Asalaam Aleiykum
Kifo kimetangazwa chako wewe na mimi, sote kuna siku tutakufa japo kwa njia au maradhi tafauti, Kifo hichi kimetangazwa tokea siku ile ulipozaliwa kutoka katika Tumbo la mzee wako, ila nashangaa ndio kimekua adui wetu mkubwa, na ukimwambia Mtu kuwa Kifo ni rafiki yako anasema (Sheikh Baja)huyoo sasa lazima akachinjiwe kinda la Kunguru, pengine Akili zinampungua.
Napenda uelewe sote tutakufa itakapofika wakati wetu, Na wakati wenyewe haupo mbali unatunyemelea kidogo kidogo.
Sasa vipi Kifo hichi kinatangazwa?.
Kwanza kabisa unatakiwa ukumbuke vitu viwili hivi kuzaliwa na kufa ni Mtu na ndugu yake, kila kitu kimezungukwa na umauti, Mwenye enzi Mungu kasema kwenye Quraan tumeujaalia usingizi kama kufa, sasa jitizame wewe jee hujalala, vipi utajiangalia kama umelala jaribu kukumbuka jina lako japo kwa dakika moja ukiweza kukumbuka basi wewe umacho, lakini ukisahau tu unakua ushakwenda kwenye ndoto kama vile ulo lala usingizi wa kitandani, tafauti yake usingizi huu unaota uko macho,Unaamka siku ya kufa, hapo tena hakuna usingizi, hakuna kusahau, kila kitu kinakua (Original), unashuhudia Maisha upande wa kushoto yanakutoka, Unasikia watu kwa mbali wanapanga mazishi yako, vipi wataufukia mwili wako, wanasema huyu haji juu tena, Upande wako wa kulia Mauti yanatokea (Live) unaona (energy)hiyo inaondoka kwa (Speed)mbona si hisi miguu yangu, mbona moyo unapiga taratibu, macho mbona yanapoteza nuru na hivi na vile, kumbuka wewe unaendelea kuwa (Hai) Roho ulonayo haifi, ukiligundua hilo ndio utaona kumbe nimezungukwa na mauti kila saa na dakika, na hiyo ndio maana ya uhai na mauti mtu na ndugu yake, unaona vipi vinyama miti vidudu vinavopita na kufa katika ulimwengu huu, Na wewe ukizaliwa unapita wakati wa kukua mpaka kipindi maalum ambacho kukua huko kuna (Stop), Hapo tena unapita katika kipindi kifupi cha subira ambapo hamna chochote chenye kutokezea isipokua (Unachapa raha za Ujana)wakati huo wote (Kifo) kinatokea lakini kidogo kidogo pasi na wewe kujua. Halafu unafika wakati wa kulisikia tangazo wengine wanasema Tangazo hili linaanza unapogonga miaka 40 na wengine wanasema 50, Lakini kwa ujumla tangazo hili lina sauti ya ukimya, hii pale ulipokua mzima hujui kumbe unakufa ndani kwa ndani, na sauti ya wazi pale maradhi yanapowasili na kukupa taarifa sasa jiandae, karibu utaondoka, dongo lishachoka linataka likafukiwe, haliwezi kukubeba tena, sasa ukiamua kusikia au kutokusia hilo ni shauri yako.
Unapofika Umri huo nilotaja Rafiki huyu tunaye mtaja kwa jina la kifo anaanza kujitokeza wazi wazi kwa njia ya Maradhi, hapo ndio sote tunajijua kumbe tutakufa iwe kwa ugonjwa wa Sukari au Cancer, iwe Ugonjwa wa Moyo au Ukimwi, Iwe Malaria au Homa ya Maini na Maradhi mengi tunayoyajua na tusoyajua, Na kifo hichi kinatokea Mpaka kwenye Akili zetu kitu ambacho ndio kwanza tunapata nafasi ya kugundua, kwa ufupi Kifo kimetuzunguka kila upande, huwezi kuepuka, Kifo ni Rafiki yetu na sote tumeshaanza kufa toka zamani, Napenda uelewe kufa ni fadhila kubwa kutoka kwa Mollah wako, kwa sababu hebu jiangalie unakuaje ukiumwa bila ya kupata nafuu hiyo inakua (Quality)gani ya maisha, kwa hiyo ukifikia Umri wa kuondoka usinganganie hebu nenda kwa salama nyumbani kama ulivoambiwa. "Ewe Nafsi Mwenye Matumaini Rejea ukiwa umeridhika na Mollah wako karidhika na Wewe".
Sasa nini kino tufanya tusahau ni hizi akili zetu, na hilo ni jambo zuri kwani ingekua tunamkumbuka rafiki huyu hakuna yoyote angeweza kuishi. Sasa kwanini tunaogopa (Death)Kifo. Tunaogopa Kifo kwa sababu hatujui nini kitatokea baada ya kufa kwetu, na hilo ni jambo linalo chezea akili zetu (What Happen)?.Iman zetu zote zina simama hapo, Tunaishi kwa Ahadi lakini hata hiyo Ahadi tunaitilia shaka, Kwanini inakua hivyo? itabidi ujiulize swali hili siku zote unaumwa maradhi unayo, wakati wowote unaweza kufa, wenzako wengi washatangulia sasa kinachokupa khofu khassa ni kitu gani. Ntakufanyia wepesi wa jawabu kwa kukwambia khofu yote ipo kwenye kutolewa roho, kwenye huko kurejea, kwa sababu unajijua au ushaona huu Mwili wako ni (Body) ilotokana na Udongo, hilo huna shaka nalo, lakini matatizo makubwa hujijui wewe nani, Na Ukifa unakwenda wapi, na Mwanzo ulitokea wapi?.
Endelea part 2.
No comments:
Post a Comment