Monday, May 22, 2017

MAFUNDISHO YA TAQWA PART 2

Asalaam Aleiykum

Mambo hayo Manne yaliyomo ndani ya hiyo Taqwa ndio yatakusaidia kuyapata mapenzi ya Mwenye enzi Mungu, Na ukipata Mapenzi ya Allah hakika wewe umefanikiwa katika mafanikio yasio na mfano. Umo ndani ya ustaadh wa kulea Roho, jambo la mwanzo(1) kabisa ambalo ndio muhimu lenye kukutia au kukuletea hayo mapenzi ni hiyo "Shahada yako" Ya kumshuhudia Mollah wako ni Mmoja wala hana mshirika, Shahada hii daima unaitamka mdomoni(Lip sevice) inakua si lolote si chochote juu yako.
Sasa umo ndani ya Ustaadh wa kulea Roho na wewe unayataka mapenzi ya Mollah wako inabidi uende (Deep)ndio maana ya Ramadhan. Utakapoulizwa una shuhudia nini? ujue cha kujibu, usiwe unatoa macho huna cha kusema, sasa twende mimi na wewe tukatafute jawabu, vipi utalijibu swali hili ni lazima lihusiane na Roho yako na sio ulimi, vipi utaipata Shahada anza japo na Miti, anza kutafakari(Kwani maneno haya si yamesemwa ndani ya sura ya Ghashiyah 17-20)"Hawatazami jinsi ngamia walivoumbwa""Na Mbingu jinsi zilivyo inuliwa""Na Milima ilivyo thubutishwa""Na Ardhi Jinsi ilivyotandazwa", basi kama hivyo vitakua mbali ndio nimeanza na miti, tafakari kwa kujua kumbe hii miti inavuta pumzi kama ninavo vuta mimi, mimi natoa (Carbon dioxide) miti inaivuta ndani na kunitolea mimi (Oxygen)na mimi huyo navuta pumzi.
Pata kujua kwanini ukiona Rangi za kijani unajisikia (Fresh), jishughulishe uelewe kwanini kila ukenda Baharini unajisikia furaha, pata fahamu Jua lina mahusiano gani na mimi, Angalia wanyama mbona wana (System)kama mimi?, wanalala, wanakula, na ukifika muda wao wanakufa.
Fikiria pia kilichomo kwenye majani, na kwenye ardhi, na katika nyota pia kimo katika nafsi yangu, ukikaa ukafikiria japo muandamo wa mwezi na siku zake 28 basi kuna kitu ndani ya moyo wako kitakujulisha nini maana ya Mungu mmoja, au nini maana ya Shahada na wapi mapenzi yanapotokea, Na itakapotokea hali kama hiyo wewe Mwenyewe utagundua kumbe hii ndio taqwa, na hii ndio hiyo Rehma ninayo ambiwa,  hapo ndio utapata nafasi ya kuliendea jambo la pili (2).
Nini hilo jambo la Pili ?.
Baada ya kuujuwa Uwezo wa Mwenye enzi Mungu na Ufalme wake, hapo tena kwa mapenzi ya hali ya juu unaanza kuomba (Mghfira)ita upendavyo(Kumi la pili)au Msamaha, unaomba msamaha huo kwa mara zisizo na idadi, usije ukadhani samahani yenye kutoka katika hali ya Taqwa ni kama ile yako ya kawaida ilojaa kiburi, unajiona ushaacha madhanbi na uko msikitini, au unafanya mema, Msamaha wa Taqwa ni ule wa (Realization)Msamaha wa kujua kwa yakini kumbe mimi nilokua na mkosea yupo, naye ndiye aliyeniumba akanipa uhai huu, Namuasi yule ambaye katika Ufalme wake kakidhibiti kila kitu pasi kuwa na mshirika, Huyu ndie Mollah wangu anayeniruzuku kila siku hata wakati ule nafanya maasi, Yeye ndie Mwenye kunipa Furaha kila niipatapo dhiki, Ananipa usingizi na Kuniamsha kila siku ya uhai wangu. Basi Mimi Mollah wangu sina cha kuomba mbele yako, na wala sistahiki chengine chochote isipokua Faraja ya Msamaha wako, na hakuna Msamaha utakao nipa mimi ila niyapate mapenzi yako ndani ya Mwezi huu wa na daima katika uhai wangu.
endelea part 3.

No comments:

Post a Comment