Saturday, December 2, 2017

MIUJIZA YA TAA PART 2

Asalaam Aleiykum

Sasa tuingie katika uchambuzi wa Nuru yenyewe ilivyo. katika utendaji wake kazi Mollah wetu akataja "Mfano wa Nuru yake ni kama shubaka" itabidi twende taratibu upate kunifahamu, ambayo imewekwa hiyo taa, taa hiyo imo kwenye tungi,(Kama chemni au hizi zenu za kisasa).
(1)Wanasayansi Wa Ulimwengu huu wanatwambia nini kuhusu Taa, Walipoifanyia Uchunguzi Taa wakasema cha kwanza kabisa Taa inasafiri kwa (Speed) kubwa kabisa ambayo hakuna kitu chengine chochote chenye kusafiri kuishinda taa, (Speed) yake ni (186,000).
(2)Taa ni kitu pekee kinacho safiri bila ya kutumia au kutegemea (Chombo)chengine kwa ajili ya kupatiwa nguvu, kwa Wale walosomea (Photon) wanajua nimekusudia nini, Kwa sababu kila kitu katika Ulimwengu huu kinategemea (Energy) isipokua Taa, Taa ni (Self-Energy)haitegemei msaada wowote,  Wewe Unaishi lakini unategemea msaada kutokea kwengine ili uweze kuishi lakini taa haina mahitaji hayo, ndio ikasemwa katika hiyo aya "yanakaribia Mafuta yake kungara" ingawa moto haujayagusa.
Kumbuka Wakati tunaendelea na darsa hii, hiyo aya ni mfano ulopigwa kuzungumzia hiyo (Nuru)Taa, lakini kadhia ya Taa inaenda (Deep) haikuishia hapo.
Lengine la muujiza kitu chengine chochote chenye kwenda (speed)hiyo ya Taa kinageuka kuwa Taa. Kwa hiyo hapo utaona ndio kwa mfano huo likaingia neno "Mwenye Enzi Mungu ni Nuru ya Mbingu na Ardhi" Ikiwa hatuijui, hatujapata kuiona, na wala hakuna atoiona sio kwamba tufahamu hiyo Nuru ni Mwenye enzi Mungu, bali ni mfano ulopigiwa huu Ulimwengu, Umeumbwa Ulimwengu huu kutokana na mambo hayo ya Muujiza niloyataja katika Darsa hii ikiwemo hiyo Nuru.Kwa maana hiyo kila kitu ni (Energy) Na (Energy)ndio hiyo(Light)  Na wala sio (Matter). Kwa hiyo tunaweza kusema (Matter) ni kitu kilichoambatanishwa au ufupisho wa (Light condense), ndio maana kikifikia (Speed)ya Taa kinarejea kwenye (Original)yake.
Na hiyo ndio maana ya Nuru juu ya Nuru, kila kitu ni (Light),Halafu muujiza mwengine kuwa (Light) haina haja ya kutegemea kuishi, Kama kila kitu kinavotegemea Maji kuishi, kama alivosema Mwenye Enzi Mungu "Tukajaalia kila chenye kuishi maji ndio kuwa chanzo chake"(sura ya Al-Anbiyaa aya ya 30)

وَلَمۡ يَرَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ ڪَانَتَا رَتۡقً۬ا فَفَتَقۡنَـٰهُمَا‌ۖ وَجَعَلۡنَا مِنَ ٱلۡمَآءِ كُلَّ شَىۡءٍ حَىٍّ‌ۖ أَفَلَا يُؤۡمِنُونَ
"Jee Hawakuona wale waliokufuru ya kwamba mbingu na ardhi vilikuwa vimeambatana, kisha tukaviambua(Big bang). Na tukafanya kwa maji kila kitu kilicho hai, basi jee hawaamini".
Kila chenye Uhai kimefanywa na Maji ila Taa, Kwa hiyo utaona Maji yanaitegemea Taa, lakini Taa haitegemei maji, Nayo hiyo Taa inakwenda (Beyond)Uhai. Kwa hiyo hapo utaelewa Taa inaishi bila ya Uhai(Self Existence). Kila kitu kinaweza kuyayuka isipokua Taa haiwezi kuguswa na chochote kile, Isipokua Taa ikizimika basi kila kitu kitakufa katika Ulimwengu huu ikiwemo hayo maji.

Endelea part 3



No comments:

Post a Comment