Monday, May 1, 2017

IJUWE RAMADHAN PART 1

Asalaam Aleiykum

Mwanzo napenda kufahamisha ili unielewe kwanini darsa hii ikaanza na sentensi (Ijuwe Ramadhan), kumbuka kuna tafauti nyingi ambazo zinatokea katika maisha na wewe bado huzifahamu, mfano kama (Kusikia na Kusikiliza)vitu viwili hivi tafauti lakini kuvifahamu lazima upate muongozo. Kawaida ya kusikia ni ile ya uhuru wa masikio kusikia kila kitu, Lakini kusikiliza inatakiwa umuhimu wa (Roho)yako ihudhurie pasi na kushughulishwa na chochote ili kukipa nafasi ya pekee hicho ambacho (Unaambiwa au kukisikia), kusikiliza unatakiwa usiingize chochote kati yake,kwa maana hiyo hata Akili yako isiingie kati katika hilo tendo la kusikiliza, Isiwe Mtu anakwambia kitu, wewe ndani ya Akili yako unatafisiri vyengine kabisa.
Hali kadhalika juhudi hiyo pia unatakiwa uifanye wakati wa kujifunza jambo, au ukiwa katika harakati za kujua. Kwa wale ambao bado hawajanifahamu wacha nifupishe misemo na kuwatolea mfano rahisi wa kujua, ni kama vile unafundishwa kuogelea ukaambiwa sasa jiregeze, usigombane na maji, peleka mkono huu taratibu mbele, mara huyo ukajiona umeelea, uko juu ya maji hapo inakua ushajua kuogelea na hiyo inaitwa (Experience),na hiyo ndio maana ya kujua.
Sasa vipi imehusiana na kuijua Ramadhan, Kwa sababu siku zote ""(Unasikia)"wanasema Masheikh Funga mwezi umefika, Na wewe huyo unaamua kukaa na njaa,Kwanini nikasema kukaa na njaa?, kwa sababu huipati Taqwa, pengine miaka yote hali kama hiyo inakukuta, sio makosa kwa sababu pengine ulikua hujui, lakini ukishamaliza kuisoma darsa hii ukaendelea kama ulivokua unafunga mwanzo, hapo utakua unatenda makosa kwa sababu umeshajua ila wewe sasa hutaki.
Nakuchukua katika (Deep sea) ili funga yako mwaka huu iwe vyengine kabisa, ili upate kujua kusudio la Mwezi huu na wewe ufunge kama mawalii, ufunge kama (Mystic). Siku zote nasema kama utaona mafunzo yangu (batil)huyafahamu, sio kama alivosema (Sheikh wako)basi niachie mwenyewe, mie ndio dhamana wa hili somo, na wewe baki na mwenendo wako, huna haja yakuchuma dhanmbi au kunitupia maneno yasofaa.
Kumbuka darsa zangu naziandaa ili nikufanyie (Shock)hakuna kitu kipya ila yale yale yalosemwa nyuma ila mimi nayaleta kwa njia nyengine tu. Kwa hiyo wakati mwengine utaona mbona mambo mepya haya, na hilo ndio kusudio langu, usibakie na mambo ya zamani, pata kujua mambo mepya, Ulimwengu huu una mambo mepya kila siku yanavumbuliwa, Kwanini unaogopa upya?. Naamsha moyo wako , Masheikh wanapiga kigoma cha daku kila mwaka na wewe bado umelala, sasa mimi nakuja na Tarumbeta(Saxphone)ili nipate kukushitua.
Nini Ramadhani?
Ramadhan ni kama ilivyo (Hajj)ila tafauti yake (Hijja)ni mara moja tena kwa mwenye uwezo, lakini Ramadhan ni kila mwaka unatakiwa ukahijji wapi?. Tuliza Akili upate kunifahamu vizuri na hii itakufanya uione Ramadhan kwa muonekano mpya kabisa, na kama darsa hii itafika moyoni mwako itakubadilisha milele kama ilivo nibadilisha mimi.
enedelea part 2

No comments:

Post a Comment