Sunday, September 24, 2017

SIRI YA FAHAMU PART 1

Asalaam Aleiykum

Nakupeleka kwenye Safari ya kuondosha matatizo yako, Safari ambayo kama utajitahidi ukaienda mpaka ukafika basi utakua umezaliwa tena (Born again), faida yake ni kubwa sana kwako, Safari itakayo kufanya uondokane na kiza cha tegemezi ya jamii, waganga, madaktari, maprofesa, Masheikh na kila Mwenye (Control) ya Maisha yako, wote hao utawaweka kando utakapo fika safari yako katika mji wako wa Fahamu.
Huwezi kwenda kwenye mji huu wa fahamu lazima upitie kwenye Moyo, nikisema moyo watu wengine wanafahamu labda ufanyiwe operesheni, Kutokana na ile fahamu ya moyo ni kipande cha nyama, ndio ni kipande cha nyama lakini kina siri nyengine kimeificha ya (sipiritual)tunajua (Biological)ni (Pump)ya kusukuma damu, na vile vile tunaelewa kuwa damu ndio ina (Supply) kile chombo muhimu cha uhai wetu (Oxygen) lakini hatufahamu siri yake ya upande wa pili kuna nini, kulijua hilo ndio tunaingia katika darsa yetu ya leo (Siri ya Fahamu) ili upate kujua japo kwa uchache nini kinatokezea ukirudi kwenye fahamu.
Kumbuka hujawahi kurudi kwenye fahamu toka ulipotoka, na hilo ndio tatizo letu wengi, nakupa wasia jitahidi sana kabla ya kuondoka Ulimwengu huu urudi kwenye Fahamu yako, nikisema Fahamu nakusudia (Your real self). Ulipokua Mtoto ulikua na Fahamu lakini hukuwa na Akili, ulipokua mtu mzima umejaa Akili lakini umesahau Fahamu. Nimesema umesahau kwa sababu unayo ndio (original) yako, itafute urudi kama mwanzo, itafute urudi (pure) Vipi utaitafuta .
Endelea part 2

No comments:

Post a Comment