Asalaam Aleiykum
Kwanini Nikasema kama (Hajj)?.
Kumbuka haya ni maneno yangu, au ufahamu wangu, na nitakuonesha kwa mifano ipi hata nikaita Ramadhan ni kama (Hijja)ya kila mwaka kwa Muumin, Yamekua Mapenzi ya Allah makubwa juu yetu kwa kutuletea Mwezi huu Mtukufu wenye Baraka kila mwaka.
Ili upate kunifahamu vizuri itabidi nikujulishe mambo mawili ambayo ndio msingi wa darsa yetu, Ama jambo la kwanza ni ile desturi ya "Bwana Mtume s.a.w alipokua kila akilizungumza jambo la Taqwa akionesha kifuani kuashiria ndani""Alikua akiashiria kitu kilichomo ndani akisema Taqwa imo ndani, Taqwa imo Ndani", Wengi hawalijui na wanadhani alikua akionesha kifua chake, au kuashiria moyo, lakini kusudio lake ilikua kutufahamisha kuna kitu ndani ya mwili wetu, hicho ndio chenye uwezo wa kutenda Taqwa, mkiweza kukijua, mkifanikiwa kukigundua, basi moja kwa moja unakua Mcha Mungu, na usidhani Ucha Mungu unapatikana bila ya kitu hicho, unaweza kujidanganya, nje ukawa Mcha Mungu, lakini ndani kutwa ukawa unazini, unadhulumu,unafisidi hapo bado hujawa Mcha Mungu, Ucha Mungu lazima uwe na (Control)ya ndani na nje, lakini ukiona bado ndani unateseka basi fanya jitihada, zidisha safari ya (Umrah) ya ndani mpaka ukijue hicho kinachoweza kutenda (Taqwa).
Ama Jambo la Pili nalopenda kukufahamisha ni zile (Ngazi)tatu za kukufanya wewe ufikie huo Ucha Mungu au kuwa Muislam kamili, Wengi katika sisi tumepata baraka(Blessing)za kuzaliwa ndani ya Uislam, tumeinukia kwenye Uislam, kwa hilo tunapaswa kumshukuru Mollah kwa hisan hiyo, kwanini nikasema hisan, kwa sababu wewe hukuchagua uzaliwe na wazazi wa dini gani, kakuchagulia Mollah wako ndio na wewe ukajikuta Muislam, pengine ungezaliwa na wazee wenye dini nyengine usingekua Muislam, ndio maana nikaita (Ihsan).
Sasa jambo la mwanzo katika hizo (step 3)kuwa wengine Uislam kwao unakuja (Automatic)kama kwa kuzaliwa, na wengine wanaingia kwa kupewa (dawa)au mawaidha wakubali kuwa waislam. Sasa Uislam ni ngazi ya kwanza, ni kama kitambulisho, ndio maana unakua Muislam lakini unatenda mambo yote yenye kukatazwa na Mollah wako, huna tafauti na asiyekua Muislam, halafu jambo la pili katika hayo matatu niliyo yataja ni lile la wewe kuwa Muumin, Nini Muumin?.
Ni yule aliyeanza kuzitii Amri, akaanza kuzifata kidogo kidogo, mara anateleza anaanguka, ikisha anainuka na kuendelea na safari ya kujitahidi kuwa Muumin, Halafu jambo la tatu kukutana na (Truth)kufungukiwa na fahamu, kukutana (Face to Face)na yakini ya mambo yalofichwa kwa uwazi.kupata uhakika kwa njia ya (Ilham)Na ukipata au kujua uhakika hapo unakua Mbarikiwa, na wala si kwa njia ya kusoma sana ukakusanya (Information), Ni njia ya ku (Experience)kwenye moyo wako, hapo ndio inatokea hiyo (Surrender),unakua (Total)umewasili kwenye kisiwa cha (Taqwa)sasa wewe unaweza kuvaa taji la (Ucha Mungu).
Hapo ulipo visa vyote vinapotea, huna haja ya chochote, umeshagundua utajiri wa Mwenye enzi Mungu, humtegemei tena Binaadamu mwenzako, unakaa kimya kuangalia Ulimwengu, Raha za hali kama hiyo sio tena za Ulimwengu huu (Full of bliss). Hapo huna tamaa, huna chuki, huna ufisadi, huna hamaki, hutaki maasi, vyote vinatoweka katika nafsi yako, Na hiyo ndio funga ya Ramadhan ambayo na wewe unatakiwa uionje kila mwaka, pengine ukiigusa au kuionja hali kama hiyo unaweza kuamua kudumu nayo, ndio maana nikaita kama (Hijja),nenda kahudhurie uipate kila mwaka. Na hayo ndio mashiko yenye kutufungulia darsa yetu ya leo.
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment