Friday, July 14, 2017

BARAKA ZA UGANGA PART 1

Asalaam aleiykum

Moja kwa moja naanza na maswali yenu mengi kuhusu mimi kama mnavo niuliza jee wewe Mganga?.
Jawabu ndio Mimi mganga tena mkubwa ila tatizo langu sitibu mtu, najiganga mwenyewe, na watu wachache wale ninao waona kweli wanahitaji utibabu, tena nafanya bure kwa kuwa mie nimejua bure, lakini ukija na shida zako za mahitaji mimi ni ghali sana sio kunilipa tu bali hata kunipata nikakufanyia huo uganga.
Sasa tuingie kwenye darsa yetu ya baraka za uganga.
Kwanza kabisa kabla ya kukoga kwenye bahari hii ya Uganga nataka nikufahamishe ili upate kujua kuwa Mganga mkubwa wa nafsi na Roho yako ni Mwenyewe aliyoiumba Rabbil-Allahu(Mwenye enzi Mungu). Ukiweza kuwasiliana naye utakua huna haja ya Waganga wadogo wadogo wa Kidunia.
Sasa Mtu wa mwanzo kutujulisha siri hii ya Mganga Mkubwa ni Rafiki wa Mwenye enzi Mungu Nabii Ibrahim a.s aliposema kwenye Quraan sura ya Shuaraa aya ya 80 "وَإِذَا مَرِضۡتُ فَهُوَ يَشۡفِينِ "
"Na ninapoumwa Yeye ndiye anayeniponesha".
mmetaka tuzungumze mambo ya Uganga Uganga sasa wacha tuweke wazi baadhi ya siri za Kiganga ambazo mlikua hamzijui, kwa hiyo kuanzia leo kumbuka ukenda Hospital au ukija kwangu sie sio tunayekuponesha, sisi sote tunataka Idhini ya Mganga Mkuu ambaye ni Mollah wetu.
Na lakushangaza zaidi ambalo watu wengi hawalifahamu au kujiuliza kwanini wakati mwingi inasisitizwa Mgonjwa lazima alale au anapewa dawa ya usingizi au anakua kalala?, hapo kuna siri kubwa inafaa uzamie ili kupata kuijua. Leo tumo ndani ya darsa ya uganga wacha tuendelee na mambo ya kiganga na hakuna Mganga aliyetuonesha fani ya utibabu wa hali ya juu kama Nabii Isa a.s (Jesus).(Quraan Al-Imran- 49)

وَرَسُولاً إِلَىٰ بَنِىٓ إِسۡرَٲٓءِيلَ أَنِّى قَدۡ جِئۡتُكُم بِـَٔايَةٍ۬ مِّن رَّبِّڪُمۡ‌ۖ أَنِّىٓ أَخۡلُقُ لَڪُم مِّنَ ٱلطِّينِ كَهَيۡـٴَـةِِ ٱلطَّيۡرِ فَأَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيۡرَۢا بِإِذۡنِ ٱللَّهِ‌ۖ وَأُبۡرِئُ ٱلۡأَڪۡمَهَ وَٱلۡأَبۡرَصَ وَأُحۡىِ ٱلۡمَوۡتَىٰ بِإِذۡنِ ٱللَّهِ‌ۖ وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأۡكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِى بُيُوتِڪُمۡ‌ۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَةً۬ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ
"Na (Atamfanya) Mtume kwa wana wa Israili(Na kuwaambia) Nimekujieni na hoja (Muujiza) kutoka kwa Mollah wenu, ya kwamba nakuumbieni katika udongo(Natengeneza mfano)kama sura ya ndege kisha nampuliza mara anakua ndege, kwa Idhini ya Mwenye enzi Mungu, Na ninawaponesha Vipofu na Wenye Mabalanga(Ukoma)Na Ninawafufua (baadhi ya )walokufa, kwa Idhini ya Mwenye enzi Mungu, Na Ntakwambieni mtakavyovila na mtakavyoweka akiba katika nyumba zenu, Bila shaka katika hayo imo hoja kwenu ikiwa nyinyi ni watu wa kuamini.
Naam Mambo makubwa usidhani huo ni uchawi, tungetaka mambo ya kichawi tungemtafuta nabii Musa a.s lakini tupo tunachambua mambo ya Kiganga na tuna hadithiwa habari hii na yule Mganga aloletwa na Mollah wetu ili kuja kutupa taarifa na maalumati hayo, basi kwa uchambuzi zaidi endelea part 2.

No comments:

Post a Comment