Friday, July 14, 2017

BARAKA ZA UGANGA PART 2

Asalaam Aleiykum

Nabii Isa a.s kaja na mambo  manne(4) Jambo la kwanza(1) kumtengeneza ndege kwa udongo ikisha akampuliza ndege huyo akaruka, kumbuka huo si uchawi kama vile (Magician)wanavo kutolea njiwa kwenye kofia. Halafu jambo la pili(2)Anaponesha Vipofu na wenye Ukoma. Jambo la tatu (3) Akawafufua baadhi ya walokufa. Na hilo la Nne (4)Ntakwambieni mtakavyokula na mtakavyo weka Akiba.
Hapo kuna mambo yanafaa kuzingatiwa wakati ukiendelea na darsa hii, katika hayo mambo manne tumefanikiwa kuyapata mawili tu nayo ni namba (2) na Namba (4), Nitayataja haya mawili tukiwa tunaendelea na darsa hii. Napenda Uelewe Uganga umegawika mapande mawili yenye sehemu mbili, Kama alivotuonesha Nabii Isa a.s hapo juu kuwa Uganga una sehemu ya (Body)yaani(Physical) hii unatibu kwa kutumia dawa za kienyeji na za kisasa na Una sehemu ya Roho nayo ni hiyo (Spiritual) hiyo tiba yake ni ya maombi na mambo mengine ya (Mystical), Wenzetu wa (Western)wamefanya jitihada kwenye utafiti wa (Physical)mpaka wamefanikiwa kuponesha maradhi mengi yakiwemo hayo ya ukoma na mpaka sasa wanajitahidi katika fani ya macho ili kuponesha upofu.
Na upande wa pili wa (Eastern)hapo zamani walikua wako (advance)katika mambo ya utibabu wa Kiroho na Kimwili lakini yalotokezea katika (History)ndio yalofanya mpaka leo hatujaendelea katika fani zote mbili isipokua kwa watu wachache sana walo bahatika au kubarikiwa.
Sasa nini Uganga?.
Kwa Mfano wa kwanza Uganga ni Baraka (Blessing)za Mollah wako unazopewa kuwatibu viumbe wenzio kama alivopewa Nabii Isa a.s, lakini Nabii Isa yeye alikua Mtume, na Uganga ni kama wakala, Ima uwe wa kusomea au wa kushushiwa na Mollah wako. Wakala huyo au Mganga ukenda kwake na shida zako au dhiki yako, au Maradhi yanayokusumbua basi atafanya elimu aliyojaaliwa na wewe kupona au kufanikiwa, au dhiki kukuondoka kwa njia usizozijua.
vipi anafanya endelea part 3.


No comments:

Post a Comment