Asalaam Aleiykum
Tumeingia ndani ya mwezi wa (December), ama kwa sisi wenye kuishi nchi za ulaya tunafahamu vipi kiza kinavo utawala mchana wetu, Sio kuwa mchana unakua mfupi tu, Bali hata Akili zetu zinafunikwa na huzuni ya kuikosa Taa hii ya jua ambayo ndio tegemezi ya mchangamko wa furaha. Madhara ya kukosa jua yanajulikana na yako mengi lakini leo hapa sio uwanja wake wa kuyazungumza, leo ni siku ya Taa, tunataka tujue siri zake taa ili tupate faida mbili tatu za hichi kitu kiitwacho (Taa au Nuru).
Nini Taa?
Kulijibu swali hili itabidi tutafute baadhi ya mashiko yenye kuhusiana na Taa, Taa au Nuru Hakuna Mwenye kuijua, wala aliyeiona, au atakae iona, huo ndio Muujiza katika miujiza mingi ya Taa. Hakuna sehemu nzuri ilipozungumzwa Taa kama katika sura ya (Noor aya ya 35)
"ٱللَّهُ نُورُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ مَثَلُ نُورِهِۦ كَمِشۡكَوٰةٍ۬ فِيہَا مِصۡبَاحٌۖ ٱلۡمِصۡبَاحُ فِى زُجَاجَةٍۖ ٱلزُّجَاجَةُ كَأَنَّہَا كَوۡكَبٌ۬ دُرِّىٌّ۬ يُوقَدُ مِن شَجَرَةٍ۬ مُّبَـٰرَڪَةٍ۬ زَيۡتُونَةٍ۬ لَّا شَرۡقِيَّةٍ۬ وَلَا غَرۡبِيَّةٍ۬ يَكَادُ زَيۡتُہَا يُضِىٓءُ وَلَوۡ لَمۡ تَمۡسَسۡهُ نَارٌ۬ۚ نُّورٌ عَلَىٰ نُورٍ۬ۗ يَہۡدِى ٱللَّهُ لِنُورِهِۦ مَن يَشَآءُۚ وَيَضۡرِبُ ٱللَّهُ ٱلۡأَمۡثَـٰلَ لِلنَّاسِۗ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَىۡءٍ عَلِيمٌ۬"
"Mwenye enzi Mungu ni Nuru Ya Mbingu na Ardhi, Mfano wa Nuru yake ni kama Shubaka ndani yake (inakaa) Taa, Taa (ile imo)katika tungi(mfano Chemni)Tungi(Lile ni)ni kama nyota ingarayo, inayowashwa (Taa hiyo kwa mafuta yanayotoka)Katika Mti ulobarikiwa wa mzeituni, usio (Upande) wa Mashariki wala wa Magharibi, Yanakaribia mafuta yake kungara (Wenyewe) ingawa moto haujayagusa, Nuru juu ya nuru Mwenye enzi Mungu humuongoza katika Nuru yake amtakaye, Na Mwenye enzi Mungu hupiga mifano kwa watu, Na Mwenye enzi Mungu ni mjuzi wa kila kitu".
Naam tunaingia katika sayansi ya Quraan lazima uwe makini kukijua kinaelezwa nini ili upate kuifahamu darsa hii kwa ufanisi wa hali ya juu dhamira na makusudio yake ili upate kuijua faida ya Taa.
Aya inasema Mwenye enzi Mungu ni Nuru ya Mbingu na Ardhi, Kuna baadhi ya watu wakadhani hiyo Nuru ndio ufalme wenyewe kashajitaja.(Kumbuka Mollah wako hana alicho fanana nacho vipi fikra zako zikupeleke kwenye Nuru).Kumbuka kuna vitu viwili vimeumbwa kimoja tumeoneshwa chengine tumefichiwa na Muujiza wenyewe vyote hatuvijui mpaka leo, Cha mwanzo ni hiyo (Dark Matter)(Dhulumati)tunajua ipo (Kiza) lakini hatuwezi kukishika, Na hii (Light) hatujui ni kitu gani, tunachojua sisi kama Taa haipo kinatawala kiza, Taa ikiletwa kiza kinatoweka tunaona vilivyokua vimefunikwa wakati taa ilipoondokaa, Kwa hiyo Tunachojua sisi ni vile vinovyo murikwa na taa lakini hatuifahamu taa yenyewe.
Nini (Light)Taa.?
Endelea part 2
Saturday, December 2, 2017
MIUJIZA YA TAA PART 2
Asalaam Aleiykum
Sasa tuingie katika uchambuzi wa Nuru yenyewe ilivyo. katika utendaji wake kazi Mollah wetu akataja "Mfano wa Nuru yake ni kama shubaka" itabidi twende taratibu upate kunifahamu, ambayo imewekwa hiyo taa, taa hiyo imo kwenye tungi,(Kama chemni au hizi zenu za kisasa).
