Asalaam Aleiykum
Kuipata Siri hii ya Fahamu inatakiwa jambo la kwanza Urudi kwenye Moyo, vipi utarudi kwenye moyo, ukirudi kwenye moyo kwa kutumia akili utakutana na damu tupu, (Pump)inasukuma damu mambo yamekwisha, sasa vipi utarejea kwenye Moyo?.
Hakuna njia nyengine isipokua ukahudhurie aya ya (28)sura ya Rad ikupe habari ni vipi inakua.
ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَتَطۡمَٮِٕنُّ قُلُوبُهُم بِذِكۡرِ ٱللَّهِۗ أَلَا بِذِڪۡرِ ٱللَّهِ تَطۡمَٮِٕنُّ ٱلۡقُلُوبُ
(Na) wale waloamini na zikatulia nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenye enzi mungu.Sikilizeni Kwa Kumkumbuka Mwenye enzi Mungu nyoyo hutulia.
Aya hiyo ni kama mbegu ukiipanda katika moyo wako basi ina faida kubwa kabisa, Mwanzo aya inataja kuamini, kwanini kuamini, kwa sababu Imani inatokana na kuambiwa, na kuambiwa ni kama kuoneshwa njia, usibaki njiani sasa unatakiwa uende, uende wapi, nenda moyoni kwa kufanya nini? kumkumbuka Mollah wako, "Hapa itabidi nifafanue"kuhusu kumkumbuka, sio kufanya ile dhikr ya kutoa sauti (Allahua Allahua)Kumkumbuka ni kuchagua katika vile alivyoumba Mwenye enzi Mungu halafu ukaanza kuzingatia uwezo wa Mwenye enzi Mungu bila ya kutumia Akili, Ni kazi lakini inawezekana, kwa sababu ukiangalia mpira unaweza unakuwepo katika (Centre)yako, ukiwepo senema hutumii Akili, Ukizungumza pia hutumii Akili, unatoa (Direct)unakuwepo kwenye Fahamu kwa hiyo hicho ndio kinachotakiwa kifanyike kila wakati, na wakati mwengine unapotizama jambo uwepo kwenye fahamu, Akili isiingie kati, ukitizama mti akili isiingie, ukiangalia Ua akili isiingie, kidogo kidogo ukiweza kufanya hivyo una (Polish your Heart)Mpaka ukisafika Moyo unatulia, kutulia kwake tena inakua huna (SplitMind)nani anakwenda motoni, nani haingii peponi, sala yako inakubalika haikubaliki hushughuliki kabisa na mambo ambayo hayako kwenye uwezo wako, hapo tena unakua umetulia unaanza kupata (Siri ya Fahamu)mambo mengi yanafunguliwa kwako, ita upendavyo (Hekima) au Makarama, Khofu zote zinaondoka, Sala zako zinakua tafauti, mazungumzo yako yanakua ya aina nyengine kutokana na kuishi kwako kwenye Fahamu.
Watu watakushangaa wakikukuta wanaona kuna kitu kimekutokezea lakini hawajui kitu gani, maisha yako yanakua na furaha tupu, ushaondoka kwenye Akili unaishi moyoni, Mtu akikusema, akikutukana unacheka tu, kwa sababu huna tena ile desturi ya Akili ya kureje rejea mambo, na ghadhabu, hamaki, Moyo umetulia unaishi kwenye siri ya mambo, lakini shuruti lake lazima (Uache kutumia Akili)uwe unaishi kwenye Fahamu ambayo ina (Control)akili, kumbuka jambo lolote unalotaka kulifanya ukiwa umetulia mwanzo linatokea kwenye Fahamu, halafu ndio linatumwa kwenye Akili, lakini kwa kuwa Akili imekutawala kwako wewe linaanza Akilini na kupeleka Amri kwenye Fahamu, ndio maana toba hazikwishi, Akili inailaza Fahamu, ndio utasikia anajitoa Fahamu kwa mazungumzo, kwa Ulevi na vyengine mnavyo vifahamu, zote hizo ni mbinu za kuilaza fahamu, lakini ukitumia njia za kufatilia kwa uwezo wake Muumba basi utafikia pahala utakua wewe ndio (Master)wa Akili yako.
Kumbuka Udogoni kwanini ulikua na Furaha? kwa sababu ulikua hujajaza (Book)lako la Akili ndio maana ulikua uki(Enjoy), basi uwezo wa kurejea tena unao, ndio maana utaona tuna uwezo wa kukumbuka raha za utotoni, pale tunakua tumerudi kwenye Fahamu, ndio kila mtu utoto wake anaeleza furaha alokua nayo, umemsikia mtu mzima akakwambia ana furaha(Stress) tupu kwa sababu ya Maisha ya Akili, utaona tuna uwezo wa kukumbuka mpaka umri wa miaka minne baadhi ya mambo, lakini ukipata fahamu yako unaweza kurudi nyuma ukakumbuka mpaka mtoto wa mwaka nini kilitokea, kwa sababu Roho yako sio Mtoto wala mtu mzima ni yenye kuishi milele na yenye kujua yote yenye kutokea katika maisha yako ya Uhai na mauti, itafute siri ya Fahamu uone uzuri wa maisha.
No comments:
Post a Comment