Sunday, September 24, 2017

SIRI YA FAHAMU PART 2

Asalaam Aleiykum

Hilo ndio kusudio la darsa yetu ya leo ili kukufanya kwa mara ya mwanzo uipate (Control)ya maisha yako, Kwa sababu muda huu wote (Control)Yote iko katika Maandiko(Akili). Akili imekutia uvivu, hutaki kujijua weye nani na hapa Ulimwenguni unafanya nini, Umri wote huu unaishi kwa kuitegemea Akili na imekuweka kwenye (Automatic Mode). Umefika wakati ukabidhiwe (Gear) uwe wewe Mwenyewe una (Control)Maisha yako.
Mwenye Enzi Mungu hakutunyima Elimu, Katwambia katika sura ya (Qalam)kwa kuapia  Akili na kusema Naiapia Akili na kwa yaandikayo Akili hiyo, Na Wala haikua Neema hiyo kuwa wendaazimu, Akili yako kila siku inaandika na kwa kuwa unaituma sana sasa imejaa na ishachoka kwa hiyo imeweka desturi ya ku(Repeat)inarejea mambo hayo kwa hayo, mara chache unatumia nyenzo yako nyengine ulonayo ambayo ni hiyo Fahamu, au ita Roho, au ita (Consciousness)upendavyo wewe, ila ninacho kujulisha kuwa nyenzo hii unaitumia mara chache sana ima inapotokea mshituko au unapojifundisha jambo, na inawezekana umeitumia mara ya mwisho ulivokua mdogo, Nakuuliza jee umeshawahi kurudi tena pahala hapo kwenye (Centre)yako, najua unarudi mara kwa mara lakini hujijui.
Kabla ya kuendelea mbele wacha nifahamishe vizuri kusudio la neno (Fahamu) au (concsiousness). Mwenye Enzi Mungu Kaumba Mauti na Maisha katikati ya viwili hivi kuna hicho chenye kuishi enzi ya milele kiitwacho (Roho)au (Life)ambayo inaishi hiyo Fahamu.
Ndio maana utaona Fahamu ina (Capacity)yake, nisiseme hivi ukadhani Fahamu ndio hiyo Roho, Kwa sababu kumbuka unatokwa na Fahamu lakini roho unayo, Na hiyo Fahamu inaishi ndani ya Roho, kwa hiyo ndani ya hiyo fahamu kuna Muujiza wake wa aina mbili, unaweza kuipata Fahamu ndani ya Maisha au kwenye Mauti, ukawa huku unakufa na unajiona unavomalizika, Sasa ikiwa si mvivu unaweza hapa hapa ulimwenguni ukaishi katika hiyo fahamu ambayo itakufungulia mambo mengi, nisiseme fahamu ukaanza kudhani ni Akili, Fahamu ni (Sipritual Phenomenon) na Akili ni (Biological Process) Sasa vipi utaipata siri hii ili uwache kuishi kwenye Akili.
Endelea part 3


No comments:

Post a Comment