Asalaam Aleiykum
Zimekujia taarifa kama hivi karibuni utanyanganywa zawadi yako ulopewa, Hakuna zawadi njema ulopewa kama hii ya Uhai, ila ina masharti kuwa ni lazima baada ya muda ichukuliwe, Na kabla ya kuchukuliwa zawadi hii unaletewa dalili ili upate kujiandaa kuishi bila ya zawadi hiyo.
Umeshawahi kukaa na kuzichunguza dalili hizo ili upate kujua nini cha kufanya. Basi ikiwa bado hujafanya, nakupa nafasi usafiri na mimi ili kuzishuhudia dalili hizo na kuweza kuzifanyia kazi kwa dhumuni la kupewa tena zawadi hiyo ya uhai kwa mara ya pili.
Uhai utakaopewa kwa mara ya pili una mambo mawili Ima Furaha na Raha isokatika, Au Shida na Tabu za milele za kuendelea. Bado unayo nafasi ya Kubadilika, kwanini nikasema kubadilika nisiseme kugeuka, kugeuka ndio kawaida yako kama kinyonga, Mfano na wewe Mwenyewe jitizame unavo geuka Ukiwa na Mkeo Umehamaki, mara akiingia Rafiki unacheka, Mara umekua Sheikh mara unaasi, Mara hichi haramu, mara kile halali, wakati wowote unageuka, lakini mfano mmoja tu wa kubadilika utakutosha nao ni Kama vile (Butterflies)anavobadilik kutoka kwenye (Caterpiller)na kuwa Kipepeo.
Dalili gani zitakufanya ugeuke kabla ya mwisho wa uhai wako?. Mwenye Enzi Mungu simwenye kumdhulumu Mja wake katoa nafasi mpaka dakika za karibu ya Mwisho nafasi hiyo ipo, Lakini kwa Mwenye kutaka kuitumia, ziko dalili hizi kwenye Quraan lakini kwa Mwenye kusoma kwa Njia ya (Fahamu) ikiwa umesoma (Siri ya Fahamu)utajua nimekusudia nini.
Kwenye Quraan yamesemwa maneno yaloficha Hekima ndani yake, wakati ule ulipokua kijana na jeuri zako, mbishi husikilizi mtu uliambiwa maneno haya yaliyomo kwenye sura ya Tariq aya ya (5-6-7)."فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَـٰنُ مِمَّ خُلِقَ"
"Hebu ajitizame mtu, ameumbwa kwa kitu gani" Binaadamu umeumbwa kwa mali ghafi ya maji ya uhai, maji haya ni (Very Powerful)ulipoambiwa yatizame ili ujue uwezo wa maji hayo ambayo ukiyatoa yanaweza kutengeneza kiumbe kama wewe.
"خُلِقَ مِن مَّآءٍ۬ دَافِقٍ۬ "
"Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa" Kutokana na Dalili hiyo kinochupa chochote kinatoka juu na kwenda kutua chini, na hiyo ndio (Sex)lau ungekua unaweza kuzuia yasichupe maji hayo basi Miujiza mikubwa ingetokea juu yako, ndio maana (Watawa na Makasisi wanajificha) ili kuzuia (Gravitation)hii isitokee, kwa sababu kama haitokei (Gravitation)lazima Sheria ya maumbile ya mrengo wa pili wa (Levitation)ichukue nafasi yake, na hapo ndio yanatokea hayo (Mabadiliko)Rehma, Miujiza ita utakavyo.
Lakini maji haya (Nature)yake lazima yachupe yakitokea.
"يَخۡرُجُ مِنۢ بَيۡنِ ٱلصُّلۡبِ وَٱلتَّرَآٮِٕبِ"
"Yatokayo katikati ya mifupa ya mgongo na Kifua"
Wewe hujapata au hujui kuyasikiza inakuaje yakitokea huko hali yake au Raha zake zinakua vipi, kwa sababu ya kushughulika kwako na akili ziko kwengine unashituka sekunde za mwisho, maskini hasara yako, mpaka unaondoka kwenye Ulimwengu huu hujapata kujua inakuaje ladha ya maji haya yakianza kuondoka kifuani au mgongoni hali inakuaje.(Hapa siko kwenye darsa ya mambo hayo ila nagusia na kupita njia tu). Nafahamisha kuwa zipo raha zaidi ukiwa una weledi wa mambo.
Wacha kutoa macho endelea part 2.
No comments:
Post a Comment