGIZI WA ROHO PART 1

Asalaam Aleiykum

Kuna Mambo Mwanaadamu yanatokezea unashindwa kujiuliza kwanini inakua hivi, mfano kwanini unapopigiwa honi kwa ghafla, au ukishtuliwa usingizini una hamaki?, umeshapata kujiuliza swali hili, au ndio umeshikiwa Dini yako na watu wengine hata mambo yako Mwenyewe lazima yasimamiwe na watu wengine.
Mimi kazi yangu kukuamsha usingizini unipende, au usinipende hilo sio tatizo langu, na kila ukinichukia najua kweli sasa unaanza kuamka, maradhi haya ya usingizi mzito yanaanza kupona.
Naijua sababu kubwa Mtu anakukera, Wewe unataka ubembelezwe yeye anakuja na kigoma cha daku,"Amka Amka" toka usingizini wewe, Kifo Kimekaribia, umeshakula chunvi nyingi, sasa hebu japo kidogo onja na sukari.
Najua unajiuliza kasema nimekula chunvi nyingi kakusudia nini kusema hivi?. Kwa Mimi Chunvi ni yale Matatizo yako, Mateso, Ghadhabu, Visasi, Chuki,Maudhi,Dhiki,Matamanio, Fikra Mbovu, Viburi na mengi ambayo unayajua, Ama kukuamsha kwangu ni kukwambia upo upande wa pili huku kuna sukari, ili kuipata unatakiwa uamke tu.Ukiamka utajua hazina ya Sukari isokwisha ni yale mazuri yaliyopo upande huo ambayo mara chache unayaonja lakini hujui kuwa hii ni sukari, kuwa nikenda mbele kidogo naweza kupata na (Asali), Lakini umekua Mteja wa Usingizi, una enjoy madhila na tabu za maisha haya na wala hutaki kuamka.
Sasa nimekuja kukuamsha basi kulala tena, inatosha ulivolala wacha kukoroma. Kulala kuko kwa aina mbili, aina ya kwanza ni ile ya (Nature)yako ilotajwa kwenye Quraan aya ya (9 sura ya Naba)
"وَجَعَلۡنَا نَوۡمَكُمۡ سُبَاتً۬ا "
Na tukaufanya usingizi wenu kama kufa.
Usingizi huu ni lazima kila kiumbe aupate, bila ya kulala siku saba  tu utaanza kubadilika akili yako, na zikiendelea zaidi utapoteza akili na kupata madhara makubwa, kwa hiyo usingizi huu wa (Nature)ndio unaokufanya urejee Nyumbani,Na huwezi kurejea Nyumbani lazima upitie njia ya Mauti, ndio maana ukaambiwa(Tukaujaalia usingizi wao kama mauti). Sasa nini faida unayoipata ukenda huko nyumbani,(Ndio maana unasisitizwa uwe na tabia ya kulala mapema)huko unapata afya, unapata nguvu mpya,huko unapata (Vitality and Nourishment)huko ndiko kwenye mapumziko mazuri, huko ndiko unakotibiwa maradhi yako yote(Ndio Maana madaktari wanasisitiza mgonjwa mwacheni alale)mwacheni apumzike, na wao pia wanaomba kwenye nguvu za Miujiza na Rehma za Mollah wako zifanye kazi yake, huo ndio usingizi ambao pale ukiamka unasema najisikia vizuri,niko (Fresh) huo ni usingizi wa aina ya kwanza. Upi usingizi wa aina ya pili?.
endelea part 2

No comments:

Post a Comment