Asalaam Aleiykum
Aya ikaendelea na maneno haya:
"Nuru juu ya nuru Mwenye enzi Mungu humuongoza katika Nuru yake amtakaye, Na Mwenye enzi Mungu hupiga mifano kwa watu, Na Mwenye enzi Mungu ni mjuzi wa kila kitu".
Aliposema anapiga mifano kwa watu ili kutueleza sisi Wanaadamu uwezo wa elimu yake na miujiza iliyopo katika hiyo Taa aliyoumba,
(Let There Be Light)
Inaendelea Miujiza hii kutufata kwanza imeanzia Kwenye Mbingu na Ardhi na sasa imetufata katika Nafsi, Anasema Mollah Humuongoza Katika Nuru yake amtakaye, Ipi nuru ilokusudiwa hapo?, Ama zile za kuifata Nyota tunazijua, Napenda kukumbusha kuwa sisi hatuoni Nuru(Light)ila tunaona vinavomurikwa na Nuru, Humuongoza katika Nuru yake amtakaye, Nuru katika nafsi inagawika katika aina mbili ile aina ya kwanza ni (Inner light) wacha niitolee mfano, kwa sababu hujapata kuiona hiyo (Inner Light)lakini unaijua, vipi utaijua hii (light). Jichukue Mwenyewe uende sehemu ya kiza kikubwa uwe huoni chochote, Katika kiza hicho kuna kitu kimoja utakua na hakika nacho kipo, Na hakuna kitu chengine isipokua wewe Mwenyewe, Kwa mfano huo ni lazima iwepo (Light) Ya kukufahamisha kuwa wewe upo, kumbuka kwenye kiza hakionekani kitu chochote, sasa vipi wewe unajiona kama upo?, Lazima una (Inner Light) ndio ukaweza kujiona, Wewe Mwenyewe (Light)tupu kuanzia kuumbwa kwako, Ikiwa Ulimwengu Umeumbwa kwa (Light), Na Ardhi hii ndio umeumbwa nayo wewe(What is You)Jiulize Mwenyewe, Ukifanya Uchunguzi ukenda (Deep)ndani ya Maumbile yako utakutana nayo hiyo Taa pasina shaka, Jitizame juu juu tu utaona Jambo la Mwanzo unaanza na (Spina cord, nerve,heart)vyote hivyo ni (Form of Light), Akili yako inafanya kazi kutumia hiyo (Light), hiyo ndio (Inner light) ya Nafsi yako, lakini bado (light) hiyo haina (Movement)yoyote imekaa ndani ya Mwili wako mpaka ipate (Guidance) Hapo ndio yanaingia yale maneno ya "Humuongoza amtakaye kwenye (Nuru)Taa yake.(Baqarah-257)
ٱللَّهُ وَلِىُّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يُخۡرِجُهُم مِّنَ ٱلظُّلُمَـٰتِ إِلَى ٱلنُّورِۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَوۡلِيَآؤُهُمُ ٱلطَّـٰغُوتُ يُخۡرِجُونَهُم مِّنَ ٱلنُّورِ إِلَى ٱلظُّلُمَـٰتِۗ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ أَصۡحَـٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيہَا خَـٰلِدُونَ
"Mwenye Enzi Mungu ni Mlinzi wa wale Walioamini", Huwatoa katika giza na kuwaingiza katika Mwangaza, Lakini waliokufuru, walinzi wao ni Mashetani, huwatoa katika Mwangaza na kuwaingiza katika giza, hao ndio watu wa Motoni humo watakaa motoni".
Mwangaza ni (Outer light) ni (Nature) Ya Ulimwengu huu hakuna makosa kila kitu kiko kwenye (Parfection)Yake, sasa kwa kuwa wewe Mwanaadamu unafahamishwa hizo elimu zote ili upate kuijua (Light) Na kama wewe Muumin unaoneshwa fanya hivi, vile usifanye, hii itakudhuru, ile ina madhara, unamurikiwa mambo yote kwa ukamilifu, ukishayaona ukatulia katika Mwangaza wa (Consciouness)yako hapo ndio unapata (Affect)ya hiyo Nuru, Na hiyo ndio Ibada, huo ndio muongozo , yaani lazima uzame katika hiyo Taa, Lazima zikutane taa hizi mbili ya ndani na ya nje, ukiingia katika (Full Light) huo ndio Ucha Mungu, hapo ndio unasafishika na kila giza katika maisha yako.
"Lakini Mashetani kazi yao wao kukutoa kwenye hii Taa na kukupeleka kwenye giza, Na hilo giza kwa kuwa huoni basi utatumbukia motoni milele.
Na Dalili za giza unaziona hapa hapa Ulimwenguni, huna furaha, maisha tafran, mambo hayendi,kutwa unawaza magonjwa, huyaoni mazuri ya dunia hii kabisa, hata ufanyiwe nini huna raha kabisa, na hiyo ni dalili yakuwa taa yako ina sinzia, karibu itazimika, Iwashe kwa Ibada upate kuona mazuri ya Ulimwengu huu na Akiba yako ya Akhera. Zama Kwenye Miujiza Ya Taa, nayo itakuonesha mambo mengi yalofichika katika giza la Ulimwengu huu, Na ukipata hilo ndio umepata hicho kitu kiitwacho (Bliss)Na wewe sasa umegeuka kuwa Taa.
No comments:
Post a Comment