Asalaam Aleiykum
Hapo utakua tayari kuliingia jambo la tatu(3) ambalo ni kumuomba Mollah wako (Pepo yake). Unapotajiwa pepo akili yako mbio inakimbilia kwenye jumba la ghorofa na mto(River)inapita mbele, basi umemaliza. Lakini Jambo unalo ahidiwa na Mwenye enzi Mungu elewa halina mfano, ikiwa haya maisha ya dunia katika huu (Uhai)ulopewa unaupenda hali hii, ukiambiwa sasa wakati wako ushafika wa kurudi Akhera unakua na huzuni kubwa, hutaki kwenda, unapigana kwa kila hali, mara dawa hii mara ile, iteni (doctor)huyu au yule, Sasa hebu fikiria nini habari yetu sisi hiyo Pepo, (Jicho halijawahi kuona, sikio halijapatapo kusikia) ina hali gani Pepo ya Mollah wetu.
Nyinyi Mmeonewa huruma ndio maana hesabu zenu zikazidishwa, kwa sababu wengine wana Maringo wanadhani vijithawabu vyao katika miezi ya kawaida vinaweza kununu pepo. Basi thamani ya hiyo Pepo imetajwa kama unataka kuinunua itazame fadhila iliyomo ndani ya mwezi huu, umeambiwa nini?.
Ukifanya au ukitujia na jambo moja la kheri katika mwezi huu wa Ramadhan malipo yake ni sawa sawa na mambo sabini (70)ya Fardh, Pia unaambiwa "Ewe Mcha Mungu" huu ni mwezi wa subira, Na kwa ajili hiyo ya kujizuia kwako na mambo yote, basi imekua zawadi ya subira yako ni hiyo Pepo.
Nini (Sabr)? Subira ni (Eternity) ni sehemu ambayo haina mwisho, subira haina saa wala dakika, haina usiku wala mchana, haina miezi wala miaka, ndio maana ukiingia ndani ya tendo la subira mara moja linatoweka, yatizame mambo yote mazuri yanakwisha haraka sana, kwa sababu umeonja subira, umeonja mapenzi, umeonja Taqwa, lakini zitizame dhiki unavoziona zinadumu milele, ndio maana ukilala hujui masaa mangapi mpaka uamke, lakini ukiwa macho (Unasema Mwenyewe Funga ya leo kali haimaliziki).
Basi kwa ajili ya Mollah wako umefanya subira na kukubali amri yake, kwa hiyo malipo yako ndio hiyo Pepo.
Hiyo ndio maana ya ukitujia na jema moja tunakulipa mara sabini, kwa sababu hilo moja lako limo ndani ya hiyo (sabr)Subira, Jee unaijua Sabini ya Mwenye enzi Mungu ikoje?. (Wallahi)ungeijua ilivyo basi ungeifata kwa Magoti na unyenyekevu ukawalisha watu japo kokwa ya tende, ukawafutarisha watu japo maji, ukawapa japo maziwa, Nini habari yako Mja wewe ulokushika Ucha Mungu Mwaka huu Ukaamua Kuwafutarisha Masikini Mwezi Mzima malipo yake yatakuaje?.
Enyi Mliopo Arabuni na Ulaya na Kwengineko zikimbilieni Thawabu hizi zitakuja kukusaidieni siku ya kufunga macho ya dunia, siku ambayo utashangaa unatolewa Roho yako na huku mbele unaoneshwa malipo yako kwa ajili tu ya kumfutarisha mwenzio alofunga. Fanyeni bidii kuipata hiyo Taqwa kwa kuwalisha watu futari, Hayo ndio mapenzi ya Mwenye enzi Mungu juu yenu. Anataka na nyie muyapate ndio maana anakuhimizeni na kukuulizeni vile tulokupeni mmevitoa, Angalia kawaida ya Mwanaadamu jee anayo Tabia ya kutoa, hutokuta ila wachache sana, na hiyo ndio dalili ya mapenzi, ukiona huwezi kutoa basi na mapenzi au hiyo Taqwa itakua ngumu sana kuipata.
Mwenye enzi Mungu kakupa uhai hapa duniani na kesho Akhera, Ukiijua Rehma hiyo ndani ya Mwezi huu wa Ramadhan basi utafanya bidii kubwa kuyaendea mapenzi ya Mwenye enzi Mungu.
Utabadilika kuwa Mtu wa aina nyengine, hutomuasi Mollah wako, hutopindukia mipaka uliyowekewa, Ndani ya Mwezi huu Mollah wako kakukumbusha kuwa wewe ni (Special)Kakupa (Gurantee)ya Msamaha kwa ajili ya hiyo (Taqwa)yako, kwa kuwa huu ni Mwezi wake (Special) kakupa hilo jambo la (4) la kukunusuru na adhabu ya Moto wa Jahannam. Hiyo ndio (Taqwa) ndani ya mwezi huu wa Ramadhan.
No comments:
Post a Comment