Asalaam Aleiykum
Tumeingia ndani ya mwezi wa (December), ama kwa sisi wenye kuishi nchi za ulaya tunafahamu vipi kiza kinavo utawala mchana wetu, Sio kuwa mchana unakua mfupi tu, Bali hata Akili zetu zinafunikwa na huzuni ya kuikosa Taa hii ya jua ambayo ndio tegemezi ya mchangamko wa furaha. Madhara ya kukosa jua yanajulikana na yako mengi lakini leo hapa sio uwanja wake wa kuyazungumza, leo ni siku ya Taa, tunataka tujue siri zake taa ili tupate faida mbili tatu za hichi kitu kiitwacho (Taa au Nuru).
Nini Taa?
Kulijibu swali hili itabidi tutafute baadhi ya mashiko yenye kuhusiana na Taa, Taa au Nuru Hakuna Mwenye kuijua, wala aliyeiona, au atakae iona, huo ndio Muujiza katika miujiza mingi ya Taa. Hakuna sehemu nzuri ilipozungumzwa Taa kama katika sura ya (Noor aya ya 35)
"ٱللَّهُ نُورُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ مَثَلُ نُورِهِۦ كَمِشۡكَوٰةٍ۬ فِيہَا مِصۡبَاحٌۖ ٱلۡمِصۡبَاحُ فِى زُجَاجَةٍۖ ٱلزُّجَاجَةُ كَأَنَّہَا كَوۡكَبٌ۬ دُرِّىٌّ۬ يُوقَدُ مِن شَجَرَةٍ۬ مُّبَـٰرَڪَةٍ۬ زَيۡتُونَةٍ۬ لَّا شَرۡقِيَّةٍ۬ وَلَا غَرۡبِيَّةٍ۬ يَكَادُ زَيۡتُہَا يُضِىٓءُ وَلَوۡ لَمۡ تَمۡسَسۡهُ نَارٌ۬ۚ نُّورٌ عَلَىٰ نُورٍ۬ۗ يَہۡدِى ٱللَّهُ لِنُورِهِۦ مَن يَشَآءُۚ وَيَضۡرِبُ ٱللَّهُ ٱلۡأَمۡثَـٰلَ لِلنَّاسِۗ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَىۡءٍ عَلِيمٌ۬"
"Mwenye enzi Mungu ni Nuru Ya Mbingu na Ardhi, Mfano wa Nuru yake ni kama Shubaka ndani yake (inakaa) Taa, Taa (ile imo)katika tungi(mfano Chemni)Tungi(Lile ni)ni kama nyota ingarayo, inayowashwa (Taa hiyo kwa mafuta yanayotoka)Katika Mti ulobarikiwa wa mzeituni, usio (Upande) wa Mashariki wala wa Magharibi, Yanakaribia mafuta yake kungara (Wenyewe) ingawa moto haujayagusa, Nuru juu ya nuru Mwenye enzi Mungu humuongoza katika Nuru yake amtakaye, Na Mwenye enzi Mungu hupiga mifano kwa watu, Na Mwenye enzi Mungu ni mjuzi wa kila kitu".
Naam tunaingia katika sayansi ya Quraan lazima uwe makini kukijua kinaelezwa nini ili upate kuifahamu darsa hii kwa ufanisi wa hali ya juu dhamira na makusudio yake ili upate kuijua faida ya Taa.
Aya inasema Mwenye enzi Mungu ni Nuru ya Mbingu na Ardhi, Kuna baadhi ya watu wakadhani hiyo Nuru ndio ufalme wenyewe kashajitaja.(Kumbuka Mollah wako hana alicho fanana nacho vipi fikra zako zikupeleke kwenye Nuru).Kumbuka kuna vitu viwili vimeumbwa kimoja tumeoneshwa chengine tumefichiwa na Muujiza wenyewe vyote hatuvijui mpaka leo, Cha mwanzo ni hiyo (Dark Matter)(Dhulumati)tunajua ipo (Kiza) lakini hatuwezi kukishika, Na hii (Light) hatujui ni kitu gani, tunachojua sisi kama Taa haipo kinatawala kiza, Taa ikiletwa kiza kinatoweka tunaona vilivyokua vimefunikwa wakati taa ilipoondokaa, Kwa hiyo Tunachojua sisi ni vile vinovyo murikwa na taa lakini hatuifahamu taa yenyewe.
Nini (Light)Taa.?
Endelea part 2
No comments:
Post a Comment