(1)Wanasayansi Wa Ulimwengu huu wanatwambia nini kuhusu Taa, Walipoifanyia Uchunguzi Taa wakasema cha kwanza kabisa Taa inasafiri kwa (Speed) kubwa kabisa ambayo hakuna kitu chengine chochote chenye kusafiri kuishinda taa, (Speed) yake ni (186,000).
(2)Taa ni kitu pekee kinacho safiri bila ya kutumia au kutegemea (Chombo)chengine kwa ajili ya kupatiwa nguvu, kwa Wale walosomea (Photon) wanajua nimekusudia nini, Kwa sababu kila kitu katika Ulimwengu huu kinategemea (Energy) isipokua Taa, Taa ni (Self-Energy)haitegemei msaada wowote, Wewe Unaishi lakini unategemea msaada kutokea kwengine ili uweze kuishi lakini taa haina mahitaji hayo, ndio ikasemwa katika hiyo aya "yanakaribia Mafuta yake kungara" ingawa moto haujayagusa.
Kumbuka Wakati tunaendelea na darsa hii, hiyo aya ni mfano ulopigwa kuzungumzia hiyo (Nuru)Taa, lakini kadhia ya Taa inaenda (Deep) haikuishia hapo.
Lengine la muujiza kitu chengine chochote chenye kwenda (speed)hiyo ya Taa kinageuka kuwa Taa. Kwa hiyo hapo utaona ndio kwa mfano huo likaingia neno "Mwenye Enzi Mungu ni Nuru ya Mbingu na Ardhi" Ikiwa hatuijui, hatujapata kuiona, na wala hakuna atoiona sio kwamba tufahamu hiyo Nuru ni Mwenye enzi Mungu, bali ni mfano ulopigiwa huu Ulimwengu, Umeumbwa Ulimwengu huu kutokana na mambo hayo ya Muujiza niloyataja katika Darsa hii ikiwemo hiyo Nuru.Kwa maana hiyo kila kitu ni (Energy) Na (Energy)ndio hiyo(Light) Na wala sio (Matter). Kwa hiyo tunaweza kusema (Matter) ni kitu kilichoambatanishwa au ufupisho wa (Light condense), ndio maana kikifikia (Speed)ya Taa kinarejea kwenye (Original)yake.
Na hiyo ndio maana ya Nuru juu ya Nuru, kila kitu ni (Light),Halafu muujiza mwengine kuwa (Light) haina haja ya kutegemea kuishi, Kama kila kitu kinavotegemea Maji kuishi, kama alivosema Mwenye Enzi Mungu "Tukajaalia kila chenye kuishi maji ndio kuwa chanzo chake"(sura ya Al-Anbiyaa aya ya 30)
وَلَمۡ يَرَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ ڪَانَتَا رَتۡقً۬ا فَفَتَقۡنَـٰهُمَاۖ وَجَعَلۡنَا مِنَ ٱلۡمَآءِ كُلَّ شَىۡءٍ حَىٍّۖ أَفَلَا يُؤۡمِنُونَ
"Jee Hawakuona wale waliokufuru ya kwamba mbingu na ardhi vilikuwa vimeambatana, kisha tukaviambua(Big bang). Na tukafanya kwa maji kila kitu kilicho hai, basi jee hawaamini".
Kila chenye Uhai kimefanywa na Maji ila Taa, Kwa hiyo utaona Maji yanaitegemea Taa, lakini Taa haitegemei maji, Nayo hiyo Taa inakwenda (Beyond)Uhai. Kwa hiyo hapo utaelewa Taa inaishi bila ya Uhai(Self Existence). Kila kitu kinaweza kuyayuka isipokua Taa haiwezi kuguswa na chochote kile, Isipokua Taa ikizimika basi kila kitu kitakufa katika Ulimwengu huu ikiwemo hayo maji.
Endelea part 3

MIUJIZA YA TAA PART 3
Asalaam Aleiykum
Aya ikaendelea na maneno haya:
"Nuru juu ya nuru Mwenye enzi Mungu humuongoza katika Nuru yake amtakaye, Na Mwenye enzi Mungu hupiga mifano kwa watu, Na Mwenye enzi Mungu ni mjuzi wa kila kitu".
