Asalaam Aleiykum
Sasa kwa kuwa hatujijui wewe ni nani?, ina tushinda pia kuelewa lini unaondoka, Lini utavua guo la udongo na ubaki wewe (Pure Soul), siku gani hiyo utakayo kaa pembeni ukashuhudia watu wanakosha Mwili wako ikisha hao wanauchukua kuupeleka makaburini, halafu wanautupa bila hata ya dua.
Ukiishi Maisha ya Kiroho siku hiyo ni Rahisi kwako kuijua, au kusikia hilo tangazo kabla ya miezi sita kufika, leo hapa nitakupa dalili mbili za (Mystic)Mawalii wengi ambao wanajua kama karibu kuondoka, ndio maana wengine wanaandika, wengine wanasema, wengine wanataarisha sanda zao kwa kujua safari ishawadia, wewe unaogopa kuzijua kwa sababu ya mali yako, kwa sababu ya majumba yako, sababu mkeo au mumeo hutaki aolewe au kuoa mtu mwengine, au pengine hutaki kuondoka kwa sababu ya watoto wako, ndio maana inakua shida hata kutolewa hiyo roho, umengangania hutaki kuondoka, unabururwa mpaka chini ya vitanda.
Lakini ukiridhia laa hakuna mashaka taratibu unavua guo lako la udongo halafu baada ya siku tatu huyoo unapaa kwenda Barzak bila ya matatizo, lakini wapi ukingangania (Riyal au Pound au Shilingi)zako inakua Mtihani, hata ukipewa dawa za usingizi hazifanyi kazi kwa sababu mbishi, hutaki kuondoka, lakini ukiwa Maridhia umetulia watu wanafanya kazi yao kwa urahisi bila ya vishindo. Sasa leo ntakupeni dalili mbili za upande wa Mawalii ili mzijue ukianza kuziona hizo jitaarishe, halafu nitaelekeza wasemavyo wanasayansi ili tupate kuchungulia inakuaje wakati wakutoka Roho.
Endelea Part 3
No comments:
Post a Comment