Wednesday, November 1, 2017

NJIA YA KUMKUMBUKA ALLAH PART 1

Asalaam Aleiykum

Mnaniuliza vipi kumkumbuka Allah mbona sisi inatushinda inakuaje hali hiyo, Mbona hatuwezi wakati tunajitahidi?, Anapouliza Mja swali kama hili ajijue kashafika mlangoni, huyu anataka afunguliwe, sasa anagonga katokea mbali, kapanda milima na  kupita kwenye majangwa mpaka kuwasili kutaka kujua kitu Adhimu kama hicho.
Siku zote wanasikia aya ya (191)sura ya (Al-Imran)inosema:

"ٱلَّذِينَ يَذۡكُرُونَ ٱللَّهَ قِيَـٰمً۬ا وَقُعُودً۬ا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمۡ وَيَتَفَڪَّرُونَ فِى خَلۡقِ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ رَبَّنَا مَا خَلَقۡتَ هَـٰذَا بَـٰطِلاً۬ سُبۡحَـٰنَكَ فَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ"
"Ambao humkumbuka Mwenye Enzi Mungu Wakiwa Wima na Wakikaa na Wakilala, Na Hufikiri Umbo la Mbingu na Ardhi, (Wakasema)Mollah wetu huku viumba hivi bure, Utukufu ni wako, basi tuepushe na adhabu ya Moto".
Kwanza kabisa nataka kufundisha vipi utazama kwenye neno, ukitaka kuzama kwenye neno lazima ujiulize kwanini likawepo hapo, nikisema kuwepo hapo sina maana nyengine ila kutizama mashiko yake, mashiko yanayo onekana hapo ni kutajwa vitu viwili ambavyo wewe huvioni, ndio maana nikasema zama kwenye maneno, ndio maana Masheikh wazamani walikua wakichambua aya moja kwa siku nzima.
Sasa midamu umegonga Mlango na mimi ntakufungulia uchungulie ndani kidogo uone raha ya kufahamu, katika hiyo aya kumetajwa maneno mawili ambayo ndio tutozama nayo katika darsa hii yatuoneshe hiyo njia ya kumkumbuka Allah, Sasa itizame uzuri hiyo aya inasema neno la kwanza (kumkumbuka)halafu neno la pili(Kufikiri).
Naam Kumkumbuka ni lazima, Kukumbuka ndio (Nature)yako, Unalala unaamka, unasimama, unakaa yote hayo yanatokana na Amri ya Mwenye Enzi Mungu katika Rehma zake, huna haja ya kukumbuka mie niko hai, halafu tena unapewa nafasi ya kuchagua, Ukichagua Kumkumbuka Mollah alokufanyia hayo, hiyo ndio Pepo yako, Na ukichagua Mengine hayo ndio yanokupeleka kwenye moto wako, Sote tuko kwenye Ufalme wa Mwenye Enzi Mungu, ila katupa Uhuru, Uhuru wenyewe ndio huo uwezo wa (Kufikiri)Ambao linaingia neno la Pili.
Fikira ni tendo linohusiana na Akili au (Mind)yako, Akili ina desturi ya kuzunguka au niseme ina athari za (Rebellious), ndio maana utaona ukitaka kusali tu, inaanza kukuletea visa, unapanga biashara, unakumbuka mambo yote ulosahau, kwa sababu ya Athari zilezile za maasi, kwa hiyo ikiona unataka kutenda mema inakurejesha kule kule kwenye mabaya, ukitoka kusali inakukumbusha mpira, wanawake au wanaume, dhuluma, siasa fujo tupu hilo ndio linakufanya huwezi Kumkumbuka Mollah wako ukiwa unasali, umesimama au umekaa hata wakati umelala. Sasa hao walotajwa kwenye hiyo aya wamefanya nini hata wakapata mawili hayo?.
Endelea part 2

No comments:

Post a Comment