Aliposema anapiga mifano kwa watu ili kutueleza sisi Wanaadamu uwezo wa elimu yake na miujiza iliyopo katika hiyo Taa aliyoumba,
(Let There Be Light)
Inaendelea Miujiza hii kutufata kwanza imeanzia Kwenye Mbingu na Ardhi na sasa imetufata katika Nafsi, Anasema Mollah Humuongoza Katika Nuru yake amtakaye, Ipi nuru ilokusudiwa hapo?, Ama zile za kuifata Nyota tunazijua, Napenda kukumbusha kuwa sisi hatuoni Nuru(Light)ila tunaona vinavomurikwa na Nuru, Humuongoza katika Nuru yake amtakaye, Nuru katika nafsi inagawika katika aina mbili ile aina ya kwanza ni (Inner light) wacha niitolee mfano, kwa sababu hujapata kuiona hiyo (Inner Light)lakini unaijua, vipi utaijua hii (light). Jichukue Mwenyewe uende sehemu ya kiza kikubwa uwe huoni chochote, Katika kiza hicho kuna kitu kimoja utakua na hakika nacho kipo, Na hakuna kitu chengine isipokua wewe Mwenyewe, Kwa mfano huo ni lazima iwepo (Light) Ya kukufahamisha kuwa wewe upo, kumbuka kwenye kiza hakionekani kitu chochote, sasa vipi wewe unajiona kama upo?, Lazima una (Inner Light) ndio ukaweza kujiona, Wewe Mwenyewe (Light)tupu kuanzia kuumbwa kwako, Ikiwa Ulimwengu Umeumbwa kwa (Light), Na Ardhi hii ndio umeumbwa nayo wewe(What is You)Jiulize Mwenyewe, Ukifanya Uchunguzi ukenda (Deep)ndani ya Maumbile yako utakutana nayo hiyo Taa pasina shaka, Jitizame juu juu tu utaona Jambo la Mwanzo unaanza na (Spina cord, nerve,heart)vyote hivyo ni (Form of Light), Akili yako inafanya kazi kutumia hiyo (Light), hiyo ndio (Inner light) ya Nafsi yako, lakini bado (light) hiyo haina (Movement)yoyote imekaa ndani ya Mwili wako mpaka ipate (Guidance) Hapo ndio yanaingia yale maneno ya "Humuongoza amtakaye kwenye (Nuru)Taa yake.(Baqarah-257)
ٱللَّهُ وَلِىُّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يُخۡرِجُهُم مِّنَ ٱلظُّلُمَـٰتِ إِلَى ٱلنُّورِۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَوۡلِيَآؤُهُمُ ٱلطَّـٰغُوتُ يُخۡرِجُونَهُم مِّنَ ٱلنُّورِ إِلَى ٱلظُّلُمَـٰتِۗ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ أَصۡحَـٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيہَا خَـٰلِدُونَ
"Mwenye Enzi Mungu ni Mlinzi wa wale Walioamini", Huwatoa katika giza na kuwaingiza katika Mwangaza, Lakini waliokufuru, walinzi wao ni Mashetani, huwatoa katika Mwangaza na kuwaingiza katika giza, hao ndio watu wa Motoni humo watakaa motoni".
Mwangaza ni (Outer light) ni (Nature) Ya Ulimwengu huu hakuna makosa kila kitu kiko kwenye (Parfection)Yake, sasa kwa kuwa wewe Mwanaadamu unafahamishwa hizo elimu zote ili upate kuijua (Light) Na kama wewe Muumin unaoneshwa fanya hivi, vile usifanye, hii itakudhuru, ile ina madhara, unamurikiwa mambo yote kwa ukamilifu, ukishayaona ukatulia katika Mwangaza wa (Consciouness)yako hapo ndio unapata (Affect)ya hiyo Nuru, Na hiyo ndio Ibada, huo ndio muongozo , yaani lazima uzame katika hiyo Taa, Lazima zikutane taa hizi mbili ya ndani na ya nje, ukiingia katika (Full Light) huo ndio Ucha Mungu, hapo ndio unasafishika na kila giza katika maisha yako.
"Lakini Mashetani kazi yao wao kukutoa kwenye hii Taa na kukupeleka kwenye giza, Na hilo giza kwa kuwa huoni basi utatumbukia motoni milele.
Na Dalili za giza unaziona hapa hapa Ulimwenguni, huna furaha, maisha tafran, mambo hayendi,kutwa unawaza magonjwa, huyaoni mazuri ya dunia hii kabisa, hata ufanyiwe nini huna raha kabisa, na hiyo ni dalili yakuwa taa yako ina sinzia, karibu itazimika, Iwashe kwa Ibada upate kuona mazuri ya Ulimwengu huu na Akiba yako ya Akhera. Zama Kwenye Miujiza Ya Taa, nayo itakuonesha mambo mengi yalofichika katika giza la Ulimwengu huu, Na ukipata hilo ndio umepata hicho kitu kiitwacho (Bliss)Na wewe sasa umegeuka kuwa Taa.

Subscribe to:
Posts (Atom)