Asalaam Aleiykum
Katika Dunia hii kila kitu kimeumbwa na mwenzake kuifahamu njia ya kumkumbuka Allah kwanza lazima uijue sheria ya (Foward)na (Reverse Affect)katika Akili yako. Tizama wewe inakuaje ukikatazwa kitu unavokua, au umwambie mtu jambo asiseme uone anavohangaika kulitangaza, na hivyo hivyo Ukijifanya, na sema Ukijifanya unataka kuwa Mcha Mungu jiangalie vipi ukatili, au ubaya unavyo kuzunguka katika Roho yako, Watizame hao wanojifanya watu wa dini wanavokua, nini hali zao, sisemi kitu angalia mwenyewe halafu utapata jawabu, usitizame makanzu yao angalia huyu hana (Reverse affect)kama hana basi huyo Mcha Mungu.
Yote hayo yanatokana na hiyo sheria niloitaja hapo juu, Kwa hiyo ukitaka Kumkumbuka Allah lazima uende (Beyond) ya Sheria hiyo, vipi utafanya?. Jambo la kwanza unatakiwa kuishughulisha Akili yako wakati wote iwe katika Kumfikiri Mollah wako katika mambo ya Uhai na Umauti, Na katika Ulimwengu huu sidhani kama utavimaliza vitu vyote katika kuitizama Neema na Rehma ya Mwenye Enzi Mungu alojaza katika Umbaji wake, iwe kila ukionacho basi kinakukumbusha Mollah wako, ukifanikiwa kufanya hivyo ndio utajiunga na walotajwa katika hiyo aya niloitaja hapo mwanzo, utakua na wewe unamkumbuka na kumfikiri kwa wakati mmoja, sio ukiona mbuzi unamkumbuka Mollah wako na ukiona Mbwa unakamata jiwe, hapo itakua kumbukumbuka ishakupotea, na utakua ni mwenye kupotea njia.
Ukifanikiwa kudumu kwa kila unachokiona kina kukumbusha uwezo wa Mwenye enzi Mungu hapo utakua umeiweza Akili, Na ukiiweza Akili unabaki kwenye kukumbuka na wewe unajiunga katika Waja walotajwa katika sura ya Furqan aya ya (63-64)
"وَعِبَادُ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلَّذِينَ يَمۡشُونَ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ هَوۡنً۬ا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ ٱلۡجَـٰهِلُونَ قَالُواْ سَلَـٰمً۬ا"
Na Waja wa Mwenye Enzi Mungu ni wale wanaokwenda Ulimwenguni kwa Unyenyekevu, Na Wajinga wakisema nao huwajibu Salama.
"وَٱلَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمۡ سُجَّدً۬ا وَقِيَـٰمً۬ا"
Na Wale wanaopitisha baadhi ya (Nyakati)saa za usiku kwa ajili ya Mollah wao kwa kusujudu na Kusimama.
Kwanini wakaitwa Waja wa Mwenye enzi Mungu kwa sababu saa zote wako na Mollah wao, hakiingi chengine kati yao, washafunguliwa siri za mambo, wanageuka kuwa wanyenyekevu, wanajua sisi hatuna cha kumlipa Mollah wetu, tumeletwa katika dunia hii kuhakikisha tunamkumbuka Mollah wetu wakati wote, Na ndio wakikutana na wasojua(Wajinga)wanawapa ishara ya huku kwetu Salama tupu, Na nyinyi chagueni kumkumbuka Allah mtaipata salama hiyo(Hawagombani nao)hawana mabishano neno lao ni usalama, na hiyo ndio sifa ya (Muumin)(Peace)Upande wa Mungu hakuna dhuluma, hakuna kutaka pesa, hakuna mabishano wala chuki, ukiona unayo mambo hayo basi jijue bado uko upande wa (Shetani) na endelea kumkumbuka shetani wako.
Na Mollah wako akijaa katika Akili yako huwezi kulala mpaka asubuhi bila ya kusujudu na kusimama kwa ajili yake, yeye ndie mwenye kukupa usingizi, Na mchana kutwa ulikua umeshughulika na maisha, kwa hiyo sasa usiku umeingia ni wakati mzuri wa kusimama kusema na Mollah wako na Ku(Surrender)kuanguka kwa ajili ya Sujjud.
Endelea Part 3
No comments:
Post a Comment