Monday, May 1, 2017

IJUWE RAMADHAN PART 3

Asalaam Aleiykum

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡڪُمُ ٱلصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِڪُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ
(Bakarah 183)
"Enyi Mloamini Mmelazimishwa kufunga(Saumu)kama walivyolazimishwa waliokua kabla yenu ili mpate kumcha Mungu"
Kwanini aya ikaanza na enyi Mloamini melazimishwa, kwa sababu mngeambiwa mmeamrishwa bado mngebakia kama waislam wengine wanaendelea kutenda dhanmbi, wanabakia na kitambulisho tu cha majina, lakini kumbuka hiyo lazima ya hapo ni lazima ya mapenzi, sio lazima ya mtutu wa bunduki kama hufanyi utakufa, ila Mollah wako anataka uonje ladha ya kumtii yeye inakuaje, hali inayo kutokezea ukiwa karibu naye, anakutaka japo mara moja kwa mwaka uka (Hijj)ndani ya nafsi yako ujijue (How bless are you).
Sasa kwanza tuitizame funga yenyewe ina siri gani?, sitaki kwenda kwenye faida zake katika darsa hii nikawa kama nafanya biashara, kwani wengine wanasubiri wasikie funga inaponesha maradhi, ndio wanafunga ili wapate kupona, inafanya hivyo sikatai, lakini ukifunga kwa ajili hiyo utakua umeikosa Taqwa, unatakiwa ufunge kwa ajili ya mapenzi ya Mollah wako ili ukutane na hicho chenye kutenda taqwa.
Nini funga inafanya juu yako, na kwanini nikasema (Hijja)ya kila mwaka, siku zote unafunga hujui mambo haya, sasa kuanzia leo nataka funga yako iwe ya aina nyengine isiwe kama za miaka ya nyuma, ndio maana nikakwambia kwanza (Ijue Ramadhan)halafu ndio utaifunga kwa vizuri, ikisha ndio utaipata hiyo Taqwa.
Kitu cha mwanzo kabisa nataka ukumbuke tu, ndipo utaipata hiyo (Hijja)ya kuhudhuria (Body)Mwili wako, ili upate kujua vipi inakua, vipi unakumbuka, Jambo la kwanza kabisa au saumu yako ya mwanzo unapata jambo la kuwa (Alert)(Awareness) au Dhahir, unapata fahamu kuwa hujala, sasa itabidi ujiulize huyu nani mwenye kujijua sijala, na kuwa nimefunga, ukishagundua hilo litaanza kukupeleka kwenye mambo mengine moja baada ya jengine katika nafsi yako na hiyo ndio (Hijja)yenyewe nilokusudia.
Utaona vipi Akili inavo hangaika na kuhaha kutaka chakula, kwa kuwa (Body)yako yote ni (Intelligence)tupu inatambua kuwa (Boss)leo kagoma kuleta chakula, hakuna huduma kutoka nje, kwa hiyo inaanza kwenda ndani kwenye (Store) na kutoa akiba hapo (Body)inajilisha yenyewe(Cannibal)unajila mwenyewe, na hapo unapata hiyo (separation)baina ya Mwili wako na hicho chenye kutenda Taqwa ukiweza kulijua hilo unakua wewe ni Mwenye kufuzu.
Mara unaona njaa hiyo imepotea , kumbuka huyu mwenye kuona ni nani?, Ikipotea njaa mara unakuja usingizi, na usingizi upo wa aina mbili uko ule wa kulala umezidiwa au ule wa kujizubaisha ambapo Akili sasa imehamaki inakwambia rudi kwenye desturi yetu ya Miezi 11, ya nini unataka kugundua au kufanya jambo la Taqwa, wewe shika simu, au angalia TV, au twende tukajiliwaze senema, hee basi safari hii hata barazani hupiti, Akili inakuvuta kwenye mazoea yako ya kumuasi Mollah wako, inakurudisha katika yale mambo yote unayofanya miezi 11 ilopita, mimi nakwambia safari hii pigana na akili, Yaache mambo yote ya Mwezi wa kula mchana, nenda kinyume na maamrisho yake, vipi utafanya? usije ukashindana na akili, huwezi kushinda, ila nakupa (Trick)mawazo yote yakija (Just watch inside you)ukiweza kuangalia Akili yako mara baada ya sekunde chache wazo la karata, barazani,sokoni, kutizama wanawake au wanaume litatoweka,  kidogo kidogo utaanza kuishinda Akili.
Kawaida unakuwa ni mwenye kushinda vita ya ndani, Njaa pale inapokuja unaipuuza, usingizi unapokuja unaushinda, lakini Ramadhan zote vita vya nje vinakushinda na hilo ndilo lenye kukukosesha hiyo Taqwa, Basi kama ulivoamrishwa na Mollah wako kumbuka Taqwa haitakiwi iwe nusu, inatakiwa (Total)Taqwa ni ncha mbili ndani na nje ndio uweze kuifikia, uweze kuigundua, uweze kuifanya, Kumbuka ndani unaishinda njaa, sex,usingizi, lakini nje mambo yote yanaendelea kama kawaida, haitakiwi hivyo, kuipata Taqwa unatakiwa hiyo (Surrender total)Itakubidi mwaka huu ubadilike, funga yako iwe ya aina nyengine, jiandae na mambo ya nje yote uyaache, kumbuka ni siku chache tu lakini manufaa yake ni ya kudumu, ikiwa unaweza kujizuia Bia na sigara na mirungi, maji, chakula na vyengine vyote  unaweza kuviepuka, basi mwaka huu ongeza mambo ya nje, kimbia mambo ya kipuuzi, iepuke simu, achana na facebook, acha kukimbilia mazungumzo ya kipuuzi,gomea mipira,ichukie Tv,usitizame machafu,usende karibu na mambo machafu, acha kudhulumu, usiseme seme sana, acha uongo, jiepushe na matamanio, acha kuwa muandishi wa habari kuwa kila kitu ushuhudie, acha kukaa kuanza kufikiria mafutari, ukiweza kubakia (Empty) au kufanikiwa kuyashinda mengi katika hayo japo kwa siku tatu za mwanzo, hapo utaanza kupata (Glimpse)ya hiyo Taqwa, utaanza kui (Experience) wewe mwenyewe, nitakua sina haja ya kukuhadithia.
Taqwa itaanza kuzaliwa kwenye Roho yako, Utakua Mwenye(Bliss)umewasili nyumbani, (You are Blessed) Taqwa itakuchukua pale ambapo wanafika Mawalii, wanapofika (Mystic)utafika hapo kwenye kujibiwa duwa, utafika hapo kwenye (Makarama)yote wanapofika wacha Mungu, hutotaka tena Mtu akuombee dua, Hapo ndipo iliposemwa kumi la Mwanzo ni (Rehma)hiyo ndio taqwa ambayo ukiipata wewe ndio utakua shahid wa hilo, kumbuka darsa hii ni kuijua na darsa ijayo ukishakua katika hali ya hiyo Taqwa nini kinatokezea?kwanini nikasema kinatokezea kwa sababu hiyo ndio (Nature)ya Taqwa, na kama haitokezei basi unakaa na njaa, na wakati wa kukaa na njaa sasa ushakwisha unatakiwa ufunge huku umeshiba, na hiyo ndio Taqwa, na kumbuka ukishiba chakula lazima ukigawe, na hilo tutalikuta katika mada ya (Mafundisho ya Taqwa)Tukijaaliwa na Mollah wetu kabla ya kuingia katika mfungo wa Ramadhan.

No comments:

Post a Comment