Monday, May 22, 2017

MAFUNDISHO YA TAQWA PART 1

Asalaam Aleiykum

Nianze kwa kusema kwa anayejua atacheka sana akisikia eti (Taqwa)ina mafundisho, Lakini inabidi tuseme hivyo kwa ajili ya wale wasoijua, Kwa wale wenye kujua wanaelewa Taqwa haina haja ya mafundisho, Kwa sababu hakuna yoyote Mwenye kufundishwa Mapenzi. Lakini huruma ziwafikie wale ambao hawajawahi kupenda, au kufikia daraja hiyo ya Mapenzi ya Taqwa, hawa wanahitaji muongozo, wanataka kujua wakifika kwenye hilo daraja wafanye nini?. wana wasiwasi labda itakuaje, huwezi kuwalaumu kutokana na wasiwasi huo kwa sababu katika hali ya kawaida wanaogopa kupenda, Nini habari yetu sisi wakiingia kwenye Mapenzi ya Mwenye Enzi mungu itakuaje, wengine wanaamua kujiua, wengine wanaihama dunia, wengine wanapoteza akili kwenye mapenzi haya.
Utaona kuna siri kubwa ya kuyakwepa Mapenzi haya kwa njia za kutafuta ulevi wowote ule, wengine wanasema hakuna chochote, lakini ndani ya nafsi kuna shaka inabakia ya kiu cha kutaka kujua  Mapenzi haya ya aina gani?,  jee haya maisha yana mwisho au yanaendelea?, Napenda ukumbuke (Kiu)Ulonayo na dhiki ya maisha haviondoki mpaka uyapate Mapenzi ya Mwenye enzi Mungu. Nataka pia uelewe sio hujayapata, unayo lakini bado huyajui.
Najua tunajiuliza siku zote haya mapenzi yanatokea wapi?. Jawabu itabidi ujitizame Mwenyewe, pale unapokua huna dhiki, huna magonjwa, uko safi utagundua kwamba wewe una vipande vipande vya mapenzi, mara unapenda Mwanamke au Mwanamme, mara unapenda gari, halafu huyo unapenda shamba lako, na mara unapenda watoto wako, Jee ushawahi kujiuliza yanatokea wapi mapenzi haya?, Umeshawahi kwanini unachukia kufa?, Jee huijui kama hiyo ndio (Nature) yako, Quraan inasemaje kuhusu  jambo hili la mapenzi. (Aya ya 14 Al-Imran).
زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ ٱلشَّهَوَٲتِ مِنَ ٱلنِّسَآءِ وَٱلۡبَنِينَ وَٱلۡقَنَـٰطِيرِ ٱلۡمُقَنطَرَةِ مِنَ ٱلذَّهَبِ وَٱلۡفِضَّةِ وَٱلۡخَيۡلِ ٱلۡمُسَوَّمَةِ وَٱلۡأَنۡعَـٰمِ وَٱلۡحَرۡثِ‌ۗ ذَٲلِكَ مَتَـٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا‌ۖ وَٱللَّهُ عِندَهُ ۥ حُسۡنُ ٱلۡمَـَٔابِ 
Watu wametiwa huba ya kupenda Wanawake na watoto na (wingi)mirundi ya dhahabu na fedha, na farasi wanotunzwa vizuri, na wanyama na mashamba, Na hayo ni matumizi ya maisha katika dunia, Na Kwa Mwenye enzi Mungu ndiko kwenye marejeo mazuri.

Sasa ukisha kulijua hilo nakurejesha kwenye aya ya (183)iliyomo ndani ya sura ya (Bakarah) inayosema Melazimishwa kufunga ili mpate kumcha Mungu, Hapo nakuomba uitizame aya kwa undani, usipite juu juu utakua huipati maana yake, na hapo ndipo wengi wetu tunashindwa kufafanua tafauti na kusudio la aya hii. Sasa pata nafasi ya kuijua maana yake halisi, ijue siri iliyopo hapo upate kuitumia kama utakavo ifahamu.
Nakukumbusha kwamba aya imesema ili upate kumcha Mollah wako, au kwa lugha nyengine yapate mapenzi kwa ukamilifu (Higher love)unakumbuka kule ulikua na vipande vipande huku kama utafunga kwa Imani na ukawa (Total)ume (Surrender) ndio unaipata hiyo Taqwa au (Mapenzi ya Mwenye enzi Mungu).
Napenda ukumbuke aya haikutaja ulishe mayatima, wala kutoa sadaka, hukuambiwa ufanye hisan kwa yoyote yule ila umeambiwa upate kumcha Mollah wako(seek the love of your god). Jee unaijua maana ya Kumcha Mungu?, Basi kama huijui tuliza fikra zako ili upate kuijua maana ya kumcha Mungu. Halina maana nyengine neno hili ila kulipa hadhi ya mapenzi, lakini kwa kuwa katika hali ya kawaida hatuyajui mapenzi ni nini, ni bora tuliache pembeni neno hili ili twende kuitafuta maana ndani ya mwezi huu wa Ramadhan.
Tunafundishwa maana halisi ya Mwezi huu wa Ramadhan ni kuufanya ni (Special)kwa ajili ya Mollah wetu, Ni kwa ajili ya kutafuta mapenzi ya Mollah wetu, kugundua utukufu wa yule alotuumba, kuzitafuta Radhi zake, Kuelekeza Fikra, mawazo, maswali yote kwa ajili ya kumjua Mollah wako, kuna msemo unasema (Gonga utafunguliwa), kumuomba atuwezeshe kuyapata mambo manne muhimu yaliyomo ndani ya hiyo Taqwa katika Mwezi huu wa Ramadhan, Mambo yenyewe yepi yaliyomo ndani ya mwezi huu?.
Endelea part 2

No comments:

Post a Comment