Wednesday, November 1, 2017

NJIA YA KUMKUMBUKA ALLAH PART 1

Asalaam Aleiykum

Mnaniuliza vipi kumkumbuka Allah mbona sisi inatushinda inakuaje hali hiyo, Mbona hatuwezi wakati tunajitahidi?, Anapouliza Mja swali kama hili ajijue kashafika mlangoni, huyu anataka afunguliwe, sasa anagonga katokea mbali, kapanda milima na  kupita kwenye majangwa mpaka kuwasili kutaka kujua kitu Adhimu kama hicho.
Siku zote wanasikia aya ya (191)sura ya (Al-Imran)inosema:

"ٱلَّذِينَ يَذۡكُرُونَ ٱللَّهَ قِيَـٰمً۬ا وَقُعُودً۬ا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمۡ وَيَتَفَڪَّرُونَ فِى خَلۡقِ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ رَبَّنَا مَا خَلَقۡتَ هَـٰذَا بَـٰطِلاً۬ سُبۡحَـٰنَكَ فَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ"
"Ambao humkumbuka Mwenye Enzi Mungu Wakiwa Wima na Wakikaa na Wakilala, Na Hufikiri Umbo la Mbingu na Ardhi, (Wakasema)Mollah wetu huku viumba hivi bure, Utukufu ni wako, basi tuepushe na adhabu ya Moto".
Kwanza kabisa nataka kufundisha vipi utazama kwenye neno, ukitaka kuzama kwenye neno lazima ujiulize kwanini likawepo hapo, nikisema kuwepo hapo sina maana nyengine ila kutizama mashiko yake, mashiko yanayo onekana hapo ni kutajwa vitu viwili ambavyo wewe huvioni, ndio maana nikasema zama kwenye maneno, ndio maana Masheikh wazamani walikua wakichambua aya moja kwa siku nzima.
Sasa midamu umegonga Mlango na mimi ntakufungulia uchungulie ndani kidogo uone raha ya kufahamu, katika hiyo aya kumetajwa maneno mawili ambayo ndio tutozama nayo katika darsa hii yatuoneshe hiyo njia ya kumkumbuka Allah, Sasa itizame uzuri hiyo aya inasema neno la kwanza (kumkumbuka)halafu neno la pili(Kufikiri).
Naam Kumkumbuka ni lazima, Kukumbuka ndio (Nature)yako, Unalala unaamka, unasimama, unakaa yote hayo yanatokana na Amri ya Mwenye Enzi Mungu katika Rehma zake, huna haja ya kukumbuka mie niko hai, halafu tena unapewa nafasi ya kuchagua, Ukichagua Kumkumbuka Mollah alokufanyia hayo, hiyo ndio Pepo yako, Na ukichagua Mengine hayo ndio yanokupeleka kwenye moto wako, Sote tuko kwenye Ufalme wa Mwenye Enzi Mungu, ila katupa Uhuru, Uhuru wenyewe ndio huo uwezo wa (Kufikiri)Ambao linaingia neno la Pili.
Fikira ni tendo linohusiana na Akili au (Mind)yako, Akili ina desturi ya kuzunguka au niseme ina athari za (Rebellious), ndio maana utaona ukitaka kusali tu, inaanza kukuletea visa, unapanga biashara, unakumbuka mambo yote ulosahau, kwa sababu ya Athari zilezile za maasi, kwa hiyo ikiona unataka kutenda mema inakurejesha kule kule kwenye mabaya, ukitoka kusali inakukumbusha mpira, wanawake au wanaume, dhuluma, siasa fujo tupu hilo ndio linakufanya huwezi Kumkumbuka Mollah wako ukiwa unasali, umesimama au umekaa hata wakati umelala. Sasa hao walotajwa kwenye hiyo aya wamefanya nini hata wakapata mawili hayo?.
Endelea part 2

NJIA YA KUMKUMBUKA ALLAH PART 2

Asalaam Aleiykum

Katika Dunia hii kila kitu kimeumbwa na mwenzake kuifahamu njia ya kumkumbuka Allah kwanza lazima uijue sheria ya (Foward)na (Reverse Affect)katika Akili yako. Tizama wewe inakuaje ukikatazwa kitu unavokua, au umwambie mtu jambo asiseme uone anavohangaika kulitangaza, na hivyo hivyo Ukijifanya, na sema Ukijifanya unataka kuwa Mcha Mungu jiangalie  vipi ukatili, au ubaya unavyo kuzunguka katika Roho yako, Watizame hao wanojifanya watu wa dini wanavokua, nini hali zao, sisemi kitu angalia mwenyewe halafu utapata jawabu, usitizame makanzu yao angalia huyu hana (Reverse affect)kama hana basi huyo Mcha Mungu.
Yote hayo yanatokana na hiyo sheria niloitaja hapo juu, Kwa hiyo ukitaka Kumkumbuka Allah lazima uende (Beyond) ya Sheria hiyo, vipi utafanya?. Jambo la kwanza unatakiwa kuishughulisha Akili yako wakati wote iwe katika Kumfikiri Mollah wako katika mambo ya Uhai na Umauti, Na katika Ulimwengu huu sidhani kama utavimaliza vitu vyote katika kuitizama Neema na Rehma ya Mwenye Enzi Mungu alojaza katika Umbaji wake, iwe kila ukionacho basi kinakukumbusha Mollah wako, ukifanikiwa kufanya hivyo ndio utajiunga na walotajwa katika hiyo aya niloitaja hapo mwanzo, utakua na wewe unamkumbuka na kumfikiri kwa wakati mmoja, sio ukiona mbuzi unamkumbuka Mollah wako na ukiona Mbwa unakamata jiwe, hapo itakua kumbukumbuka ishakupotea, na utakua ni mwenye kupotea njia.
Ukifanikiwa kudumu kwa kila unachokiona kina kukumbusha uwezo wa Mwenye enzi Mungu hapo utakua umeiweza Akili, Na ukiiweza Akili unabaki kwenye kukumbuka na wewe unajiunga katika Waja walotajwa katika sura ya Furqan aya ya (63-64)

