Sunday, October 15, 2017

MWISHO WA UHAI PART 3

Asalaam aleiykum

Ukitaka kujua yanakwenda wapi itabidi ujitose kwenye sheria mbili za Ulimengu huu ya kwanza ile ya (Gravitation) na ya pili ile ya (Levitation),Mwanzo ilikua maji hayo yanashuka chini kwa kasi, na sasa yamesita lazima uchunguze nini kimetokea, jee yaweza kuwa ndio (Levitation) kupanda juu kumeanza kufanya kazi, na sio kila mtu anapata zawadi hiyo ya (Levitation)wengine maji yanabakia hapo hapo kiunoni kwenye chem chem mpaka yana haribika,lakini kama umeipata hiyo hali ya (Levitation) utaijua pale inapozaliwa hekima juu yako, ukagundua sasa matamanio yamekatika na mimi nimepewa nafasi ya kugeuka.
Itumie nafasi hii ya (Levitation)kwa kutafuta (Favour) kutoka kwa Mollah wako kuupata Ucha Mungu, utastarehe katika kipindi hichi kilichobaki cha Mwisho wa uhai wako, jikubalishe kuwa mtoto tena, ipate tena ile (Innocent) yako ya Utotoni, ukifanikiwa utaanza kusafisha dhanmbi zako, sio kwenda kwa waganga na (Doctor)Wamasai kutafuta nguvu, hayo yanakuharibu na kukupeleka kaburini kabla hujatumia nafasi ya mwisho wa uhai wako.
Kumbuka sasa hivi maji yametulia, inofanya zogo ni akili yako kwa ajili ya mambo ya zamani, ukiweza kuipuuza basi ile (System) ya pili ya (Levitation) inaanza kufanya kazi yake kama inavofanya (Brain)yako kwa kula 90% ya (Vitamin) kwenye chakula unacho kula.
Hapo ndio Maji hayo yanaanza kufata (System)mpya ya (Levitation)yanaanza kupanda juu, hayakai palepale na hapo ndio inaanza kuzaliwa au kufunguliwa hiyo (Hekima)kumbuka ulivokua mdogo miaka (14)ilifunguliwa na kwenda chini, Na hivi sasa imefungwa na  ina kwenda Juu. Hapo tena Utulivu unarejea mwanzo ulikua ukitafuta mambo ya dunia, sasa unarejea kutafuta mambo ya Akhera, unaanza kupata khofu hii akhera ipo? nikenda itakuaje, Vipi ntakutana na aliyeniumba, hiyo ndio (Quest)ya Utu uzima, hapo tena unaanza kuhamia Msikitini, na ukilitizama hilo utaliona Wazee wamejaa misikitini na vijana wapo na dunia yao kwenye (Madisco).
Linatokea hilo kwa sisi Vizee kwa sababu tunajua (Mwisho wa Uhai)umekaribia, Ikifika hali kama hiyo sasa unatakiwa uwe na tahadhari kubwa, kwa sababu kuna jambo lengine jipya linakushughulisha ambalo linakujia wakati huu nalo ni la watoto na mali, Unaanza kuilinda mali ili isimalizike, na watoto wanaanza kukutesa huyu hivi yule vile, inapofika hali kama hii Mwenye Enzi Mungu anakukumbusha tena ili uwe makini kwa kukwambia maneno yaliyomo kwenye sura ya (Munafiqoon aya ya 9-11).
"يَـٰٓأَيُّہَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُلۡهِكُمۡ أَمۡوَٲلُكُمۡ وَلَآ أَوۡلَـٰدُڪُمۡ عَن ذِڪۡرِ ٱللَّهِ‌ۚ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٲلِكَ فَأُوْلَـٰٓٮِٕكَ هُمُ ٱلۡخَـٰسِرُونَ" 
"Enyi Mlioamini yasiku sahaulisheni mali yenu wala watoto wenu(Katika) kumkumbuka Mwenye enzi  Mungu, Na wafanyao hayo, hao ndio wenye kuhasirika".
Onyo hili wanapewa wale wenye imani, Mwanzo ilikua starehe ya dunia na sasa imemalizika kuna chengine kinazuka ile Mali ulochuma na watoto wako ndio inakuja kukufisidi mwisho huu wa uhai, Unataka kulinda mali usifilisike, unaendelea kufunga mahesabu, unataka cheo chako kisiteremke, na kufanya hivyo kunakupelekea kumsahau Mollah wako kabisa, Na watoto wanakushughulisha kwa mahitaji yao na tabia zao inakua kwenye moyo wako wewe Mungu hakai kabisa, mambo ya Akhera huyataki kabisa na hiyo ndio hasara yenyewe.

"وَأَنفِقُواْ مِن مَّا رَزَقۡنَـٰكُم مِّن قَبۡلِ أَن يَأۡتِىَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوۡلَآ أَخَّرۡتَنِىٓ إِلَىٰٓ أَجَلٍ۬ قَرِيبٍ۬ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ "
"Na toeni katika yale tuliyokupeni kabla mmoja wenu hayajamfikia mauti, kisha akasema, Mollah wangu hunighairishii muda kidogo,(Ili)Nikatoa sadaka na nikawa miongoni mwa watendao mema".
Ama tendo la kutoa lina cheo kikubwa sana mbele ya Mwenye enzi Mungu, kwanini ikawa hivyo kwa sababu kutoa ni sifa ya Mwenye enzi Mungu, "Amekupa uhai, afya, mapenzi, Akili, Mali,watoto na mengi kadhalika unayoyajua na usiyoyajua"sasa katika mtihani wake alokupa mdogo tu, ni katika hiyo mali yako anakujaribu na kukutizama, kama unamuamini, Wewe Muislam wa kweli, Kipindi cha sala hakikupiti, unataka pepo yake, jee unaweza kutoa, ukiweza kufanya hilo basi pepo haina wasiwasi wako juu yako, lakini shuruti lake utoe uko hai una nguvu zako, sio uko kwenye kitanda unawaambia watoto watoe, Toa sasa hivi una nguvu zako, toa usijali wakakushughulisha watoto watarithi nini, hiyo sio tatizo lako, ila usiwaache wakapata shida, lakini kuwa mstari wa mbele katika kutoa.
Kwani usiwache tena ushakua mgonjwa taabani ndio una wasiwasi wa kufa ukaanza kujitia ucha Mungu unatarajia Mollah wako akupe muda ili upate kuwa katika waja wema.
"وَلَن يُؤَخِّرَ ٱللَّهُ نَفۡسًا إِذَا جَآءَ أَجَلُهَا‌ۚ وَٱللَّهُ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ"
"Lakini Mwenye enzi Mungu Hatakhairisha nafsi yoyote inapokuja ajali yake, Na Mwenye enzi mungu anazo habari za Mnayoyatenda".
Usitake kudanganya unapigana kutokana na kuwa na khofu, hutaki kufa, sasa unataka na huko unakokwenda ukapate Raha, ndio moyoni unajisemesha nikhairishie kufa kwangu nikafanye mema, lakini inapofika mwisho wa uhai hakuna, msamaha kila mmoja wetu anakwenda, na Mwenye enzi mungu anajua yote mnayoyatenda. Kwa hiyo kabla Uhai haujamalizika zitoe mali zako, katake msamaha kwa makosa yako,zidisha kumkumbuka Mollah wako, tena mapenzi ya Mollah wako yatakushukia katika huu Mwisho wa uhai wako.

No comments:

Post a Comment