Asalaam Aleiykum
Kabla ya kumjua vipi anafanya kwanza lazima uzijue sifa zake za kuwa huyu kweli ni mganga. Ama wale wa kidunia wao wanaweka matangazo na vyeti vyao, na wapi wamesoma na wamesomea nini, sasa huyu wa mambo ya kiroho utamgundua vipi na yeye hana cheti.
Vipi utamjua kama yeye ni Wakala wa Mwenye enzi Mungu, anazo Baraka kutoka kwa Mollah wake?. Jambo la kwanza kukujulisha ni Ucha Mungu wake, jambo la pili si mwenye kutaka sifa, jambo la tatu hana tamaa, hachukui pesa abadan, hata ukimpa hiyo ni hiyari yako, ukimpa kingi ni mafanikio yako ya haraka, na ukimpa kidogo na wewe mahitajio yako yatapatikana kidogo kidogo, huyo ndio mganga wa aina ya kwanza huyu yeye akinyanyua mikono dua yake hairudi, huyo ndio alopewa Baraka zitokazo kwa Mollah wake.
Ama Mganga wa aina ya pili ni yule mwenye kuijua au ku (Penetrate Third Eye) Nini kitakujulisha hiyo (Third Eye) hiyo ni (Sipiritual Eye) iliyopo Baina ya Macho yako mawili kati kati ya kipaji cha uso wako, kama uko Tanzania watizame Wagogo wanapo chanja, wao wanachanja hawajui maana yake wanasema inatibu maradhi, lakini kwa kujua zaidi watizame Mabaniani pale wanapotia alama zao kwenye paji la uso, hapo ndani yake ndio kuna hiyo (Third eye).
Hiyo (Third eye) ni jicho la Roho ambalo linakufanya uone mambo yalofichika katika Ulimwengu huu, lakini huwezi kuona hayo mambo mpaka ufunguliwe hilo jicho na Mtu anaefahamu elimu hizo, au lifunguke kwa Baraka za Mollah wako. Nini kinatokea Jicho likifunguka?, kwanza napenda uelewe vishindo vyake vikubwa, unaweza kudhani unapata wazimu, au kichwa kinangoka, au mfano kama vile unatumbukia kwenye shimo lisilokuwa na mwisho. Likifunguka jicho hilo unaona mambo ya ajabu, huoni tena kwa kawaida, miti unaona vyengine, kila kitu hutokiona kama mwanzo unavo viona, hapo tena kwa uwezo wa kuona mambo utaweza kuwa mtabiri, mtu akija na maradhi yake unaona kama (X-ray). Ndio maana ukenda kwa watu wengine wanakwambia wewe una jinsi kadhaa wa kadhaa, jua huyo anaona mambo (Live).
Hapo ndio unapata hiyo (Power) ya Uganga, unapata nguvu za kufanya mambo, unaweza kutumia kwa njia ya kheri ama ya shari, shauri linakua lako mwenyewe, unapata kuzijua dawa za ajabu, na unaweza kufanya mambo ya ajabu, ukazuia meli isiondoke, ukaharibu gari isiendeshwe,unaweza kudhuru watu, unaweza kuona viumbe vya ajabu ambavyo watu wengine hawavioni, unaweza kubadilisha matukio kutokana na huu uwezo wa (Third eye).huyo ndio Mganga wa aina ya pili.,
Halafu kuna Waganga wa aina ya Tatu, ambao wao wana uganga wa uongo, uganga wa kubahatisha, uganga wa nujum, uganga wa uramali, uganga wa Ramli, uganga wa (Numerology),uganga wa kutizama na kuisoma mikono ya watu. Mambo yao yote ya kubahatisha bahatisha, wakichangaya na miti shamba wanakwambia wao waganga, lakini hawana lolote isipokua mambo ya Uongo. Kwa hiyo namalizia kwa kusisitiza wanoweza kukusaidieni ni huyo wa kwanza na wapili kwa njia za halali na wala hakuna tatizo lolote, na hizo ndio Baraka za uganga mnazo niuliza kutaka kuzijua.
nakushukuru kwa elimu hii
ReplyDelete