Sunday, October 15, 2017

MWISHO WA UHAI PART 2

Asalaam Aleiykum

Siri ya hayo maji tuliyoitaja kwenye part 1 inatokezea hata wakati wa kulala au wa kufa kwako, nyakati nyengine lazima maji hayo yamiminike au yashuke ndio upate usingizi. Hiyo ni sehemu ya kwanza ya dalili za uhai ambazo zinakufanya huwezi kujizuia, maji lazima yatoke, fujo tupu mtaani watu wanachunga watoto wakiume na kike, ile isitokee fujo mitaani, mwanamke kafungiwa na wanaume wanaranda kama simba anatafuta swala, watu wanakwiba, wanadhulumu ,wanagombana yote sababu ya maji haya yanochupa kwa kasi.
Hiyo ni dalili ya kwanza ya Uhai, ikisha kuna dalili ya pili ya mwisho wa uhai. Soma taratibu kwa uangalifu mkubwa ili upate kufahamu kusudio ya darsa hii ili upate kubadilika, kumbuka sio kugeuka. Aya gani inayo tukumbusha Mwisho wa Uhai?
Sura ya Yaasin aya ya (68)
"وَمَن نُّعَمِّرۡهُ نُنَڪِّسۡهُ فِى ٱلۡخَلۡقِ‌ۖ أَفَلَا يَعۡقِلُونَ"
"Na tunayempa Umri tunamrejesha nyuma katika umbo(Lake)(Anakuwa kama mtoto)basi jee, hawayatii Akilini(Mafunzo haya).
Hapo kuna siri nzito ya kujiandaa na mwisho wa Uhai, katika aya hiyo kumetajwa umbo na Akili, Umbo linaondoshewa nguvu lina rudi kama ulivokua mtoto, Baba akiweza kukupiga, ulipokua mkubwa una nyanyua vyuma huoni kaacha kukupiga, na sasa hivi wewe kizee, kijana wakati wowote anaweza kukunasa vibao, Umbo linarejeshwa kama mtoto, unaona mwenyewe magoti hayafanyi kazi uzuri, miguu huwezi kukimbia, moyo unakunyima pumzi, macho na masikio haviwezi kutenda kazi kama zamani, meno yashapungua, sasa ushaanza kukaa ndani kipindi kirefu, habari za kutamani zimeshatangulia na wakati, mambo huyawezi tena, sasa kama huzijui dalili hizi ndio unaanza kukimbilia madawa ya kila aina ujirejeshe ujanani, ndio mnaambiwa hamyatii Akilini?.Kuyatia Akilini maana yake rudi kwenye (Siri ya Fahamu).
Lakini ilipotajwa akili ni kwa Tafsiri yetu ya kiswahili, ama tafsiri ilo karibu zaidi ni ile ya kizungu inayosema (Sense), lakini Tafsiri ilotimia ni kurudi kwenye Fahamu. Vipi kurudi kwenye Fahamu ni wewe kujitenga na (Body)ukajua sasa mwili umekwisha kazi yake, na sasa nimepewa nafasi niangalie upande wa pili huu ulonileta hapa ulimwenguni,(Kumbuka wewe ni Body na spirit) Kumbuka uliletwa kipindi cha mwanzo ulikua mtoto na sasa hivi unarejeshwa kwenye udhaifu uleule wa mtoto lakini ukiwa na kitu adhimu kabisa cha kujijua kuwa ulipita katika njia tatu hizi, ile ya kwanza ulikua hujijui, ukapita ya ujanani ukawa na desturi ya kutokujali au kusahau kwa njia ya ulevi wa kila aina, mara (gossip)mpira,tv, mambo chungu nzima, na sasa umeingia kwenye uzee ukiwa na fahamu yako nzuri umeshapata kujiuliza jee maji haya sasa yanakwenda wapi?.
Endelea part 3

No comments:

Post a Comment