Sunday, April 2, 2017

USINGIZI WA ROHO PART 2

Asalaam Aleiykum

Ama ule wa aina ya pili, Ni ule unaporejea Ulimwenguni baada ya kulala ule wa mwanzo, unaona hautoshi bora uendelee kulala, na hivi ndivo ufanyavo umri wako wote. Vipi unalala, kumbuka kazi yangu ni kukuamsha, wala sikupigii vinada, nataka uamke uangalie ulimwengu kwa njia mpya kabisa, na hii leo ndio itakua uchambuzi wa darsa yetu.
Kwanza kabisa lazima ikumbukwe Kwenye (Quraan kwenye aya ya 9)imetajwa tukaujaalia usingizi kama kufa,Na kwenye hii aya ya (10)ikaendelea kusema "وَجَعَلۡنَا ٱلَّيۡلَ لِبَاسً۬ا "Tukaujaalia Usiku kuwa ni Guo"(Nguo), Usiku huo huwafunika walale uzuri, wapate faida ya usingizi, sasa kama wewe usiku utakukuta umo kwenye vilabu vya starehe, au unacheza bao mpaka saa tisa za alfajiri, au unatizama senema, au uko kwenye taarab, hiyo ni hiyari yako, usiku huo hauji tena. unakua ushapita.Kuanzia leo kumbuka unakosa kitu muhimu sana katika wingi wa zawadi zitokazo kwa Mollah wako.
Ikaendelea aya ya (11)na kusema "وَجَعَلۡنَا ٱلنَّہَارَ مَعَاشً۬ا "Tukaujaalia Mchana(Muangaza)kama kufufuka".Tendo hili pekee linaweza kukuridhisha kuwa Kiama kipo na kweli utafufuliwa.
Unapokaribia huu Muangaza ndio wakati wako wa kurejea kwenye hiyo (Body) Sasa swali la kujiuliza kwani wewe Nani?.Kujijua wewe nani itabidi uhudhurie sura ya (Sajdah mwanzoni mwa aya ya 9)Inasemaje, "ثُمَّ سَوَّٮٰهُ وَنَفَخَ فِيهِ مِن رُّوحِهِ" Kisha akamtengeneza na Akampulizia Roho (Inayotokana na) yeye.(Mpaka inapomalizikia aya).
Napenda uijue thamani yako, Napenda kukufahamisha hazina ulo nayo, Napenda ujijue kuwa wewe ndio hiyo (Mysterious Being)ambayo bado hujijui, wewe sio hiyo (Skeleton)Mifupa ilobeba Nyama, wewe ni (Special, Unique Being)ukichanganywa na hiyo nyama na mifupa ndio unaitwa (Human Being)Wewe ni hiyo Roho ilotokana na Mwenye enzi Mungu, kwa sasa hufanyi jitihada za kujijua kwa kuwa unaendelea na usingizi, na wala hufanyi jitihada ukakutana na hiyo (Laiylatul Qadir)umeshughulika na Dunia wakati upande wa Pili kuna hazina yako isokwisha, huko kuna kila kitu ikiwemo kusafishwa na Kusamehewa dhanmbi zako, Utapata Rehma kubwa kubwa, Ukifanya jitihada na bidii na wewe wakati wowote unaweza kuwa walii, unaweza kuwa (Mystic).
Sasa nini kinacho kufanya uendelee kulala na hutaki kuamka, na ukiamka utapata nini?.
Endelea Part 3 

No comments:

Post a Comment