Asalaam Aleiykum
Dalili mbili za (Mystic) ni Rahisi kuzijua kama wewe mfatiliaji, kwa lugha ya kawaida miezi sita kabla ya Kufa kwako inapatikana harufu kama vile ya mtoto anavoingia kwenye Baleghe yake, hiyo kwa lugha yako ya kawaida, Ama kwa lugha ya Kiwalii hua unaonekana Rangi au kama (Energy) Fulani inaanza kupanda juu mithili ya moshi au nuru isiyokua na taa inatoka katika Mwili wako.
Na dalili ya pili, nisije nikaisema mkaanza maradhi ya kujitizama, ndio maana tunaogopa kusema mengi ili tusikutieni ugonjwa wa wasiwasi. Dalili ya pili ni ile unaposhindwa kutizama ncha ya pua yako, ukiona unaumwa na huwezi kuangalia ncha ya pua yako basi jua safari tayari, furahi anza kujitaarisha, au ukiwa una mgonjwa mwambie atizame pua yake akiwa hawezi basi elewa safari haiko mbali, macho yanaangalia juu, yashakaa kwenye (Position)ya Umauti ndio maana utaona watu wote wakisha kufa mboni za macho zinabiruka na kuangalia Mbinguni. Nakufahamisheni mambo kama haya ili mpate kujiandaa, ndio maana hata mtu akilala ukifumbua mboni zake za macho utazikuta zinaangalia juu.
Japokua Dalili zinaweza kutafautiana baina ya mtu na mtu lakini wanasayansi wamegundua ule wakati wa mwisho wa masaa yalobaki sote tunapita katika njia moja ya kutoka Roho, Wengine wana bahatika kutokupata dalili zozote za umauti, lakini wengi wetu tunapata kujua harakati za vipi Roho inavotoka kama jicho la (Doctor)linavo hadithia Binaadamu anavokufa.
Tembelea link hiyo hapo chini ukasome mambo yanavokua wewe Mwenyewe.
https://mobile.nytimes.com/2017/06/20/well/live/the-symptoms-of-dying.amp.html
Nakutakia usomaji wa kufahamu.
No comments:
Post a Comment