"وَعِبَادُ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلَّذِينَ يَمۡشُونَ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ هَوۡنً۬ا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ ٱلۡجَـٰهِلُونَ قَالُواْ سَلَـٰمً۬ا"
Na Waja wa Mwenye Enzi Mungu ni wale wanaokwenda Ulimwenguni kwa Unyenyekevu, Na Wajinga wakisema nao huwajibu Salama.
"وَٱلَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمۡ سُجَّدً۬ا وَقِيَـٰمً۬ا"
Na Wale wanaopitisha baadhi ya (Nyakati)saa za usiku kwa ajili ya Mollah wao kwa kusujudu na Kusimama.
Kwanini wakaitwa Waja wa Mwenye enzi Mungu kwa sababu saa zote wako na Mollah wao, hakiingi chengine kati yao, washafunguliwa siri za mambo, wanageuka kuwa wanyenyekevu, wanajua sisi hatuna cha kumlipa Mollah wetu, tumeletwa katika dunia hii kuhakikisha tunamkumbuka Mollah wetu wakati wote, Na ndio wakikutana na wasojua(Wajinga)wanawapa ishara ya huku kwetu Salama tupu, Na nyinyi chagueni kumkumbuka Allah mtaipata salama hiyo(Hawagombani nao)hawana mabishano neno lao ni usalama, na hiyo ndio sifa ya (Muumin)(Peace)Upande wa Mungu hakuna dhuluma, hakuna kutaka pesa, hakuna mabishano wala chuki, ukiona unayo mambo hayo basi jijue bado uko upande wa (Shetani) na endelea kumkumbuka shetani wako.
Na Mollah wako akijaa katika Akili yako huwezi kulala mpaka asubuhi bila ya kusujudu na kusimama kwa ajili yake, yeye ndie mwenye kukupa usingizi, Na mchana kutwa ulikua umeshughulika na maisha, kwa hiyo sasa usiku umeingia ni wakati mzuri wa kusimama kusema na Mollah wako na Ku(Surrender)kuanguka kwa ajili ya Sujjud.
Endelea  Part 3

NJIA YA KUMKUMBUKA ALLAH PART 3

Asalaam Aleiykum

Amesema Mwenye Enzi Mungu katika sura ya (Adh-Dhariyat-56)"وَمَا خَلَقۡتُ ٱلۡجِنَّ وَٱلۡإِنسَ إِلَّا لِيَعۡبُدُونِ"
"Sikuwaumba Majini na Watu ila wapate kuniabudu"
Sikuwaumba kwa ajili yoyote, ila nimewapa (Choice)wakitaka waniabudu watakua wamechagua Pepo wenyewe, Na wasipotaka na kukataa watakua wamechagua njia yao itakayo wapeleka kwenye mateso, kwani kwenda kinyume cha Maumbile(Nature)ya Ulimwengu huu utakua umechagua kinyume na atakavyo alokuumba.
Sasa kuipata hiyo Ibada yenyewe lazima uviunganishe vitu viwili nilivyovitaja vya Fikra na Kukumbuka yaani (Roho Na Akili) Vikiungana hivyo ndio unapata huo Unyenyekevu, Akili haiyumbi tena, Vipi Akili itayumba wakati daima uko mbele ya Mollah wako, Na Mbele ya Mollah lazima upate na Unyenyekevu, Na huku Duniani wakikuona wanahisi kuna kitu (kimetokezea)ndio wakikuuliza kitu mbona imekua hivi, au wakibishana na wewe huna la kusema ila unawaambia Salaam(Peace).
Kwa habari hii nilokupeni na ikiwa umeipokea sawa sawa na sasa na wewe unataka kuanza kuipata hali kama hiyo, Basi chukua moja katika majina 99 ya Mwenye Enzi Mungu halafu litaje (Non Stop) kwa miezi mitatu ikisha (Stop) baada ya hapo ndio utafunguliwa hiyo (Nameless) ya kukumbuka daima, Nje utakua Binaadamu wa kawaida lakini ndani kiumbe mwengine kabisa, kila kitu kinafunguliwa kwako, na ukiipata hali kama hiyo utakua ushaipata hiyo njia, Na njia hiyo ndio hiyo inotajwa (Mustaqim)ambayo inakupeleka kwa Mollah wako ukiwa safi umesafishika na dhanmbi zote ulizozifanya huko nyuma. Na Mollah ndie ajuae zaidi.